Obi
JF-Expert Member
- Jul 6, 2009
- 374
- 79
Lakini mimi nina tatizo moja tu ya kwamba Mhando ni sehemu tu yan matatizo yote. Utamwondoa Mghando na kumweka mtumwingine ambaye atakuta utaratibu ni ule ule. Nimesema wazi hata mimi leo ukinambia nishike nafasi hiyo Tanesco nitavuta na kuwapa ndugu na jamaa zangu tender kwa sababu tatizo zima ni la kimfumo sio nani anaweza kutokuwa na tamaa..
Huu mpango wa kukata matawi wakati unajua kabisa mti mzima umeoza ndio naupinga miye.. Viongozi wangapi wameshakuja Tanesco toka Mwinti aondoke au IPTL kuinga mkataba.. Tumebadilisha viongozi wee hadi tunaishiwa watu kwa sababu hatutaki kukubali ama ku face the real problem..
Mfumo mzima wa mikataba na utawala ni mibovu kwa nchi yote. Hapa kilichobakia ni kata mti panda mti - ndio tutaweza pata miti safi.. Kupurura matawi ya mti ulooza unauwezesha mti kukua kustawi tena japo umeoza!..Hivi mnafikiria Ufisadi kufikia stage hii iloyopo leo ni bahati mbaya?..
Kinachotakiwa ni kuwa na reform ambayo inaweza kuisaidia nchi iondokane na mikataba feki yasiyo na tija yeyote. Mfano mzuri ni Ghana walipopata uongozi mpya Prof Atta Mills (Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi) alirekebisha mikataba mingi ya kinyonyaji. Ikiwepo ya bonus kubwa ya rais mstaafu.