Kashfa mpya Nishati na Madini; Kikwete na Pinda wajiuzulu au wawajibishwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa mpya Nishati na Madini; Kikwete na Pinda wajiuzulu au wawajibishwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jul 26, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,993
  Likes Received: 37,669
  Trophy Points: 280
  Kuibuka kwa kashifa mpya inayomhusu katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini inaacha maswali mengi kuliko majibu. Katibu mkuu huyo anadaiwa kuipa tender kampuni ya PUMA ya kuiuzia IPTL mafuta mazito ya kufua umeme kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma. Taarifa zinasema aliingilia uamuzi wa TANESCO wa kuipa kampuni nyingine kazi hiyo kwa kile kinachodaiwa ni tofauti ya bei.

  Hata hivyo gazeti la Nipashe la leo trh 26/07/2012 ambalo pia linapatikana online limetoa taarifa ambayo mimi imenishangaza kuwa waziri mkuu anafanya juhudi za kumtetea katibu mkuu huyo. Taarifa katika gazeti hilo zinasema Waziri Mkuu amekutana na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini akiwasihi waachane na mpango wao wa kutaka katibu mkuu huyo awajibishwe. Swali, kwanini waziri mkuu anamtetea mtu aliyevunja sheria badala ya kumshauri raisi amuwajibishe? Je ametumwa? Na kama ametumwa ni nani kamtuma na kwa faida ya nani?

  Watanzania hebu tutafakari mambo haya yafuatayo alafu tujiulize ni kwanini raisi na waziri mkuu wasijiuzulu au wawajibishwe
  1. Kwanini wizara hii imekuwa kinara wa ufisadi tangu Kikwete aingie madarakani na ni hatua gani za kuridhisha zimechukuliwa mpaka leo?
  2. Hivi viongozi hawa wakuu na bodi ya wakurugenzi wa TANESCO hawakujua kuwa shirika linahujumiwa ktk bei ya mafuta mpaka huyu katibu mkuu mpya bwana Maswi alipoingia ufisini na kama walijua mbona walikaa kimya?Ina maana na wao wanapata taarifa hizi kupitia vyombo vya habari?
  3. Ni hatua gani zilichukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa richmond?
  4. Kwanini mamlaka ya uteuzi ambayo ni raisi huwa haichukuia hatua kwa wakati mpaka bunge limshinikize?
  5. Kwanini waziri mkuu anamtetea mtu alievunja sheria badala ya kushauri awajibishwe?
  6. Watendaji wa wizara na TANESCO kutokuwa na hofu ya ufisadi ni nani anawapa kiburi na kuwalinda licha ya mlolongo wa matukio ya wenzao kuwajibishwa?
  7. Je, wanayafanya haya kwa maelekezo ya wakubwa na ndio maana hawana hofu licha ya kujua hatari inayowakabili?
  8. Je, ni kweli wakubwa wao wa kazi wanakuwa hawajui kinachoendelea mpaka taarifa hizi zifike kwenye vyombo vya habari?
  9. Waziri mkuu hata kama hana mamlaka juu yao na labda hapati ushirikiano mbona hajiuzulu?
  10. Mkurugenzi mkuu TANESCO amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi; Je katibu mkuu wa wizara ambae kwa mazingira ya sasa nae ni mtuhumiwa ni sahihi kuendelea kuwepo ofisini mpaka leo? Au mpaka bunge lije juu?Hii sio aibu na fedheha kwa mamlaka ya uteuzi?

  Maswali ni mengi kuliko majibu.Wahusika mjitafakari na muwajibike. Tumechoka kila siku wizara moja tu.

  Unahitajika uchunguzi huru tena wa vyombo vya nje maana hata kwenye richmond uchunguzi wa ndani ulificha baadhi ya taarifa kwa kile kilichodaiwa kuokoa serikali.
   
 2. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kizungumkuti!!!!!!
   
 3. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Jambo moja ni wazi kuwa sekta ya nishati na madini imeingiliwa left and right na kwa kuwa wanene wa awamu ya nne ni sehemu ya fikra na vitendo vilivyotufikisha hapa kwenye kasha njoo-kashfa nenda-kashfa rudi, tukubaliane kwamba kama waliokuwepo walitumia akili zao zoote za kufundishwa eti na za kwao na madini na nishati ni uozo mtupu, Taifa linahitaji mfumo mwingine na watu wengine kutuongoza
   
 4. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ... hivi sheria maana yake nini hasa? Lengo la sheria ni nini? nadhani OBJECTIVITY ndio ishu hapa. THINK DEEP.
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Watu wana miaka 3 ya kula vya mwisho mwisho tuwaachieni.. Kula kwa zamu hata cdm wakichukua nchi nao watakula vile vile
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pengine mimi niulize tofauti na swala zima.. Kwa nini iwe kazi ya Tanesco ndio wachague nani awa supply mafuta IPTL iikiwa IPTL ni shirika binafsi na linajitegemea kuzalisha umeme na kuwauzia Tanesco Umeme? kwa nini iwe jukumu la Tanesco ambaye ni mnunuzi wa umeme kutoka IPTL ndiye ampe mtaji IPTL kuendesha mitambo yake?....hamuoni ubovu wa mikataba hii iloingiwa na viongozi wetu wanasiasa isipokuwa ubovu wa uongozi wa Tanesco...

  Tunarudi kule kule, serikali yetu imejaa mafisadi na hauna mipaka kabisa, na ajabu kubwa ni kwamba baada ya kuona mafuta yanatugharimu zaidi kuyapa haya mashirika yaliyoletwa nchini kuzalisha umeme wa dharura..Sasa hivi ndio mpango mzima! haya ndio yamekuwa mashirika ya uzalishaji umeme nchini, hakuna mipango yetu wenyewe isipokuwa kupitia kwao. Tunawavutia bomba la gas toka Kusini kwa ajili yao!. Yaani sisi wanunuzi wa umeme toka kwao ndio pia walipaji wakubwa wa matumizi ya kuendesha mitambo yao vile vile...Hii akili kweli jamani..

  Kwa nini tusiwe na mitambo yetu wenyewe ya kuzalisha umeme na tuvute bomba la gas kwa ajili ya uwekezaji wa ndani na wa kudumu ktk miradi ambayo tunaipanga sisi wenyewe. Leo tunawauliza mafuta na inatugharimu sana kesho tutawalipia gas vilevile baada ya kutugharimu kuvuta bomba la gas hadi Dar. Hizi gharama za ujenzi wa bomba lazima ziingie ktk gharama ya umeme utakao uzwa na Tanesco sio IPTL au Symbion watakaolipia ni sisi wananchi kupitia Tanesco.

  Tukikataa ama mchezo wanazima machine tutawafanya nini?. hasira zetu zote tunarudi kwa Tanesco.. Actually hao IPTL, Symbion na mashirika mengine - what are their expenses for real..kuwa na generator 100mw au 45 tu basi unapewa, kiwanja, supply ya mafuta au gas bure kisha unawauzia tena Tanesco umeme kwa kutumia gharama za Tanesco!.. I mean something is very wrong here!.
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkandara, ukiangalia hii issue ya TANASECO kwa sasa utaona kuna uwezekano mtando wa Dowans umekeweza sana kwenye hili shirika na huyu bwana mdogo Mhando alikuwa ni dalali wao mzuri. Kuondoka kwake kunatoa mwanya wa kufumua mambo na sasa ndio sakarasi zinaanza ili kutisha watu na kama itabidi kuondoka na shingo ya katibu mkuu basi wako tayari kufanya hivyo.

  Nitataka kuona wabunge (regardless ni chama gani) watakao mtetea huyu Mhando na hapa itatoa picha 'uwekezaji' TANESCO ni mpana kiasi gani.

  Katibu mkuu anaweza akawa amekiuka sheria za manunuzi, lakini aliruka kwa manufaa ya mapana zaidi maana alisitisha utaratibu uliokuwepo wa kununua mafuta kupita kwa middleman na badala yake amemua mafuta yanunuliwe moja kwa moja toka kwa supplier (PUMA). Upindishaji wa sheria wa namna hii mimi naukubali kabisa. Tusibiri bunge bado linaendelea.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  FJM Lakini mimi nina tatizo moja tu ya kwamba Mhando ni sehemu tu yan matatizo yote. Utamwondoa Mghando na kumweka mtumwingine ambaye atakuta utaratibu ni ule ule. Nimesema wazi hata mimi leo ukinambia nishike nafasi hiyo Tanesco nitavuta na kuwapa ndugu na jamaa zangu tender kwa sababu tatizo zima ni la kimfumo sio nani anaweza kutokuwa na tamaa..

