nilipoiona hii habari nikamshirikisha mwanamama fulani, aliumia sana. ila niliposoma aya ya mwisho nesi akijitetea kuwa alimchapa viboko viwili tu, ikabidi nimuulize. akanambia viboko vinaruhusiwa 'leba' kwa kuwa si kazi rahisi. mama anapojifungua, kama atakuwa mbishi kusukuma (kwa sababu ya maumivu) basi wanachapwa viboko kama viwili hivi mgongoni au mapajani. tulipoendelea kujadili akanambia inawezekana huyo nesi alitumia muda mrefu sana kushurutisha!
Kitendo hicho cha muuguzi kinaonesha namna gani baadhi ya wanawake wakiwa labour wanashindwa kufuata taratibu za kujifungua na kupelekea hatari kwa wao wenyewe na watoto. Mtoto akikosa hewa wakati wa kujifungua ujue unapokea 'tahira' au mwenye uwezo mdogo ki-akili, au kukua vibaya. Pili mtoto uweza kupoteza maisha.
Kwa woga huu baadhi ya wanawake wenye fedha wanakimbilia 'kisu' kitu ambacho kinamnyima mtoto ujasiri wa kuingia duniani kwa juhudi zake binafsi badala ya kuchopolewa utafikiri 'kongolo kutoka kwenye supu ya ng'ombe'. Sioni makosa ya mkunga kwani kumwacha yule mama mjazito na ujinga wake ni hatari, kumchapa imesaidia kwa kiasi fulani ingawaje si njia sahihi sana kimaadili.
Ninaandika haya kwa sababu uzembe kama huu wa mama mjazito nimeshuhudia labour kwa baadhi ya wamama wanaojifungua.
Waume wa wake wajawazito hakikisheni wake zenu wanazingatia taratibu zote za kujifungua na hakuna cha 'honey' kwenye jambo hilo!
Source: Muuguzi aliyemchapa viboko mjamzito asakwe - Swahilihub - mwananchi.co.tz
kuna mama kanambia ya kuwa viboko vinaruhusiwa (viwili tu, ila sio upande wa tumbo) maana shughuli ya kuzaa ni pevu, mama anaweza akagoma kabisa, so anachapwa ili afanye fasta. ila kwa huyo nesi atakuwa alizidisha ndiyo maana dogo akafia tumboni.
Inauma sana, Manesi muliomo humu badilikeni. Mimi ukinifanyia hivo kwa mke wangu lazima nikuwinde.
Taaluma na ugonjwa viko kati kati, sometimes yes sometimes no. Kudeka kunapipmwa vipi?
wamlipe fidia mhanga aliyefiwa na mtoto...
sio kwamba kwakuwa hana uwezo\elimu ndio atelekezwe.
dah! wanawake wana tabu sana aisee, tujitahidini kuwapenda na kuwaheshimu sana mana haya mambo ya uzazi yana complications sana.
Nawaheshimu sana wanawake.
Kama mkeo alikuwa hasukumi ulitaka nesi afanyeje ili kuokoa maisha?