Timor
Member
- Feb 4, 2009
- 48
- 32
Nafurahi tena kupata wasaa huu kuwasalimu waJF wote pamoja na kuwashukuru kwa michango yao wakati wa sakata lile la ukombozi pale Peacock Hotel.Kwa sasa hivi niko nchini Uturuki kwa kazi ya hotel.Ilikuwa ni bahati tu katika kueleza tabu niliyoipata nilipata msamaria aliyenileta hapa Uturuki kufanya kazi SIYO ZA UBEBAJI WA MABOX bali professinal jobs .Hakika nayafurahia maisha hapa kwani kipato ninachokipata sasa ni mara mia sita ya kile nilichokuwa nakipata huko TZ.Nawakaribisha vijana wenzangu wenye fani kama yangu waje kazi nje nje hapa na maisha ulimsuwano kabisa.Sitaacha kuwakumbuka wana JF kwa harakati zao za ukemeaji wa maovu hususani ya udhalilishaji wa wanawake