Karume, Maalim Seif wakutana tena Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karume, Maalim Seif wakutana tena Ikulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Dec 12, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Salma Said, Zanzibar

  KATIKA kile kinachoonyesha kuimarika kwa uhusiano kati ya rais wa Zanzibar, Amani Karume na katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, viongozi hao wawili jana walikutana tena faragha Ikulu ya Zanzibar.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na mkurugenzi wa mambo ya nje wa CUF, zinasema kuwa kukutana kwa viongozi hao ni mwendelezo wa yale waliyozungumza walipokutana kwa mara ya kwanza Novemba 5 mwaka huu.

  "Ni kweli, katibu mkuu wa CUF amekwenda Ikulu na kukutana na Rais Karume. Walichozungumza bado ni siri. Lakini ni mwendelezo wa mazungumzo yao ya awali ya kutafuta maridhiano ya Wazanzibar na kuyaimarisha," alisema Jussa.

  Jussa alisema kuwa kama walivyoeleza viongozi hao wakuu wa vyama vikuu vya siasa visiwani Zanzibar, mazungumzo hayo ni endelevu na kwamba hiyo ni hatua ya pili.

  Ingawa kilichozungumzwa na viongozi hao kimefanywa siri, taarifa za awali ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa pamoja na mambo mengine, Seif aliwakilisha kwa Karume majina mawili ya wanachama wa CUF ambao chama hicho kimewapendekeza kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

  Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa anayepaswa kuwasilisha majina hayo kwa Rais Karume ni kiongozi wa upinzani kwenye Baraza la Wawakilishi.

  Tangu Karume aingie madarakani, Maalim Seif alikuwa hajawahi kukanyaga Ikulu na mara ya mwisho alikwenda kwenye makazi hayo ya rais wa Zanzibar wakati wa utawala wa Dk Salmin Amour.

  Ziara ya safari hiyo ilifanyika siku chache baada ya kiongozi huyo wa upinzani kurejea visiwani Zanzibar akitokea katika ziara ndefu ya barani Ulaya, ambako imeelezwa kuwa alieleza hali ya kisiasa inavyozidi kudorora.

  Baada ya mazungumzo hayo ya Novemba 5 si Ikulu ya Zanzibar wala CUF iliyotoa taarifa kwa vyombo vya habari wala kwa wanachama wake kuelezea kuwepo kwa mazungumzo kati ya Karume na Seif ambao vyama vyao vina upinzani mkubwa.
  Hata hivyo, siku chache baadaye Maalim Seif aliitisha mkutano wa hadhara na kutangaza kumtambua Karume kuwa rais wa Zanzibar, tamko lililoamsha hasira kwa wanachama wa CUF ambao walimzomea.
   
 2. B

  Bumbwini Member

  #2
  Dec 12, 2009
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi sana tunataka maridhiano ya haraka sana kuinusuru zenj,mungu yuko pamoja nanyi maalim seif na nduguyo karume undeni haraka serikali ya umoja wa kitaifa ili kuiokoa zenj na janga linaloinyemelea,inshaalah mungu atawawezesha mfikie pale dunia inapotaka penye maridhiano ya kweli na sio ubabaishaji tulio chokana nao,mungu wabariki maalim seif na amani karume mungu ibariki zenj na tanganyika yote.
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Amefanya vizuri sana kwa ajili ya uchaguzi mwakani na pia mimi siamini mambo haya yanaweza kuwa ni agenda tu ya kisiasa maana kuna ulazima kabisa kuwa Mwakani mambo yakawa mabaya sana maana sijui itakuwa vipi juu ya CUF na CCM na pia kama CCM wakishindwa wakubali pia
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  With 2010 around the corner, ni mwelekeo mzuri.
  Wafanye fasta wapange masuala yenye maslahi kwa Zanzibar ili kuzuia matatizo ya uchaguzi!
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hawa jamaa wamegundua kuwa WAO NI WAMOJA!
  ninachokiona hapa ni kwamba siku moja katika maisha watakuja kutoka na kauli moja YA KUTAKA NCHI YAO!
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi nakwambia mzee wangu ngoja tu uchaguzi uanze kule Zenji, Mambo yatabalika kabisa, baada ya kuona mambo ya CCM watabalika kabisa na pia CUF baada ya wanafanyiwa rafu watabalika sana, Bado naona kuna watu Conservative ndani ya CCM ambao wanakataa Muungano wala mabadiliko kabisa
   
