Kashfa: Msemaji wa serikali atumia picha za SGR ya Kenya

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
12,082
2,000
Kwa ofisi kubwa kama ya msemaji wa serikali anadiriki vipi kutumia picha za SGR ya kenya kuonyesha SGR ya Tanzania?

Huyu ana PHD sijui ya nini?

Watanzania sio wajinga kama ameshindwa kupata picha zinazotushawishi Watanzania sio busara na sio haki kabisa kutuwekea picha za reli ya majirani zetu.

Ni sawa na kupeperusha bendera ya kenya kwenye gari la Rais wa Tanzania.

Hapa alikua anazungumzia kwa.ba ukarabati wa reli ya zamani unaendelea.

Tunaofisi ya msemaji wa serikali ya hovyo kuwahi kutokea.

Wenye uelewa mzuri ndio wananielewa kwanini nimeita hii ni kashfa.

20191208_225357.jpeg
 
Ole

JF-Expert Member
Dec 16, 2006
2,145
2,000
Amefanya vizuri sana kutumia hizo picha kama ni za Kenya kwa sababu ni majirani zetu na wanashirikiana na Serikali hii kuliko kama angetumia picha za Japan, UK Germany au mahali popote mbali ya Tanzania. Good work Dr Abasi maana unaonyesha ukomavu wako sio tu kwa kujali uhusiano mzuri na majirani zetu. (Message sent and delivered)
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
12,082
2,000
Ni ujinga wa hali ya juu sana
Amefanya vizuri sana kutumia hizo picha kama ni za Kenya kwa sababu ni majirani zetu na wanashirikiana na Serikali hii kuliko kama angetumia picha za Japan, UK Germany au mahali popote mbali ya Tanzania. Good work Dr Abasi maana unaonyesha ukomavu wako sio tu kwa kujali uhusiano mzuri na majirani zetu. (Message sent and delivered)
 
List 255

JF-Expert Member
Oct 26, 2019
271
1,000
Kuwa na akili kidogo, Rudia kusoma alichoandika ktk ambanisho la hiyo picha kisha urudi tena
 
Lyamber

JF-Expert Member
Jul 24, 2012
10,474
2,000
Hivi huko Rwanda kuna nini haswa SGR italeta tija kama ikienda Kigoma hio, huko Rwanda ni kuifaidisha Rwanda maana wao ndo watakua wanapeleka mizigo DRC akili za hawa jamaa sijui zikoje
 
Unataka kuwachagulia Rwanda maendeleo yao?
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,987
2,000
Reli ya SGR ya Tanzania na Rwanda mlitaka atumie mfano wa picha ya SGR ya wapi ndio ingalikuwa si aibu. Kila mara tunawekewa picha za treni za kila ana za SGR wakati hata vichwa vyenyewe hatujanunua sijasikia mtu kushangaa au sababu ni picha za kutohoa toka Ulaya ila za Kenya ni nongwa😃😃
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,002
2,000
Ingependeza zaidi ameitumia picha hiyo kwa muktadha gani? Je alisema hii ndiyo SGR ya Tanzania au alikuwa anasema nini? Bila kujua hilo twaweza kumuonea baba wa watu bahati mbaya hilo silioni kwenye maelezo yako mkuu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom