Kashfa mpya Nishati na Madini; Kikwete na Pinda wajiuzulu au wawajibishwe!

Kuibuka kwa kashifa mpya inayomhusu katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini inaacha maswali mengi kuliko majibu. Katibu mkuu huyo anadaiwa kuipa tender kampuni ya PUMA ya kuiuzia IPTL mafuta mazito ya kufua umeme kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma. Taarifa zinasema aliingilia uamuzi wa TANESCO wa kuipa kampuni nyingine kazi hiyo kwa kile kinachodaiwa ni tofauti ya bei.

Hata hivyo gazeti la Nipashe la leo trh 26/07/2012 ambalo pia linapatikana online limetoa taarifa ambayo mimi imenishangaza kuwa waziri mkuu anafanya juhudi za kumtetea katibu mkuu huyo. Taarifa katika gazeti hilo zinasema Waziri Mkuu amekutana na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini akiwasihi waachane na mpango wao wa kutaka katibu mkuu huyo awajibishwe. Swali, kwanini waziri mkuu anamtetea mtu aliyevunja sheria badala ya kumshauri raisi amuwajibishe? Je ametumwa? Na kama ametumwa ni nani kamtuma na kwa faida ya nani?

Watanzania hebu tutafakari mambo haya yafuatayo alafu tujiulize ni kwanini raisi na waziri mkuu wasijiuzulu au wawajibishwe
1. Kwanini wizara hii imekuwa kinara wa ufisadi tangu Kikwete aingie madarakani na ni hatua gani za kuridhisha zimechukuliwa mpaka leo?
2. Hivi viongozi hawa wakuu na bodi ya wakurugenzi wa TANESCO hawakujua kuwa shirika linahujumiwa ktk bei ya mafuta mpaka huyu katibu mkuu mpya bwana Maswi alipoingia ufisini na kama walijua mbona walikaa kimya?Ina maana na wao wanapata taarifa hizi kupitia vyombo vya habari?
3. Ni hatua gani zilichukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa richmond?
4. Kwanini mamlaka ya uteuzi ambayo ni raisi huwa haichukuia hatua kwa wakati mpaka bunge limshinikize?
5. Kwanini waziri mkuu anamtetea mtu alievunja sheria badala ya kushauri awajibishwe?
6. Watendaji wa wizara na TANESCO kutokuwa na hofu ya ufisadi ni nani anawapa kiburi na kuwalinda licha ya mlolongo wa matukio ya wenzao kuwajibishwa?
7. Je, wanayafanya haya kwa maelekezo ya wakubwa na ndio maana hawana hofu licha ya kujua hatari inayowakabili?
8. Je, ni kweli wakubwa wao wa kazi wanakuwa hawajui kinachoendelea mpaka taarifa hizi zifike kwenye vyombo vya habari?
9. Waziri mkuu hata kama hana mamlaka juu yao na labda hapati ushirikiano mbona hajiuzulu?
10. Mkurugenzi mkuu TANESCO amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi; Je katibu mkuu wa wizara ambae kwa mazingira ya sasa nae ni mtuhumiwa ni sahihi kuendelea kuwepo ofisini mpaka leo? Au mpaka bunge lije juu?Hii sio aibu na fedheha kwa mamlaka ya uteuzi?

Maswali ni mengi kuliko majibu.Wahusika mjitafakari na muwajibike. Tumechoka kila siku wizara moja tu.

Unahitajika uchunguzi huru tena wa vyombo vya nje maana hata kwenye richmond uchunguzi wa ndani ulificha baadhi ya taarifa kwa kile kilichodaiwa kuokoa serikali.
Africa hatuna utamaduni wa viongozi wetu kujiuzulu ingekua America au Europe sawa
 
Kama utafikiria hili jambo vizuri utagundua kuna njama kubwa ya kumchafua Maswi kwa kuwa anasimamia ukweli na maslahi ya taifa.
Daima tz anayefanya mema na haki hapendwi na pia hupuuzwa kwa kila asemalo na afanyaloo..
 
Ni kweli maswi alifanya right thing kununua mafuta rahisi kuliko yale ya mhando.
Tatizo la watanzania nini? Yule aliyeokoa hela za walipa kodi au yule aliyefuata sheria na kutia hasara nchi?
 
Swali nimeuliza hamkulijibu.. Why Tanesco ndio wanunue mafuta kwa ajili ya IPTL? Kwa nini IPTL wenyewe wasinunue mafuta wanakotaka wao sii lazima Puma. Mafuta is part of their expenses, wayanunue wao kisha wao wawauzie Tanesco umeme.

Jibu ni moja tu IPTL na mashirika yote ya kuzalisha umeme ni mali za viongozi wetu.. we are all paying for their expenses lakini hamtaki kutazama huko na sasa mnawavutia na bomba la gas watumalize vizuri. Tunagom,bana na Tanesco lakini hatutaki kutazama IPTL na Symbions na mashirika haya yalokuwa ya dharura leo ndio yameshika uchumi wa nchi..

