Karibuni wadada/wamama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karibuni wadada/wamama

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kimbweka, Feb 11, 2011.

 1. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii nimeikuta sehemu fulani, nikaona ni vyema niikandamize huku JF huenda ikaleta changamoto ama kwa kujikumbusha ama kwa kutilia mkazo na kadhalika hasa hiki kipindi tuiendeapo ileeee siku ya wapendanao. Haya embu soma hii:

  LEO nataka tukumbushane kitu kimoja nacho ni jinsi ya kumfanya mwenzi
  wako aonekane maridadi wakati wote. Hapa nazungumzia wale walio katika
  mahusiano ya kudumu ambao wanaishi pamoja.
  “Nikiamka asubuhi jambo la kwanza ni kumuandalia mume wangu maji ya
  kuoga, nahakikisha nguo zake zimepigwa pasi, viatu vimeng’arishwa,
  soksi ziko safi, na akivaa lazima nimfunge tai, na nguo za kazini mimi
  ndiye nachagua siku hiyo avae nguo gani” anasema Mama mmoja mkazi wa
  Kimara Jijini Dar es Salaam.
  Sikiliza na hii “ Mimi mume wangu huwa anaandaa nguo zake mwenyewe
  anafua, apige pasi au asipige shauri yake, aoge asioge atajijua, huo
  muda sina kabisa siku hizi” anasema mwanamke mmoja Mkazi wa Buguruni
  Jijini Dar es Salaam.
  Siku zote tumekuwa tukisisitiza urembo kwa wanawake na utanashati kwa wanaume.
  Mmoja ya jukumu la mwanamke ni kuhakikisha kuwa, mwanaume wake anakuwa
  maridadi na mwenye kuvutia. Jaribu kuangalia ni nguo za aina gani mume
  akivaa zinampendeza na hapo unaweza kumchagulia shati na suruali
  ambazo rangi zake zinaendana na hata akivaa zitamfanya apendeze.
  Pia suala zima la kufua na kupiga pasi vizuri ni moja ya njia ya
  kuonyesha kuwa unamjali na unamjengea namna ya kujiamini
  zaidi.Utunzaji wa soksi ikiwemo ufuaji wa nguo za ndani ni jambo
  linalosisitizwa sana kwani wanaume wengi wanaonekana kutojali sana
  vitu hivyo ama kutokana na muda au kwa kukosa ushirikiano wa wenzi wao
  katika kutunza na kufanyia usafi aina hizo za nguo.
  Jamani mwanaume akiwa maridadi au mtanashati huwa anamvutia kila mtu
  na zaidi sifa zinakwenda kwa mkewe ambaye anaaminika kuwa ni chanzo
  cha mwanaume kuwa msafi.
  Jenga mazingira ya kujali usafi wa nguo za mwenzi wako ili kuhakikisha
  kuwa kila kitu kinakwenda sawa.
  Pia kuna wanawake wengi ambao ni wajuzi wa kufunga tai, kama hilo bado
  hulifahamu tafuta mtu ambaye atakufundisha namna bora ya kufunga tai
  ili uweze kumpendezesha mume wako.
  Kama unapita dukani au sehemu zinakouzwa nguo si vibaya kama unaona
  kuna nguo inaweza kumfaa mwenzi wako mna ukahakikisha kuwa akivaa
  anapendeza usisite kununua kwani itakuwa ni zawadi nzuri sana kwake.
  Jaribu kuwa na tabia ya kumvika mwenzi wako, si kuacha kila kitu
  afanye yeye kuanzia kufua, kupiga pasi na hata kung’arisha viatu.
  Ni vizuri kama utaamua kuhakikisha kuwa, unamuaandaa mume wako kabla
  ya kwenda kazini kisha na wewe kuendelea na shughuli zako.Hilo
  litaongeza upendo na amani kwenye nyumba.
  Wanawake wengi wamejisahau sana na kuacha wanaume wafanye kila kitu
  wenyewe jambo ambalo husababisha wanaume wengine watoke nyumbani bila
  kupiga pasi au kusahau kuchana nywele.
  Jirekebishe kama una tabia za kutojali usafi wa mwenza wako,
  utanashati ni muhimu kwa wanaume pia usiishie kwa wanawake kujipenda
  na kujiremba kila wakati huku wakisahau waume zao
   
 2. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,562
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Here we go again
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Still more to come broda
   
 4. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  asante
  ntamwogesha ,kumvalisha,kumtana nywele na kumpa kiss mlangon wakat anatoka


  dahh nilijisahahu bwana na i ndoa yangu inayokarbia kufika miaka 50...ANNIVERSARY JUMATATU.karbun
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sasa niliona nikukumbushe maana mambo yalianza kwenda mrama! Embu tukumbushe nasisi midume tunayopaswa kufanya...
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Haya ndio mafunzo wayapatao wamama Kitchen party!
  Mh kazi kweli kweli!
   
 7. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kUWAI KURUD NYUMBAN
  kumshirikisha mipango
  kumsapot anachokifanya
  kudirect,kumshauri kumfanya awe rafik na sio habar za CHACHA MWITA....aiisseee mimi mwanaume azihitajiki,..
  kutoa poket money...(km unayo usiwe mbahili)

  usipige kaz za nje
   
 8. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Asante kwa kitchen party, will do that.
   
 9. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Asante rose!!:hungry:
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Haya mama! Hapo kwenye red patamu tehteh tehe
   
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Bado inakuja bedroom party ....
   
 12. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #12
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na wanaume wafanyeje wao? miaka nenda rudi ni sisi tu,sasa nafikiri na majukumu yao yawe defined,asante sana umetukumbusha wajibu!
   
 13. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tukumbushe tu mama tutafanya si ndiyo mapenzi yenyewe!!!!
   
 14. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kazi za nje muhimu Rose wenzio wataliwazwa na nani?
   
 15. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Na kumfulia nguo za ndani?????? huku ni kuwaendekeza sasa.
   
 16. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Nadhani ni mapenzi na maamuzi siyo JUKUMU hili. Kila mtu ajali usafi wa mwenzie na kuvaa kwa mwenza wake..matendo ya kupenda na kujali yawe pande zote siyo tu kwa wanaume!!..
   
 17. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Utumwa huu!..period!
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Na anaemwandaa mwanamke ni nani?
   
 19. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #19
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anajiandaa mwenyewe!kila mtu na aishi maisha yake,kuna vitu vingine havifanyiki mpendwa!
   
 20. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #20
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa,nguo ya ndani afuliwe,?utumwa huu kweli!
   
Loading...