Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mheshimiwa Mhandisi Geoffrey Kasekenya amesema barabara Mianzini hadi Ngaramtoni Juu inafunguliwa upya kwani kuna maeneo ya km 8 hayakuwa na barabara kabisa lengo ni kuhakikisha Wananchi wa maeneo hayo ambao ni wafanyakazi wakubwa wa shughuli za kilimo, wanapata unafuu wa kuyafikia masoko Arusha Mjini kwa Urahisi, kwa haraka na kwa bei rahisi na itatumika pia kama Njia ya Mchepuo [Arusha By Pass] kwa ajili ya kupunguza msongamano kwenye barabara kubwa inayotoka Moshi - Arusha kwenda Namanga.
"Ukiacha hii barabara tulioweka jiwe la Msingi, tutajenga barabara nyingine ya njia nne kutoka Kisongo hadi Soko la Kilombero, tutajenga Km 10 tena njia nne hadi Usa River, Junction kwenda Arusha National Park, Serikali Itajenga KM 10 barabarani ya Kikavu mji wa Moshi na tunaendelea kufanya usanifu kuanzia Tengetu, Mbuguni hadi Merirani barabara hiyo ijengwe kwa kiwango cha lami, tunakamilisha Usanifu wa barabara ya kuanzia Longido kwenda Sia ili watu wanatoka Kilimanjaro kwenda Nairobi sio lazima wapite Arusha mjini" ameongeza Naibu Waziri Kasekenya.