Sijawahi kufika Ruangwa, lakini mazungumzo yako katika habari hii yamenifanya niamini kwa asilimia mia (100%). Kwanza, ni kutokana na huyo unayemzungumzia. Nadhani sio mimi tu nimeamini maneno yako; wapo wengi wameamini uliyoyaandika.
Kuna watu wakizungumziwa kuwa wameleta maendeleo mahala fulani, unaweza kushangaa na kuhoji jambo hilo, kwa kuwa hawakuzoea kumwona akifanya hivyo. Kwa Majaliwa, hakuna asiyejuwa utendaji wake. Najaribu kufikiria, hii husababishwa na nini?; ni tabia ya mtu, malezi aliyopewa na wazazi wake, au ni shinikizo?
Kwa mtu anayemfuatilia mzee huyu atagundua kuwa Majaliwa alikulia kwenye maadili mazuri. Kwa hiyo anachofanya sasa hivi sio maigizo, bali ni tabia aliyonayo tangu utotoni mwake. Lakini pia alikomazwa zaidi alikopitia katika maisha yake; shuleni, vyuoni, kazini, nk.
Nawapongeza Wanaruangwa, mmepata jembe, mtafika mbali sana, hayo mnayoyaona sasa ni manyunyu tu, mvua yenyewe bado.