Mara ya mwisho nilifika Kivukoni mwaka 1994; kwa hiyo sijui leo panafananaje. Ila kulingana na picha ulizoweka hapo, sioni kama kuna mabadiliyo yoyote ya maana. Kuwa msongamano mkubwa sana wa watu na mazingira yake ni mchafu kama ilivyokuwa wakati huo. Ninadhani kuwa uchafu huo unatokana zaidi na msongamano wa watu, lakini nisichojua ni kwa nini watanzania tunapenda sana misongamamno ya watu. Hebu angalia ukiwa mitaani, hasa Kariakoo, utashangaa misongamano ilivyo; inawezekana kuwa inatokana na imani yetu potofu kuwa maana ya mji ni msongomano. Ni vigumu hata kwa polisi kumfuatilia mhalifu ndani ya misongamano ya aina hiyo, na likotokea jendawazimu moja na bunduki likarusha risasi hovyo hovyo kama hilo lilitokea huko Colorado, basi litaua watu wengi sana mitaani mwetu.