Kashfa: Nesi amchapa Mjamzito Viboko, Kitoto Chafariki

Kashfa: Nesi amchapa Mjamzito Viboko, Kitoto Chafariki

Tuache masihara huyu anatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu, kwanza amlipe fidia mgonjwa na kifungo juu, utakujaje kazini umepigwa au umetukanwa na mumeo hasira uziamishie kwa mgonjwa? anatakiwa apewe adhabu kali ili fundisho kwa wengine.

Na mume wake achukuliwe hatua za kisheria kwa kumpiga na kumtusi mkewe (nurse) hivyo kumsababishia hasira zilizopelekea kumchapa mjamzito viboko!
 
kuna mama kanambia ya kuwa viboko vinaruhusiwa (viwili tu, ila sio upande wa tumbo) maana shughuli ya kuzaa ni pevu, mama anaweza akagoma kabisa, so anachapwa ili afanye fasta. ila kwa huyo nesi atakuwa alizidisha ndiyo maana dogo akafia tumboni.

Duh! Ina maana hii kanuni ya kuwalamba viboko iko hata Ulaya au ni hapa kwetu tu inatumika? Haikubaliki. Let us protest.
 
Pole sana ndugu yangu,nafurahi sana nikienda hospital nimkute mwanaume kuliko mwanamke hasa nikienda kujifungua,yaani unahudumiwa vizuri sana.

Wanaume hawana roho mbaya kama wanawake. Kwa kweli wana huruma. Sijui nini huwa kinawapata baadhi ya wanawake hata kuwa wakatili kiasi hicho.
 
Manesi ndivyo walivyo, binafsi nilishuhudia kwa macho yangu mwenzangu akipigwa makonde kisa eti anamchelewesha nesi anataka kwenda kulala japo na mimi nilikuwa nimesuswa kisa eti nililetwa Muhimbili nikitokea TMJ nilipokuwa nimelazwa hivyo wakawa wananiangalia pasipo hata kunihudumia huku wakinizodoa eti mnajifanya mna hela mnaenda TMJ mmeona huko yamewashinda ndiyo mnakuja huku. Waliniacha tokea usiku wa saa saba nikiwa na hali mbaya mpk kesho yake saa nane nilipoomba nipatiwe cm yangu na ku wapigia ndugu zangu nikiwaambia mimi nakufa taf nitafutieni Dr aje aniokoe. Walikuja ma dr watatu ndiyo walionizalisha na nilijifungua mtoto mfu. Ukweli huwa naumia sana, mpaka leo hii nikikumbuka huwa nalia sana! yaani manesi wamekuwa na roho mbaya sana utadhani hawana dini!!

Dah! Pole mwayego
 
Duh! Ina maana hii kanuni ya kuwalamba viboko iko hata Ulaya au ni hapa kwetu tu inatumika? Haikubaliki. Let us protest.

hahaha!!! kuchapwa viboko ni kanuni. kinamama wanasema unachapwa mgongoni au mapajani, ila sio kama kupiga mbwa. bila amasha-amsha kazi ya kuzaa inachukua muda mrefu ambapo yaweza leta hatari kwa mtoto au mama.
 
viboko mashuleni vimekatazwa sasa wengne wanataka kuhalalisha kwa wajawazito wenye uchungu...

hii hatari sana
 
Manesi ndivyo walivyo, binafsi nilishuhudia kwa macho yangu mwenzangu akipigwa makonde kisa eti anamchelewesha nesi anataka kwenda kulala japo na mimi nilikuwa nimesuswa kisa eti nililetwa Muhimbili nikitokea TMJ nilipokuwa nimelazwa hivyo wakawa wananiangalia pasipo hata kunihudumia huku wakinizodoa eti mnajifanya mna hela mnaenda TMJ mmeona huko yamewashinda ndiyo mnakuja huku. Waliniacha tokea usiku wa saa saba nikiwa na hali mbaya mpk kesho yake saa nane nilipoomba nipatiwe cm yangu na ku wapigia ndugu zangu nikiwaambia mimi nakufa taf nitafutieni Dr aje aniokoe. Walikuja ma dr watatu ndiyo walionizalisha na nilijifungua mtoto mfu. Ukweli huwa naumia sana, mpaka leo hii nikikumbuka huwa nalia sana! yaani manesi wamekuwa na roho mbaya sana utadhani hawana dini!!
Pole sana mama dah nimeumia moyoni walipaswa kukulipa fidia kwa huduma mbovu iliyopelekea mpaka mtoto wako kufariki.
 
Huyo nesi inabidi achukuliwe hatua za kisheria ingelikuwa mimi ni muhusika ningehakikisha anapoteza hio leseni yake ya unesi.Nimekwazika mno na kitendo chake!
 
hizi kanuni sio halali na zpo knyume na sheria

Kabisa kabisa. Shangaa Ulaya mwanamke anatoka hosp baada ya kujifungua anatembea untadhani ametoka dukani. Huku ni majanga, umechokaaa kwa sababu nesi anakuwa na haraka ya kuuza soksi na kofia, anakimbilia mikasi na kukusababishia stitches zisizokuwa na lazima, hata kama muda wa kujifungua bado. Unajiuguza mshono kwa muda mrefu na kukuathiri kwa kiasi kikubwa. Mengine hayafai kusema maana yanasikitisha. Oh Mothers...
 
Manesi ndivyo walivyo, binafsi nilishuhudia kwa macho yangu mwenzangu akipigwa makonde kisa eti anamchelewesha nesi anataka kwenda kulala japo na mimi nilikuwa nimesuswa kisa eti nililetwa Muhimbili nikitokea TMJ nilipokuwa nimelazwa hivyo wakawa wananiangalia pasipo hata kunihudumia huku wakinizodoa eti mnajifanya mna hela mnaenda TMJ mmeona huko yamewashinda ndiyo mnakuja huku. Waliniacha tokea usiku wa saa saba nikiwa na hali mbaya mpk kesho yake saa nane nilipoomba nipatiwe cm yangu na ku wapigia ndugu zangu nikiwaambia mimi nakufa taf nitafutieni Dr aje aniokoe. Walikuja ma dr watatu ndiyo walionizalisha na nilijifungua mtoto mfu. Ukweli huwa naumia sana, mpaka leo hii nikikumbuka huwa nalia sana! yaani manesi wamekuwa na roho mbaya sana utadhani hawana dini!!

pole sana mami...mi mwenzio almost nipoteze mtoto hospital ya st.kizito mikumi, manesi walikua wananishambulia nadeka, alafu kwanini nimezaa na 27yrs old (it was my first preg).. it was so frustrating walipoona kazi yangu ktk kadi yani chuki ikawajaa nilisemwa adi ikabidi niwachimbe biti..nikawaambia nikikosa mtoto wao watakosa vingi sana dah hatimae walikubali nifanyiwe oparesheni coz my baby was 4.6 na walikua wanang'ang'ania nipush wakat njia imegoma! I will never forget them
 
hahaha!!! kuchapwa viboko ni kanuni. kinamama wanasema unachapwa mgongoni au mapajani, ila sio kama kupiga mbwa. bila amasha-amsha kazi ya kuzaa inachukua muda mrefu ambapo yaweza leta hatari kwa mtoto au mama.

Mkuu are you serious?!, hii ni kweli kwenye hospitali zetu?!...please niambie unatania!
 
Manesi na makarani wa mahakama ni namba za kuchunga sana. sio wote lkn baadhi yao.

Anzisha Mada yako utapata mawazo mapya, nadhani una jambo la muhimu ila unalimalizia moyoni. Weka mambo hadharani tukusaidie.
 
Ni wakati wa uchungu wa kujifungua, Mtoto afia tumboni, hali ya mama utata.
Dodoma-25April2015.jpg

Dodoma.

Muuguzi mmoja wa zahanati ya Muungano, Chamwino, mkoani hapa, amekumbwa na kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama mjamzito, wakati akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha mtoto aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni.

Aidha, mama huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, hali yake inaelezwa kuwa mbaya. Mwanamke huyo, Mariamu Maroda, anadaiwa kulazwa kwenye chumba hicho kwa zaidi ya wiki moja, ambapo pamoja na kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata mtoto wake akiwa hai.

Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles, alisema Aprili 3, mwaka huu Saa 12:00 jioni, walimpeleka zahanati ya Muungano akiwa na dalili za kujifungua na kupokelewa na muuguzi aliyemfahamu kwa jina la Lucy. “Nilishuhudia Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia asimdhuru zaidi mwanangu, ila nilihuzunika sana,” alisema.

Alisema muuguzi huyo alitumia fimbo tatu kumchapa mgonjwa wake, ambazo alikuwa akizitumia kila moja inapovunjika. Alisema fimbo hizo zilipomalizika, alianza kumfinya kwenye mapaja kwa kutumia rula.

“Kesho yake saa 12:00 alfajiri, huku hali ya mgonjwa ikiwa mbaya, walitupatia gari likatupeleka hospitali ya Mvumi Misheni, ambako walisema hali aliyokuwa nayo mgonjwa wasingeiweza na kutuelekeza tumpeleke hospitali ya rufaa, lakini walimpa mgonjwa chupa mbili za damu,” alisema.

Alisema Maroda alifikishiwa chumba cha upasuaji na kisha alilazwa wodi namba 17, lakini miguu na tumbo vilianza kuvimba na alipochunguzwa ikabainika ana usaha tumboni, hivyo aliamriwa arudishwe kwenye chumba cha upasuaji. “Yaani ukimuona, mwilini ana alama za fimbo na kufinywa. Sasa walipomfanyia upasuaji kwa awamu ya pili, alipelekwa ICU mpaka hivi tunavyozungumza ni zaidi ya wiki moja,” alieleza Charles.

Viongozi wa Hospitali ya Rufaa, wenye mamlaka ya kuzungumzia suala hilo walionekana ‘kurushiana mpira’ walipotakiwa kuelezea suala hilo. Hata hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anatoria Mkindo, alikiri kuwepo kwa mgonjwa huyo.

Awali Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainab Chaula, alisema hakuwa na taarifa za kina kuhusu Maroda.
Mkindo alisema walikuwa wameagiza Ofisi ya Mganga wa Wilaya wa Chamwino, kuwapelekea taarifa kuhusu suala hilo. Alisema pia wametaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, ifahamishwe hatua zilizochukuliwa dhidi ya mtumishi aliyedaiwa kumchapa viboko mjamzito huyo.

“Mimi sio msemaji, anayetakiwa kuwapa taarifa kamili ni RMO (Chaula) kwanini awalete kwangu, nilichowaeleza ni ambacho nafahamu lakini siyo msemaji, nashauri muende ofisini kwa matroni wa hospitali mtapata taarifa kamili,” alisema.Afisa Muuguzi wa ICU, Christina Mlumba, alisema, Maroda alipelekwa ICU baada ya kufanyiwa upasuaji na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Mdogo wa Maroda, Silika Mkwawi alivieleza vyombo vya habari kuwa ingawa hakuingia kwenye chumba cha kujifu
ngulia katika zahanati ya muungano, dada yake alipotolewa nje, muuguzi alimueleza kuwa alimchapa fimbo mbili tu, kwa sababu ya kudeka kwake.

Chanzo:
Nipashe

Cha ajabu Regional Health Management Team(RHMT) haitasema lolote, usalama wa wilaya kimya, mkoa kimya....nk. sasa mwenyezi Mungu aingilie kati
 
Huyo nesi inabidi achukuliwe hatua za kisheria ingelikuwa mimi ni muhusika ningehakikisha anapoteza hio leseni yake ya unesi.Nimekwazika mno na kitendo chake!

Changamoto kwa serikali za kiafrika, nchi za wazungu wanatoa kipaumbele kwenye afya za Wananchi ndo mana tunakimbilia kutibiwa kwao, lakin nchi nyingi za Africa wauguzi ni wale manunda walioshindwa kuendelea na elimu ya sekondari, yaani ukifeli Kidato Cha Nne, hata usipokuwa na cheti, unachukua certificate of nursing, laboratory technician, midwifery etc. Hayo Ni Matokeo Yake.
 
Mkuu are you serious?!, hii ni kweli kwenye hospitali zetu?!...please niambie unatania!

nilipoiona hii habari nikamshirikisha mwanamama fulani, aliumia sana. ila niliposoma aya ya mwisho nesi akijitetea kuwa alimchapa viboko viwili tu, ikabidi nimuulize. akanambia viboko vinaruhusiwa 'leba' kwa kuwa si kazi rahisi. mama anapojifungua, kama atakuwa mbishi kusukuma (kwa sababu ya maumivu) basi wanachapwa viboko kama viwili hivi mgongoni au mapajani. tulipoendelea kujadili akanambia inawezekana huyo nesi alitumia muda mrefu sana kushurutisha!
 
  • Thanks
Reactions: kui
Changamoto kwa serikali za kiafrika, nchi za wazungu wanatoa kipaumbele kwenye afya ya mwananchi ndo mana tunakimbilia kutibiwa kwao, lakin nchi nyingi za Africa wauguzi ni wale manunda walioshindwa kuendelea na elimu ya sekondari, yaani ukifeli Kidato Cha Nne, hata usipokuwa na cheti, unachukua certificate of nursing, laboratory technician, midwifery etc. Hayo Ni Matokeo Yake.
Inasikitisha kwa kweli mzazi anatakiwa apewe encouragement akiwa anajifungua maskini mwanamke wawatu kapata mateso bure kwasababu akitaka kukipa kiumbe kingine uhai...Inabidi tanzania waweke vigezo vya juu zaidi kwa watu wanaotakiwa kusomea elimu ya unei na hizo fani nyingine jamani kwasababu hawa watu wanadeal na maisha ya watu uzembe wa kijingia tu unaweza kuhatarisha maisha ya mtu!
 
Back
Top Bottom