  Huu mpango wa kukata matawi wakati unajua kabisa mti mzima umeoza ndio naupinga miye.. Viongozi wangapi wameshakuja Tanesco toka Mwinti aondoke au IPTL kuinga mkataba.. Tumebadilisha viongozi wee hadi tunaishiwa watu kwa sababu hatutaki kukubali ama ku face the real problem..

  Mfumo mzima wa mikataba na utawala ni mibovu kwa nchi yote. Hapa kilichobakia ni kata mti panda mti - ndio tutaweza pata miti safi.. Kupurura matawi ya mti ulooza unauwezesha mti kukua kustawi tena japo umeoza!..Hivi mnafikiria Ufisadi kufikia stage hii iloyopo leo ni bahati mbaya?..
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. m

  mliberali JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 2,885
  Likes Received: 1,517
  Trophy Points: 280
  nadhani tujipe muda kidogo tupembue,pumba na mchele tutajuatatizo nini? kuna mambo yanafichwa, yawezekana, kuwa katibu mkuu ni "mzalendo" ila alikiuka utaratibu kwa maslahi ya taifa twaweza kumuhukumu kwa hilo,hoja zake zinashawishi watu makini, na mkurugenzi aliyesimamishwa na wanomtetea hawajajenga hoja shawishi, zaidi ya kulalamika tu., naona hata vyombo vya habari vimeanza kuwa na upande,tuwe makini
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Nakubaliana na wewe, kwamba uwozo ni widespread. Lakini that's what we have right now. Hivyo, attempt ya kujaribu ku-save cent here and there ni bora kuliko attempt za kufanya ovrerhaul kwa sababu hilo haliwekani kabisa, not under the current team anyway. 2015 iko chance kwa watanzania kujenga upya provided hawataonegewa na t-shirt au taarab.
   
 11. B

  Bob G JF Bronze Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni wizi na wezi watupu Dawa ni kuipiga chini ccm then sheria ichukue mkondo wake na mwisho wafilisiwe kabisa
   
 12. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Well said mkuu.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hii ndio mimi sikubaliani nayo ya kusema this is what we have right now.. Unataka tuwaeleze madudu ya nani ktk wizara ya nishati na Madini? au mnataka tuanzie wapi ili mfahamu kwamba Mhando ni product ya kile tulichokipanda.. Unapurura mti ulokwisha oza zamani kwa sababu wamesema hizo mil 800 kwa mkewe - changa la macho, wakati wao wanaiba mabillioni kila siku tunavyoongea hapa.

  Je unajua ya kwamba Tanesco miaka yote matumizi yao huzidi Mapato! miaka yote wanafanya kazi ya kanisa kwa sababu wanalipia hadi miradi ya mawaziri na viongozi wetu. Unamkumbuka yule katibu mkuu Patrick Rutabanzibwa aloachishwa baada ya kumwaga radhi ktk zengwe la IPTL ilikuwa vipi na yumo ktk list of shame?..Nadhani mwaka jana alikuwa katiba mkuu wizara ya ardhi kama sikosei nilimuona Kigamboni ktk sakata la mji mpya..
  Je, tuliwafikisha mahakamani kujua ukweli uko wapi..The guy will die being mistaken for Fisadi kwa sababu tu tuliamua kumtundika yeye..
   
 14. M

  Mzeenani64 Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wewe ni mpumbavu sana..kama una cha kuandika kaa kimya sio unaleta ujinga kwenye inshu nyeti inayogusa maisha ya mtanzania
   
 15. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Mimi nasema hivi, hata aje nani, maadamu kazaliwa na kulelewa Tanzania hakuna jipya, labda atoke jamii nyingine, labda ya kihindi au sijui mtanzania lakini aliye adoptiwa nje ya nchi lakni sio ndani ya utamaduni wetu! Utamaduni wetu unakingana na hayo ambayo mnapendelea yatokee na ninawahakikishia mtasubiri sana huyo mtu lakini hatatokea nakila mtapojaribu kudhani kwamba mmepata mtu stahiki atawakatisha tamaa mwisho wa siku kama Zitto & Co.
   
