Mzee wa Masaki
Member
- Sep 30, 2012
- 21
- 15
Huyu Naibu Waziri wa Fedha Janeti Mbene ameanza kutumia vibaya madaraka yake kwa ajili ya kujinufaisha yeye binafsi. Hivi karibuni Naibu Waziri huyu ameuelekeza uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kwenda kubomoa nyumba ya kijana mmoja maeneo ya Masaki karibu na Double Tree hoteli kwa kusingizia eti anataka eneo hilo lijengwe ofisi za mtendaji wa mtaa. Eneo hilo limekuwa na mgogoro kwa siku nyingi kwani kijana Shomari ambaye huko nyuma aliwahi kutoswa baharini na kuokolewa amekuwa akiishi katika eneo na nyumba hiyo tokea bibi yake akiwepo. Bibi yake Shomari aliishi katika eneo hilo tokea enzi za ukoloni na eneo hilo inaonesha lilipimwa mwaka 1948 na kuwekwa katika mpango wa kujengwa barabara. Wanaoishi katika eneo hilo waliahidiwa kufidiwa lakini haikufanyika hivyo na badala yake wakawa wanaelekezwa wajenge makazi yasiyo ya kudumu ili Serikali ikiamua kutekeleza mradi wake wa kujenga barabara iwe rahisi. Kilichotokea bwana Shomari aliwahi kufuatwa na mmiliki wa Double Tree ili amuuzie hilo eneo. Shomari alipokataa huyo mmiliki wa Double Tree aliamua kumfuata Mwenyekiti wa Mtaa ambaye ni Janeti Mbene ili amsaidie kupata eneo hilo. Janeti Mbene akiwa kama Mwenyekiti wa Mtaa alikubali na kisha naye akawa ametamani eneo hilo ili wagawane na mmiliki wa Double Tree, ndipo wakaanza kufuatilia ili kulipata eneo hilo na kuzua mgogoro. Walipoona wanakwama wakamtumia mtu mwingine ajulikanaye kama Jaspreet ili amfungulie kesi Shomari kuwa amevamia eneo lake. Bwana huyu kaja na hati ya kufoji inayoonesha kama yeye ni lmmiliki wa eneo hilo tokea mwaka 1996. Hayo yote yameendelea kukwama kwa sababu ukweli kuhusu kiwanja hicho unabaki kuwa dhahiri kuwa Shomari ndiye mmiliki halali wa eneo hilo. Hivi karibuni kilichotokea mara baada ya Janeti Mbene kuteuliwa kuwa Naibu Waziri alienda kwenye uongozi wa Kinondoni na kuwaelekeza wakamtoe kwa nguvu bwana Shomari, ndipo hao watu wakampa notisi na kisha juzi wakaenda kutekeleza azma yao ya kubomoa na kuharibu haribu kila kitu. Wamewachukua hadi watoto wake ili kumlazimisha aondoke eneo hili. Ukibahatika kufika pale utahuzunika sana jinsi palivyo kwani kuna walinzi wanaolipwa na Janeti Mbene wanalinda eneo hilo ambalo tayri limewekwa uzio wa mabati kuonesha kuwa kuna nyumba itajengwa hapo. Bwana Shomari amebakishiwa banda ambalo analala yeye tu. Akiwa ndani ya uzio amezingwa, nje ya banda analolala kuna mbwa, bata kuku na makororo kibao, kitu ambacho kinasikitisha sana. Yaani huyu kijana kafanyiwa uonevu wa hali ya juu na hata hatima yake haijulikani kwani uongozi wa Kinondoni Manispaa unasema hautaki kabisa kumaliza mgogoro huo kwa sababu hawahusiki na anayehusika ni Naibu Waziri Janeti Mbene. Ili kuelewa zaidi haya ninayoyasema unaweza kusoma baadhi ya nyaraka kuhusu mgogoro ambazo nakuwekea hapa baada ya muda mfupi ujao.
View attachment 66928
Mlio online kwa sasa naomba mnielekeze namna ya kufanya attachment niwatumie documents
Sasa ukifungua hiyo attachment hapo juu utaona kuwa Manispaa walisema kuwa hilo eneo ni la barabara kwa mujibu wa upimaji wa mwaka 1948 wakati bibi yake Shomari akiwa anaishi eneo hilo, inakuwaje sasa Serikali ya Mtaa inalibadili eneo la barabara kuwa na Serikali ya mtaa. Inasemekana na ofisi za CCM zitajengwa hapo hapo karibu. Acheni uonevu jamani, hata aibu hamna. Wako wapi wapigania haki za binadamu, wanasheria wetu wanataka pesa tu. Pesa hii pesa itatutoa utumbo.
View attachment 66928
Mlio online kwa sasa naomba mnielekeze namna ya kufanya attachment niwatumie documents
Sasa ukifungua hiyo attachment hapo juu utaona kuwa Manispaa walisema kuwa hilo eneo ni la barabara kwa mujibu wa upimaji wa mwaka 1948 wakati bibi yake Shomari akiwa anaishi eneo hilo, inakuwaje sasa Serikali ya Mtaa inalibadili eneo la barabara kuwa na Serikali ya mtaa. Inasemekana na ofisi za CCM zitajengwa hapo hapo karibu. Acheni uonevu jamani, hata aibu hamna. Wako wapi wapigania haki za binadamu, wanasheria wetu wanataka pesa tu. Pesa hii pesa itatutoa utumbo.