Jibu langu lili-reflect statement yako...
Ilionesha mambo manne ama zaidi ndani yake:
1. JF ni ya chadema (membaz wa chadema). Hili uongozi wa jf ulishalikanusha tangu katibu mwenezi wa chama chenu alipotoa tuhuma kama hizo.
2. Memba wa jf huwa wanahudhuria kwenye misiba ya membaz wenzao tu (hata kama ni kweli sioni tatizo hapo)
3. Msiba ukiwa ni wa mwanachadema basi wanachadema lazima wahudhurie (hili pia sioni tatizo lake)
4. Ukiona watu maelfu kwa maelfu wamehudhuria msibani basi ujue kuwa aliyekufa ni mwanachadema.
Hiyo ya nne ndo iliyonifanya niamini kuwa kweli Dr. Slaa aliibiwa kura. Kama wanachadema wanaweza kujitokeza kwa wingi namna ile kwenye msiba ni wazi kuwa kwenye uchaguzi ni vivyo hivyo kwani nchi yetu sasa hivi ni kama ipo msibani, na kama umati huo wote una mapenzi na chadema ni aglabu watu hao wataichagua chadema. na kama wameichagua chadema halafu eti haikushinda...kura zimeenda wapi?
Na kwa kuwa nimeona mara nyingi ukiikejeli chadema na ukijiweka karibu na magamba, nakuchukulia kuwa wewe ni mmoja wao.
Kama wewe ni dereva wa taxi, majambazi watatu wakakukodi mkafanye uhalifu, askari wakiwatia mbaloni watasema tumekamata majambazi wanne.