 16. j

  jaridotcom2 Member

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Huna jipya laiti ungeyajua maovu ya mhando na kwa nn huyo mwenyekiti wa bodi auze mafuta kwa bei ya Juu ambayo alikua anayanunua ktk kampuni ya PUMA ebu jaribu kufikilia hao PUMA wangekua na bei ya juu kulikua hakuna haja ya huyo Mboma (mwenyekiti wa bodi) kuyanunua mafuta na kuyauza kwa bei ya juu huu ni ushenzi na Maswi yuko sahihi na watanyooka hawa Management ya Tanesco maana walizoea sana kufisadi
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Swali nimeuliza hamkulijibu.. Why Tanesco ndio wanunue mafuta kwa ajili ya IPTL? Kwa nini IPTL wenyewe wasinunue mafuta wanakotaka wao sii lazima Puma. Mafuta is part of their expenses, wayanunue wao kisha wao wawauzie Tanesco umeme.

  Jibu ni moja tu IPTL na mashirika yote ya kuzalisha umeme ni mali za viongozi wetu.. we are all paying for their expenses lakini hamtaki kutazama huko na sasa mnawavutia na bomba la gas watumalize vizuri. Tunagom,bana na Tanesco lakini hatutaki kutazama IPTL na Symbions na mashirika haya yalokuwa ya dharura leo ndio yameshika uchumi wa nchi..
   
 18. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,592
  Likes Received: 2,976
  Trophy Points: 280
  Katibu mkuu ni mzalendo sana. Wale wachumia tumbo waliteua kampuni ya kati inayonunua mafuta kutoka PUMA, na hivyo kuyafanya mafuta hayo yawe na bei ya juu kwa kiasi cha TZS 3 billion.

  Katibu Mkuu akagoma, akailazimisha TANESCO kuchukua mafuta moja kwa moja toka kwa PUMA bila ya mtu wa kati. HUYU NI MZALENDO, AMEOKOA TZS 3 BILLION AMBAZO WATU WALITAKA WAZIVUNE ETI KWA KUTOA MAFUTA PUMA NA KUYAPELEKA IPTL.

  Kwa jinsi serikali mpaka wabunge walivyo wachumia matumbo, si kitu cha ajabu wakamng'ang'ania katibu mkuu mpaka atolewe. Maana hawa wezi ni syndicate kubwa, wana watu wao kila mahali, ndani ya bunge, ndani ya kamati za bunge, kwenye baraza la mawaziri mpaka kwa watendaji wa serikali.

  Na nchi yetu hii ilivyojaa wezi ni vigumu sana mtu mwadilifu kudumu kwenye nafasi za maamuzi.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,606
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  MZOZO NISHATI NA MADINI: Pinda amuokoa JK

  • Mbatia adai kuna wabunge wamehongwa

  na Mwandishi wetu | Tanzania Daima

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda juzi jioni alifanya kazi ya ziada kuzima hasira za wabunge waliokuwa wakitaka kuona Waziri wa Nishati na Madini, Pofesa Sospeter Muhongo, na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi, wakiwajibika kwa kujiuzulu nyadhifa zao vinginevyo wangekwamisha bajeti ya wizara hiyo.

  Habari ambazo Tanzania Daima, imezipata zinadai kuwa wabunge hao walidhamiria kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2012/2013 inayotarajiwa kusomwa bungeni leo.

  Chanzo cha habari hizo kilidai wabunge walifikia hatua hiyo baada ya vigogo hao kuripotiwa kuwa waliruhusu ukiukwaji wa sheria ya manunuzi ya umma kwa kuipa zabuni kampuni ya Puma Energy (T) Ltd zamani BP.

  Kampuni hiyo ilipewa zabuni ya kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na kuziweka kando kampuni zilizokuwa zimechaguliwa kupitia mchakato halali wa zabuni ya TANESCO.

  Suala hilo linahusishwa na kusimamishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, William Mhando, kwamba alichukuliwa hatua baada ya kukataa kutii maelekezo ya wizara.

  Katika kikao cha juzi usiku cha wabunge wa CCM, kilichoongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wabunge hao walikuwa na msimamo wa kumuwajibisha Muhongo na Maswi. Wakati wabunge wakiwa na msimamo huo, Pinda aliingia akiwa na lengo la kuilinda serikali na chama kinachotawala (CCM).

  Pinda alidai kuwa kumshinikiza Rais Kikwete amuwajibishe waziri aliyemteua miezi mitatu iliyopita ni kutomtendea haki na kuuonyesha umma kuwa hakufanya chaguo sahihi.

  Tanzania Daima, ilidokezwa kuwa wajumbe wote walikubaliana kwamba Katibu Mkuu wa Nishati na Madini alifanya makosa na alivunja sheria.

  Wabunge wa CCM walitaka Maswi na Muhongo watoswe ili kujenga heshima ya serikali na kusimika utawala wa sheria.

  Inadaiwa kuwa kulikuwa na wabunge waliopangwa kimkakati kushawishi wenzao wasiisulubu serikali kwa kukwamisha Bajeti ya Nishati na Madini leo.

  Miongoni mwa wabunge wanaotajwa ni Waziri Mkuu Pinda, William Lukuvi, Jenista Mhagama na Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage. Inadaiwa kuwa Mwijage ana maslahi katika Puma Energy iliyopewa zabuni ya kuiuzia mafuta IPTL na Maswi.

  Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka, anadaiwa kutaka iundwe kamati teule ya Bunge kuchunguza uozo ulio ndani ya wizara na TANESCO.

  Baadhi ya wabunge wakasema wazo lake ni sawa, lakini katika mazingira ya sasa ya kisiasa ya CCM, tume itaibua uchafu mwingi ambao utaimaliza serikali mbele ya umma.

  Sendeka alisema: "Mbona katika sakata la Richmond iliundwa kamati iweje hivi sasa isiundwe wakati kosa la Maswi linafanana na la Lowassa?"

  Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, inasemekana alijenga hoja kuwa CCM na serikali walifanya makosa kwenye sakata la Richmond ambalo lilimfanya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, kuachia ngazi.

  "Tulimtosa Lowassa, baadaye ukweli umejulikana, na sasa makosa yetu yanaigharimu serikali na CCM. Tusirudie makosa yale yale, tuwaache hawa kwa maslahi ya CCM," alisema.(Dah! kwa Maslahi ya CCM eeh! na siyo ya nchi!!!)

  Hata hivyo baadhi ya wajumbe walishikilia msimamo wa kuwajibishwa kwa Muhongo na Maswi kwa madai kuwa endapo wataachwa, wataimaliza serikali ya CCM.

  Walisema kuwaacha ni sawa na kulitangazia taifa kwamba wao ni wavunjaji wa sheria walizozitunga wenyewe.

  Tanzania Daima imeelezwa kuwa hata hivyo hatimaye wabunge hao walikubaliana kwa shingo upande kuwa msimamo wa wabunge wa CCM ni kulinda chama na serikali.

  Mbatia alonga
  Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ameibua ufisadi mzito unaofanywa na TANESCO na kuwaomba wabunge wasimame kidete ili watuhumiwa wachuliwe hatua.

  Mbatia ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa na Rais Kikwete, alifichua ufisadi huo mbele ya waandishi wa habari mjini hapa, akisema kuwa serikali imekuwa ikipoteza mabilioni ya fedha kulisaidia shirika hilo wakati zinaishia mikononi mwa wajanja ambao ni menejimenti na Bodi ya Wakurugenzi.

  Tuhuma za Mbatia zinakuja ikiwa ni wiki mbili tangu Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO iwasimamishe kazi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, William Mhando, na wenzake watatu kwa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.

  Mhando na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga, na Meneja Mwandamizi Ununuzi, Harun Matambo, walisimamishwa na bodi hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Jenerali mstaafu, Robert Mboma, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yao.

  Kwa mujibu wa Mbatia, wabunge wamekuwa wakifuatwa ndani na nje ya Bunge na hata kwenye mahoteli walikofikia wakishawishiwa kuiunga mkono TANESCO, jambo alilodai limewaingiza baadhi ya wenzao kwenye ufisadi.

  Akifafanua kwa undani, Mbatia ambaye aliongozana na wabunge wote wa chama chake, alisema kuwa mpaka sasa hawana imani na Kamati ya Nishati na Madini kwa kuwa baadhi ya wajumbe wake vile vile ni wajumbe kwenye bodi ya TANESCO na wamekuwa wakitumika kuwarubuni wabunge wakingie kifua ufisadi.

  "Tulipokwenda Ikulu kuonana na Rais Kikwete kama chama kuzungumzia mchakato wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Januari 21 mwaka huu… tuligusia pia hali mbaya iliyokuwa ikiikabili TANESCO lakini Rais alitueleza kuwa serikali imeipa ruzuku ya sh bilioni 136 ili kuliwezesha," alisema Mbatia.

  Aliongeza kuwa kwenye bajeti ya mwaka jana, iliafikiwa kuwa TANESCO itafutiwe mkopo wa sh bilioni 408 na serikali pia ikalipa deni lake la sh bilioni 68 kwa shirika hilo pamoja na kulipatia mafuta ya sh bilioni 17.

  Alisema kuwa mgogoro wa TANESCO ulianza kuibuka baada ya kuzushwa uongo kuwa nchi inaweza kuingia gizani wakati wowote kutokana na hali mbaya ya shirika, madai ambayo Mbatia alisema si ya kweli kwani ulikuwa ni ujanja wa mafisadi kuzima kwa makusudi mitambo.

  "Kisha TANESCO iliingia kwenye mchakato wa kutafuta wazabuni wa kuiuzia mafuta mazito ya kuendesha mitambo yake ambapo ilifanya mazungumzo na kampuni tatu zilizoonyesha kuwa tayari kuiuzia mafuta hayo kwa sh 1,800 kwa lita," alisema.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, naye alifanya mazungumzo na Kampuni ya Puma ambako serikali ina hisa za asilimia 50 na kuafikiana kuwa inaweza kusambaza mafuta hayo kwa gharama ya sh 1,460 kwa lita, bei iliyoonekana kuwa na unafuu zaidi.

  Mbatia alifafanua kuwa pamoja na kampuni ya Puma kutokuwa kwenye orodha ya zile zilizoomba zabuni hiyo, Maswi alitumia kanuni ya 42 (1) ya mamunuzi ya umma inayompa mamlaka ya kuamua vinginevyo kwenye masuala yenye maslahi ya umma kuipa zabuni hiyo hiyo.

  "Kosa na kelele zote zimetoka hapo, mianya ya mafisadi imezibwa kwani walitaka kuzipa zabuni kampuni za bei kubwa ili wavune sh bilioni tatu ambazo zinaokolewa kila baada ya wiki mbili. Sasa kama kwa mwezi TANESCO inaokoa sh bilioni sita kwa nini tumnyime zabuni huyu?" alihoji.

  Mbatia alisema kwa mwezi Mei pekee TANESCO ilikusanya sh bilioni 85 na matumizi yake kwa mwezi ni sh bilioni 11 ambapo kwa wastani wanapata zaidi ya sh bilioni 60 wakiwa na ziada ya sh bilioni 50 kila mwezi.
   
 20. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,993
  Likes Received: 37,669
  Trophy Points: 280
  Mkuu unachongea kinaweza kikawa na ukweli lakini tujiulize huyu katibu mkuu kateuliwa hivi karibuni na kukuta tatizo hilo la bei ya ufisadi. Sasa najiuliza huyu mhando na wenzake wakati wananunua hayo mafuta kwa bei ya juu viongozi wengine serikalini walikuwa hawajui kuwa TANESCO inauziwa mafuta kwa bei ya kulangua?

  Na kama walijua mbona wao hawakuchukua hatua mapema kukomesha wizi huo au kwa maneno mengine mbona wao hawakuonyesha uzalendo kama Maswi?

  Ina maana bila Maswi wizi huu ungeendelea tu?Hivi ni kweli viongozi wakubwa wa nchi hii hawakujua kuhusu ulanguzi huu?Ukisoma mwanahalisi ya jana trh 25/07/2012 katibu mkuu Maswi nae anaonekana ana yake ktk sakata hili.

  Mkuu hapa solution ni tume huru iundwe kama ile ya richmond ndio tutajua ukweli ni upi.
   
Loading...