Karibuni kwa wazo la biashara ya kukodisha baiskeli

BrazakakaBura

Member
Feb 16, 2017
88
103
Habari wakuu,, natumaini ni wazima wa afya njema,, kwa wenye matatzo Mungu awafanyie wepesi mpone tuendelee na harakati za kujikwamua kimaisha.

Naitwa Brown Job wazo langu kuhusu biashara ya kukodisha baiskeli lilikuja baada ya kufatilia vzuri jinsi biashara hii inavokwenda,, kwa kiasi cha mtaji wa 500000/= laki tano,,,
kama kiasi cha kuanzia tu, lakin inawezekana kuanza hata zaidi ya huo mtaji.

Mchanganuo;
Nitanunua baiskeli tano kila baiskeli sh.100000/=
5 baiskeli= 500000/=
hiyo garama ni pamoja na usafirishaji kutoka dsm hadi moro eneo husika.
baiskeli moja itakodishwa kwa sh 200/= kwa saa moja na 2000/= kwa mtu anayekodi kutwa nzima.
baiskeli moja itaingiza sh2000/= kwa siku ni sawa na sh10000/= kwa baiskeli tano kwa siku moja.
Hivyo ni sawa na 300000/= kwa mwezi kwa baiskeli tano. HAYO NI MAKADILIO YA CHINI KABISA.

Changamoto;
1)Kuharibiwa baiskeli
2)Kuibiwa/kutoroka nayo
Udhibiti wa changamoto kuhusu kuharibiwa baiskeli.... baiskeli inakaguliwa mara baada ya kurejeshwa na endapo itabainika kuwa na tatzo ni juu yake na pia baiskeli inakaguliwa ili kubaini kama kuna kifaa kimebadilishwa pia sehem muhim za baiskeli huwekwa alama za utambulisho.
Kuhusu kutoroka na baiskeli,,,,, baiskel inakodishwa kwa mtu anayefahamika tu ama awe na mtu anayemfahamu maeneo hayo

Ili kulinda ubora wa baiskeli hufanyiwa marekebisho madg mara kwa mara.
baada ya miezi 6 nitakusanya 2m.

Hayo ni makadilio ya chini kabisa na ni kwa baiskeli tano tu.
karibuni kwa mawazo na ushauri wakuu pia jinsi ya kufikia utekelezaji naombeni ushauri wenu maana mtaji ni changamoto
 
Mkuu hizi baiskeli zilikuwa zinafanya kazi ya kukodishwa kutokana zishakuwa kuukuu nauza tu

Zipo mbili ambazo zinaafadhali na mbili kama fremu, za kufanyiwa service zote nauza 20,000/= tu
IMG_20180820_172136.jpg
IMG_20180820_172155.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni biashsra nzuri kwa mtu usiyemfahamu akuachie hata dhamana kama simu yenye thamani zaidi ya baskeli.


Hiyo hesabu inategemea Na ulipo maana sehemu nyingine baskeli inaingiza 600 ikizidi sana 1000 . unakuta inashinds sana kijiweni kuliko barabarani
 
Ukipata kakijiwe kazuri itakulipa sana,haswa kuwakodishia wa maeneo hayo unaowafahamu,kila la kheri mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom