Kashfa ndani ya Kashfa, Uozo ndani ya Uozo: Mwema, Chagonja, Manumba need to go! (Lowassa pia yumo!)

Napata kizunguzungu. Mwema, ukiwa kama mvaa gwanda mkuu, heshima haipo tena. Umelivunjia heshima gwanda na waTZ kwa ujumla wao. Sasa nahisi kichefuchefu.
 
duuuh kama polisi, u/taifa inaweza kushindwa kutambua ni dhairi kuwa hata watu kutoka nje ya nchi wanaweza kuja wakaingia katika tasisi hizo wakapata habari zote kisha wakasepa pasipo kujulikana!!!!
mi ninachofikiri huu utakuwa ni mtandao mkubwa ndani ya jeshi hilo tena watu wa ngazi za juu
 
Unajua inawezekana kabisa Watanzania sasa tumepigwa ganzi ya ufisadi...

Mzee ukimtoa Dr Slaa wewe ndio mtu wa pili ktk public figures ninao amini wanaipenda Tanzania kweli kweli.nimekusoma sana mpaka nahisi unaweza kufa kwa pressure kwa mwenendo tu wa sisi Watanzania.

RIP J.K Nyerere!
 
wana JF kuna mengi ndani ya majeshi yetu usishangae kuona wamo Wahabeshi, al shabaab, na hata M23 walioajiliwa kama mnyarwada aliyefikia rank ya A/inspect akiwa ktk nchi hii na alipochoka akarudi kwao Rwanda na ni boss ktk polisi yao.

Katika topic hii waliodhulumika na mdhulumaji WOTE wanahitajika kujibu kortini kupita kwa Hosea.
 
hii ni hatari, hatari saana, lkn tunakwenda mbali saana. lkn kwangu mimi tatizo ni mamlaka yaliyoko pale chuo cha polisi, kama ilivyokwenye vyuo vyovyote vya kijeshi, wanafunzi wanapoingia chuoni kwa mara ya kwanza lazima wawe na mwajiriwa wa jeshi husika toka mkoa wanapotoka na huyo mwajiriwa ndio atakaye toa taarifa pale chuoni, mfano ; mimi ni askari toka dar ,nimekuja na wanafunzi 10 na atatoa barua iliyo na maelezo ya hao wanafunzi, baada ya kupokelewa, taratibu zingine zitafuata sasa uzembe una paswa kuwasomba ,uongozi wa chuo jinsi unavyojipanga kiulinzi. binafsi naona wako legelege. pia siasa ziachwe kuliingilia jeshi la polisi, liachwe lifanye /lisimamie ajira lenyewe hizo siasa mara ajira ipitie jkt, mara oooh ipitie vyuoni hayo yote ni makosa anayetaka ajira ya polisi 'anatakiwa akafoleni kwa mkuu wa polisi wa mkoa na akimbizwe mchakamchaka mtaani, na wanafunzi wasindikizwe na mabasi yaliyokodiwa na polisi. binafsi nawapongeza saaana jwtz ni wakali saana kwa wanasiasa kujiingiza kwenye mambo ya kijeshi.mh, mwema,mh manumba. mh gonja wanapaswa washauriwe wawawajibishe viongozi wa vyuo vyao na watazame upya hadhi za wakufunzi wao na usalama wa vyuo na kambi zao zote pamoja na makao makuu ya jeshi lao.
 
Kwa uozo huu alafu anatokea mkuda mmoja anasema eti Kinana ni Kimbunga! Kinana na aoneshe njia basi si ndio kero hizi? Shwaini! CCM wameshindwa kusimamia serikali yao kuna muujiza wa Kinana hapo.
Mkuda?Kibanda mkuda?Kumbe ndio jina linalomfaa!
 
Well done mwanakijiji.umenifumbua macho kuhusu Lowasa. Alipgana kuwa mwenyekti wa kamati ya ulinzi na mambo ya nje. Matukio ya polisi na kashfa lukuki ata jesh hajawai ongerea. Aliongelea mgogoro wa ziwa nyasa.eti tumejipanga na tuko tayari. Mbona hajaongelea haya matukio machafu ambayo yamepoteza uhai wa watu na mali?
 
Kwa sasa serikali ya majimbo inatufaa sana tanzania, ili uratibu wa kazi uwe mwepesi, na maendeleo yatakuja haraka.
 
Mwanakijiji
Utalilaumu vipi jeshi la polisi kwa watu waliotaka kutapeliwa wenyewe? Taratibu za kujiunga na jeshi zipo wazi; zinaanzia wilayani; mkoani hapo ndipo unapofanyika uteuzi wanaokwenda CCP; sasa ikiwa wahusika wenyewe kwanza waliombwa kutoa rushwa hapo peke yake ni kosa; jeshi la polisi halitozi ada ya kuchukua makuruta; kwa maana hiyo wahusika walijiingiza kwenye uvunjaji wa sheria; kujiunga na jeshi kama nilivyosema awali kuna taratibu za mchujo ambao huanzia wilayani hadi mkoani; wahusika walipaswa kushtuka harufu ya utapeli ilikuwepo tangu mapema; Na unakilaumu vipi chuo? wanafunzi waliopokelewa watakuwa ni zaidi ya 200 inawezekana hata 1000 walikuwepo; usaili wa wanafunzi wapya haufanyiki kwa siku moja na hilo liligunduliwa sasa tatizo ni nini? Kama wangemaliza mafunzo hapo hoja yako ingekuwa na mshiko; bado najiuliza jinsi gani mh. Lowassa ameingia vipi pamoja ya kwamba yupo kwenye kamati ya bunge; hapa sioni unamuunganisha vipi au yeye ndiye alihusika na uandikishwaji wa hao makuruta wapya? Kama ni suala la mgeni unayemuongela yeye ndiye aliyetoa mualiko kama mwenyekiti wa kamati? Nadhani ulichopaswa nikushauri mh.Lowassa kama mwenyekiti wa tume alichunguze hilo na si kumpaka matope; Mwanakijiji usiandike vitu kama mwanaharakati umebobea kwenye hii fani haya unanaharakati wenyewe waachie kina Mtoi wao ndio wanaoandika vitu bila kujiuliza maswali ya msingi. Mwanakijiji mtu anapotafuta kitu kwa kutumia misingi ya kuvunja sheria usilaumu vyombo husika akitapeliwa hilo ni funzo; wao walijua tangu awali wanatumia mlango wa uani kuingilia sasa hapakuwa na kukosa kuwatoa kwa kutumia mlango wa mbele; na wala hupaswi kuwasikitikia

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hawa vijana watakuwa wamepitia Makao Makuu tu,huko ndo kuna uozo mwingi sana,kuna watu pale PHQ wanaendesha hilo jeshi kama ni la kwao yaani wao ndo wanaoamua nani ni nani na nani aende wapi kwa kimemo tu na hakuna mtu wa kuuliza hilo.
Kuna haja ya kufanya mabadiliko ya kweli kwenye jeshi letu hili hakuna asiye fahamu umuhimu wa jeshi la polisi ila sasa hakuna mtu mwenye imani nalo,jeshi linatumika kisiasa,
Mi napendekeza hata IJP apendekezwe na kupitishwa na BUNGE ili afanye kazi kwa manufaa ya Taifa zima
Mkuu Mzee Mwanakijiji mi naomba nyie mnaonekana ni watu mnaushawishi mkubwa kupitia kalamu zenu embu ingieni ndani kabisa ya hili jeshi kuna uozo mkubwa sana na ubabe uliopitiliza unaofanya na viongozi wa jeshi la Polisi.

Suala la Kamati ya Bunge hilo nalo ni kichekesho kwasababu mtu anayesimamia hiyo kamati hana jeuri ya kusimama na kukemea viongozi wa jeshi hilo kwani hata yeye si msafi ana kashfa nyingi tu na Polisi wanazijua sio kwamba hawajui ni kwamba "niwajibishe nikuchafue"ndo kinachofanyika sasa hivi,hakuna wa kumnyooshea kidole mwenzake.
 
Last edited by a moderator:
Hivi kweli hii aibu tutaificha vipi majirani wasisikieee.....hivi tukienda nchi za wenzetu sasahivi wanatuonaje???
 
Naona jina Mwema sasa ni kinyume. Kwa Tanzania ambayo ni mojawapo ya maajabu ya dunia watauchuna na litapita kimya kimya. Ili kulipotezea utasikia sasa hivi tume inaundwa kuchunguza. Mwisho wa siku tume itatumia milioni 500 kuchunguza na baadae tutaambiwa "wamekamatwa watuhumiwa" na wamepelekwa mahakamani hivyo ni marufuku kujadili jambo lililopo mahakamani. Kwasababu kashfa ni nyingi watu watarukia nyingine mpya. Ona la Ulimboka linavyosahaulika taratibu. Sasa hivi linaonekana ni hadithi za Abunwasi. Juzi Mwangosi wamemuua. Nalo linasahaulika taratibu kwakuwa liko mahakamani. Tume iliundwa ikaja na taarifa ya Alu lela ulela. Wajumbe wake sasa hivi wanasubiri nafasi za ukuu wa wilaya au Mkoa baada ya kazi nzuri. Akina Manyanya, Mwakyembe si tayari wamepewa vyeo baada ya kumfichia siri baba mwanaasha katika kashfa ya richmond? Sasa kwa hili hakuna atakayejiuzulu au kuwajibishwa! Toka lini mashemeji wakawajibishana? Muwe watulivu mnaweza kubahatika kuwa kwenye tume ya kuchunguza kashfa hiyo. Mkitoa ripoti nzuri kama akina Mwakyembe na kina Makunga ukuu wa wilaya au ukuu wa mikoa unawasubiri kwasababu by the time ripoti inatoka tayari kutakuwa na kashfa nyingine hivyo watu watakuwa busy na mpya!
 
Chama,

Hata haujui unakataa nini na unakubali nini. Mwanakijiji amesema kuna udhaifu mkubwa kwenye mfumo wa jeshi la polisi, wewe unasema usaili unachukua hadi siku tatu. Hivi kujua kama huyu mtu anatakiwa kuwa pale chuoni ni zaidi ya siku moja basi huo ni uozo wa hali ya juu. Kuna siku wataingia magaidi pale wakilipue chuo nadhani ndiyo utajua polisi si wakulaumiwa!
 
Unajua inawezekana kabisa Watanzania sasa tumepigwa ganzi ya ufisadi...
Mkuu Mzee Mwanakijiji ni nani aliibua hii kashafa?
kwanini aibue sasa hivi wakati huu ni utaratibu wa kila mwaka wanapotafuta vijana?
na hao ambao wapo kazini tayari waliopita kwa mtindo huo watafukuzwa kazi au?
ndo maana nawaambia watz wenzangu rushwa kamwe haitaisha....
kama walinda sheria wanaingia kwa rushwa watazuiaje watu kutotoa rushwa?
sifa kubwa ya mtanzania ni UNAINGIA KWA RUSHWA, UNAISHI KWA RUSHWA NA UTASTAAFU KWA RUSHWA.

 
Last edited by a moderator:
Inatia uchungu sana na hayo ni kama baadhi ya mambo tu ktk jeshi la polisi lkn yapo mengi sana ambayo yamejificha watawala wamekaa kimya kwa sbb ya undungu hata katika sehemu muhimu kwenye jamii lakini naamini itafikia wakati watajua watanzania wanahitaji nn.
 
Back
Top Bottom