Chama,
Hata haujui unakataa nini na unakubali nini. Mwanakijiji amesema kuna udhaifu mkubwa kwenye mfumo wa jeshi la polisi, wewe unasema usaili unachukua hadi siku tatu. Hivi kujua kama huyu mtu anatakiwa kuwa pale chuoni ni zaidi ya siku moja basi huo ni uozo wa hali ya juu. Kuna siku wataingia magaidi pale wakilipue chuo nadhani ndiyo utajua polisi si wakulaumiwa!
Mkuu umeelewa nilichokisema? Kama kuna udhaifu toa mapendekezo ya nini kifanyike; hapa hoja yangu iliegemea zaidi kwa hao makuruta waliotapeliwa; sikuwahi kusema au kudai utaratibu unaotumika CCP ni bora; kuzuia ugaidi bado intelijensia yetu ni kiwango cha chini sana na kuzuia ugaidi ni kazi kubwa sana kinachofanyika ni kupunguza athari za ugaidi; mkuu wa chuo mwenyewe anaweza kujigeuza gaidi je utamzuia vipi?
Chama
Gongo la mboto DSM