KARIBUNI; Usiku wa SUGU Dar-LIVE, May 27!!

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
Gwiji wa Hip Hop, aliye pia Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu' atakuwa na usiku maalum kwenye Ukumbi wa Dar Live, uliopo Mbagala Zakhem, Dar es Salaam.



sugureloaded.jpg



Sugu, ameahidi kufanya shoo ya ukweli siku hiyo na ameelekeza kwamba kipato chake chote kwenye shoo hiyo, kitaelekezwa kwenye mfuko wake wa elimu, jimboni kwake.
"Itakuwa siku muhimu kwa mashabiki wa Hip Hop, itakuwa mzuka kwa mashabiki wangu. Najua wengi wamekuwa wakijiuliza ni lini watapata fursa ya kuniona jukwaani, nawaomba waje Dar Live Mei 27.

"Nilishaahidi kwamba sitafanya shoo za biashara, ila nitafanya shoo za harakati. Hii ya Dar Live imenivuta kwa sababu inaniwezesha kuchangia mfuko wangu wa elimu. Kwa hiyo, nawaomba mashabiki wangu na wana Mbeya, waje ili wapate burudani na wakati huohuo wachangie elimu kwenye jimbo letu," alisema Sugu.


"Pamoja na shoo za harakati ila naangalia pia sehemu ya kufanyia onesho. Dar Live imenivutia kwa sababu ya taa zake, sound (muziki), jukwaa ni vya kiwango cha juu, kwa hiyo nina kila sababu ya kufanya shoo ya nguvu sana siku hiyo." alisema Sugu.

SOSI; deiwakaworld.com
 
Back
Top Bottom