Okay wewe ume- anticipate jambo litakalosemwa sasa.
Wanadamu wenzako ukiwakasirisha wanaweza kukuadhibu adhabu za Reviving Hell. Reviving Hell imesemwa ndio unapelekwa kama umemuua mtu mstaarabu.
Adhabu hizo ni kuchanwachanwa vipande,kugeuzwa kuwa barabara,kuingia kumi na nane za mfalme,kuchomwa na sindano,kuvutwa na kamba,kuanguka chini kutoka kwenye mgongo wa tembo,kuwa katika dhoiruba ya mchanga,kupigwa na marungu,kupigwa mjeledi,kuumwa kichwa,kujisikia moto au baridi,kutupwa katika korongo,kukamatwa na maadui,kukatwa korodani,kukatwa vidole,kunyofolewa nywele,kutapeliwa,kutumbukizwa katika lead au shaba inayochemka,pua yako kuchomwa na kitu chenye ncha kali,tamaa zako za miwili kuongezeka,kuvishwa mashada yanayowaka moto,kukatwa ngozi,kuwekwa kizuizini,kukatwa mwili wako,kupikwa katika sufuria au chungu,kuunguzwa kama tofali,kusuguliwa chumvi kwenye majeraha,kufagiwa kwa ufagio,kuunguzwa,kukatwa vidole,kukatwa vidole gumba halafu kuchomwa moto,kulamimishwa kula pilipili nyingi,kumeza mapovu ya bahari thelathini,kupigwa namikono na miguu,kupelekwa mbali,kung'olewa meno,kuunguzwa na mafuta,kupigwa kama dhahabu,kuvimba sana.
Kwa hiyo binadamu wenzako wanaweza kukuadhibu hizi adhabu za Reviving Hell lakini ukifa ukienda Relentless Hell hizi adhabu zitaongezeka mara mia.
Endelea mkuu hizo Jehanamu zipo Mbingu ya ngapi au zipo hapahapa duniani?
Huyu anakwenda agera anaadhibiwa,halafu anazaliwa tena Duniani katika maisha ya mateso.
Karma yake akiilipa anarudi Duniani.
Na mtu naye anakufa anapenda Mbinguni,anastarehe: naye pia,wema wake mara nyingi ulikuwa ni wema mdogo si wa kumfanya yeye akae Mbinguni milele. Yeye pia wema ukiisha anarudi kuzaliwa Duniani. Lakini maisha yanakuwa mazuri; labda atakuwa Diwani au atakuwa tajiri.
Kufanya wema ni kila kitu. Ukiona mambo yako yanaanza kwenda vibaya ujue ndio "nauli yako imeishia hapo" lazima ufanye wema tena kama unataka kuishi vizuri.
Ndio watu wanafanya wema,wanahawa hela,wanaambiwa wanataka rushwa,hii inaleta utata kidogo.
Yaani atumie hela zake kichoyo,halafu ndiyo aitwe ana thawabu. Watu wanampeksheni huyo mgombea,wanajua akishachaguliwa hawamuoni tena.
Hii ni Buddhist Sutra inaitwa The Application of Mindfulness of the Sacred Dharma.