Kwangu mimi hii ni dawa chungu sana kuimeza. Kuna hoja kubwa sana ya msingi, ni kwa nini wananunuliwa mafuta? Na maana yake ni nini, kuwa ndani ya mikataba hiyo tulijifunga kuwanunulia hayo mafuta for the foreseable future kiasi kwamba hakuna jinsi ya kujichomoa? Na je ndio wote tumekubali upofu wa moja kwa moja kuwa haya makosa hayawezekani kurekebishwa? Au ndio ile kauli ya Pinda kuwa tukifurumua nchi itayumba?
 
Kama utafikiria hili jambo vizuri utagundua kuna njama kubwa ya kumchafua Maswi kwa kuwa anasimamia ukweli na maslahi ya taifa.
Daima tz anayefanya mema na haki hapendwi na pia hupuuzwa kwa kila asemalo na afanyaloo..

Binafsi nina kila sababu ya kumuunga mkono Mwasi kwa uamuzi wake ila tunahitaji uchunguzi kwasababau hakuna mwenye uhakika kama Maswi alisukumwa na uzalendo au la?Nimesoma mwanahalisi la trh 25/07/2012 na kukuta mambo ya utata kuhusu huyo Mwasi na uamuzi wake.Kwahiyo hapa kinachohitajika ni tume huru ya uchunguzi?

kwa upande wa TANESCO hakuna atakaekubali dhuluma hii, nami si waungi mkono hata kidogo.
 
Kwangu mimi hii ni dawa chungu sana kuimeza. Kuna hoja kubwa sana ya msingi, ni kwa nini wananunuliwa mafuta? Na maana yake ni nini, kuwa ndani ya mikataba hiyo tulijifunga kuwanunulia hayo mafuta for the foreseable future kiasi kwamba hakuna jinsi ya kujichomoa? Na je ndio wote tumekubali upofu wa moja kwa moja kuwa haya makosa hayawezekani kurekebishwa? Au ndio ile kauli ya Pinda kuwa tukifurumua nchi itayumba?
na kwa muda tu, kama vile tunavyokodisha Limo au costa bus kwa dharura zetu na ilikuwa kwa miaka miwili tu.. Sasa ajabu ni kwamba tumeikata miaka 7 na inaonekana limeisha kuwa jambo la kawaida tu..hakuna tena dharura ila ndio maisha na wabunge wanabishana tu nani kanunua mafuta ghali au rahisi wakati bill ya kila siku ni mabillioni ya fedha na kampuni kama hizi uchwara lini BP ikabadilisha jina kuwa Puma Energy kama sii kamba zao... Tutumie umeme tusitumie IPTL wanalipwa kwa siku na gharama ni zetu.. Sasa janga kubwa kweli liko wapi?..
 
Kuibuka kwa kashifa mpya inayomhusu katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini inaacha maswali mengi kuliko majibu. Katibu mkuu huyo anadaiwa kuipa tender kampuni ya PUMA ya kuiuzia IPTL mafuta mazito ya kufua umeme kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma. Taarifa zinasema aliingilia uamuzi wa TANESCO wa kuipa kampuni nyingine kazi hiyo kwa kile kinachodaiwa ni tofauti ya bei.......................

Watanzania hebu tutafakari mambo haya yafuatayo alafu tujiulize ni kwanini raisi na waziri mkuu wasijiuzulu au wawajibishwe
1. Kwanini wizara hii imekuwa kinara wa ufisadi tangu Kikwete aingie madarakani na ni hatua gani za kuridhisha zimechukuliwa mpaka leo?

Mkuu ufisadi katika wizara hii haujaanzia kwa Kikwete, tangu enzi za Mkapa sema tu kuwa kipindi cha Mkapa hata wabunge walikuwa hawaruhusiwi kuhoji kama ilivyo leo. Mkapa aliwafunga mdomo wabunge wa CCM. Kumbuka NetGroup Solution, mikataba feki ya madini, mkataba wa IPTL umesainiwa enzi za Mkapa, kujiuzia Kiwira kwa bei sifuri n.k

Binafsi namtetea Maswi alifanya kitendo cha uzalendo sana, afterall kaipa tenda kampuni ya serikali na kwa bei nafuu tunataka nini zaidi ya hicho jamani?
 