 7. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Kuna kitu kimejifisha hapa, na ukizingatia kuwa Karume sasa hivi hatilii mkazo sana mambo ya bara, hata kwenye shughuli za muungano hatokei na hatoi sababu yoyote.
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  kinachonishangaza ni kwamba wakati maadui wanapatana visiwani,huku bara makamba anaendeleza vita,jana kamchafua kweli lipumba.

  hawa wazanzibari kuna kitu wameplan COLLECTIVELY
   
 9. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Wameshachoshwa na usanii na siasa chafu za muungano ufisadi na utawala usiobora kila sekta, bora wajenge serikali ya mseto na waiboreshe Znz.
   
 10. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #10
  Dec 12, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  How old is Makamba, labda siyo yeye ni umri.
   
 11. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  It is all about Politics mana kwa makamba kusema Lipumba ni keri kwako maana wote ni wajumbe katika vyama vyao husika
   
 12. B

  Bumbwini Member

  #12
  Dec 12, 2009
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu makamba hakuna asie mjua ni mropokaji ambae anabwabwaja kama mlevi wa pombe za kienyeji mataputapu,nazani watanzania woooote tunamjua makamba kuwa domokaya domo lisilo na breki hajui atendalo.
   
 13. Z

  Zanzibar Kwanza New Member

  #13
  Dec 12, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI 12 Disemba, 2009

  ‘Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru’, kitabu kipya kuzinduliwa rasmi

  Wapendwa Wanahabari,

  Ufunuo mpya juu ya uhalisia wa Mapinduzi yaliyofanyika Zanzibar mwaka 1964 sasa umo kwenye maandishi. Matukio na uchambuzi wa matukio hayo, ambayo yamekuja kuubadilisha kabisa mstatili wa mambo katika dola ya Zanzibar na majirani zake unawekwa wazi katika kitabu hiki kipya na cha aina yake, ambacho hakijawahi kuandikwa mfano wake kwa takriban nusu karne nzima iliyopita.

  Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru ni matokeo ya utafiti na ufuatiliaji wa kina wa Dkt. Harith Ghassany ambao ameufanya kwa zaidi ya muongo mmoja. Sasa kitabu kiko tayari na ndani yake muna maelezo ya kinagaubaga juu ya nini kilitokea, vipi kilitokea, wapi kilitokea, kwa nini kilitokea na, juu ya yote, nani hasa aliyekifanya kitokee na kwa malengo gani. Kinailezea upya historia ya Zanzibar, hasa ya tukio lile la Mapinduzi ya 1964, kwa kutumia mwanga na maneno ya wahusika wenyewe.

  Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru kimeandikwa kwa lengo moja kuu: udadisi mpya wa mambo. Kwa kutumia maneno ya mwanafalsafa wa Kiyunani, Socrates, “Maisha yasiyoathminiwa, hayana maana kuyaishi.” Mtazamo wa wananchi wengi wa kawaida, wanasiasa, wasomi na watafiti wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hata walioko nje, umekuwa wa aina moja panapohusika udhati wa Mapinduzi ya 1964 na, hivyo, historia nzima ya Zanzibar na Tanzania. Kitabu hiki sasa kinakuja na upande mwengine wa hadithi, na kwa hakika, upande halisi wa hadithi ya historia ya Zanzibar.

  Hiki ni kitabu kinachopaswa kusomwa na kila anayeutaka na kuujali ukweli. Ni kitabu kinachostahiki kuwa sehemu ya marejeo ya wasomi na watafiti wengine walioko vyuoni na kwenye taasisi mbalimbali za kitaaluma. Lakini zaidi, kwa wepesi wa lugha yake na mtiririko wa hoja zake, ni sehemu ya fasihi inayopaswa kuwa hazina kwa kila familia.

  Kuagizia kitabu hiki na au kupata taarifa zake zaidi, jiunge na mtandao wa Facebook kwa kubonyeza hapa.

  Mnakaribishwa nyote.
   
Loading...