Kufuatia sakata la baadhi ya wabunge kushutumiwa kwamba wamekula mlungula ili wafanikishe kumuwajibisha waziri wa Nishati na madini na Katibu mkuu wa wizara hiyo, kwa kukiuka sheria za manunuzi ya umma, Nilimtweet Mheshimiwa Zitto Kabwe kuhusiana na kadhia hiyo., Ilikuwa hivi

Zitto Zuberi Kabwe‏@zittokabwe
Spika ni vema aikubali hoja ya ndg. Vita Kawawa kwamba suala la tuhuma kwa baadhi ya wabunge kuhongwa na #tanesco lijadiliwe mahususi >>

Me
@zittokabwe nakufuatilia sana mheshimiwa,, but kama vile utoe kauli maana these statement they meant u....tunapata shida ss wafuas wako


Zitto Zuberi Kabwe‏@zittokabwe
@Me usiwe mfuasi wangu. Fuata 'principles' ninazoamini. 'Justice' ndio msingi hapa. Sitatolea kauli tuhuma za kubumbabumba.


Zitto Zuberi Kabwe‏@zittokabwe
>> kwenye mjadala mahususi ushahidi utatolewa na watuhumiwa kujieleza. Vinginevyo hizi ni siasa tu zenye malengo Maalumu dhidi ya mtu fulani


Mheshimiwa Zitto aliendelea kutweet kwa kumquote Nguli wa mashahiri wa kiswahili Shabani Robert akionesha kushikilia msimamo wa yale anayoaamini.


Zitto Zuberi Kabwe‏@zittokabwe
Shabaan Robert alisema, "msema kweli huchukiwa na rafiki zake, sitaona wivu juu ya wale wapendwao na marafiki zao siku zote,">>
Zitto Zuberi Kabwe‏@zittokabwe
>> 'siwezi kuikana kweli kwa kuchelewa upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga.
 
Jana nilipigwa na butwaa alipoinuka mbunge wangu kuchangia ktk wizara ya nishati na madini. kwanza, Mh. Kigwangala kabla hajasema lolote alitamka kuunga mkono hoja zaidi ya mara moja, hili si la kushangaza kwa kuwa imekuwa ni pai ya wabunge wa chama chake kuunga mkono kitu chochote tu bora liende. Kilichonishangaza mimi kwa Mbunge wetu huyu wa Nzega ni msisitizo aliokuwa nao ktkt kuunga mkono hoja. alirudiarudia kuunga mkono na kisha kuanza kumwaga sifa kwa mawaziri husika. Mimi binafsi pamoja na wananzega wenzangu tumesikitishwa na mchango huo wa mwakilishi wetu. Kwa muda sasa tangu tumchague tumekuwa na matumaini mno na mheshimiwa Hamisi. Amekuwa mstari wa mbele kutetea hasa kuhusu mzozo wa kampuni ya kigeni RESOLUTE inayochimba madini ktk jimbo letu. Je? mh. anataka kutuambia kuwa sasa mgogoro huo umekwisha?. Mh., ktk suala hili ulijitoa mhanga kutetea wanyonge hadi ikafika kipindi ukasumbuliwa na polisi kama mtoto mdogo sasa imekuwaje?. ni nini kimekubadilisha mpaka kuchangia michango butu namna hiyo bungeni?. unasema kiwango wanachotoa wachimba madini wa kigeni kwamba kimeongezeka kutoka aslimia tatu mpaka kufikia nne, Je? hili nalo ni jambo la kujivunia wakati nchi zingine wanalipa nusu kwa nusu. Kwa kweli sifichi aliyechangia jana tarehe 27/07/2012 ktk bajeti na wizara ya nishati na madini siyo KIGWANGALA ninae mfahamu.
 
Mkuu Mkandara, kwa jinsi ninavyoelewa ni kwamba IPTL iko chini ya RITA (mufilisi) kutokana na kesi iliyofungiliwa na TANESCO miaka kama 3-4 iliyopita. Jaji wa hiyo kesi alikubali kwamba kwa kuwa IPTL iko chini ya mfilisi wakati mitambo yao bado ni mizima hivo basi haina budi TANESCO waendelee kuitumia hiyo mitambo kuzalisha umeme lakini mafuta wanunue wao. Kumbuka pia kipindi hicho kuna baadhi ya wabunge wa CDM walioshauri kuwa serikali iitaifishe kabisa hiyo mitambo.

Ninavyofahamu, tangu siku ya kwanza, mkataba unasema serikali ndiyo inunue mafuta. Ndio maana siku za nyuma serikali ilikuwa inahaha kubadili mitambo hiyo badala ya kutumia mafuta itumie gasi ya songosongo ili kupunguza gharama. Sijui huu mpango umekufia wapi..
 
Ngoja nitulie kwanza ndo nisome huu uzi. tuliishaongea sana lakini du serikali inapoongozwa na watu wasojali ndo hivo. wait a bit i shall come sometimes to read and comment..........
 
Nashawishika kusema hakuna aisiye fisadi viwango tu vinatofautiana hata kujamiikaforum wakati wa muda wa kazi ufisadi tu zitto anaweza akawa fisadi ngojea list ya membe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom