Karibuni Ikwiriri....!!!

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,047
21,522
Habari wakuu,

Sasa hivi yapata ni mwezi sasa tangu nimehamia huku Ikwiriri katika harakati za kufanya ujasiriamali. Kwa wasiopafahamu, Ikwiriri ipo katika mkoa WA pwani, kata ya rufiji. Ipo njiani kama unaenda mhoro/lindi/mtwra/nachingwea.

Watu wa huku ni wakarimu sana, ila cha ajabu wengi wao asilimia kubwa ni wasukuma. Hawa jamaa zangu aisee ni madon kwelikweli na ukiwakuta baa ndio utafurahi na roho yako. Kuna bar moja inaitwa Eagle huwa wanapenda sana kwenda pale kwa sababu Kuna jukebox, basi utaskia mhudumu niletee Costa (akimaanisha castle) halafu shika hii Mia 3 weka kangwaru tatu..

Ukiachana na hayo, bar huku zinafunguliwa mapema sana asubuhi na hakuna limit ya Muda WA kuuziwa pombe wewe unaweza kuanza kunywa 12 asubuhi mpaka 8 usiku. Pia, wanawake wengi wa huku ukiwaangalia miguuni wamevaa vile wanaita vikuku miguu yote miwili, sijajua ni utamaduni wa pwani au labda huduma ya kuchimba gesi inapatikana.

All in all karibuni Ikwiriri mle nyama za mbuzi kama zote.

Weekend njema wakuu
 
Wasukuma wamejaa kila kona ya Tanzania! hawa watu wanzaana kwelikweli, nilikwenda kule Nkasi Sumbawanga nikawakuta wengi tu, wakiwa na ngoma yao ya chaguranga!
 
Habari wakuu,
Sasa hivi yapata ni mwezi sasa tangu nimehamia huku Ikwiriri katika harakati za kufanya ujasiriamali. Kwa wasiopafahamu, Ikwiriri ipo katika mkoa WA pwani, kata ya rufiji. Ipo njiani kama unaenda mhoro/lindi/mtwra/nachingwea. Watu wa huku ni wakarimu sana, ila cha ajabu wengi wao asilimia kubwa ni wasukuma. Hawa jamaa zangu aisee ni madon kwelikweli na ukiwakuta baa ndio utafurahi na roho yako. Kuna bar moja inaitwa Eagle huwa wanapenda sana kwenda pale kwa sababu Kuna jukebox, basi utaskia mhudumu niletee Costa (akimaanisha castle) halafu shika hii Mia 3 weka kangwaru tatu..
Ukiachana na hayo, bar huku zinafunguliwa mapema sana asubuhi na hakuna limit ya Muda WA kuuziwa pombe wewe unaweza kuanza kunywa 12 asubuhi mpaka 8 usiku. Pia, wanawake wengi wa huku ukiwaangalia miguuni wamevaa vile wanaita vikuku miguu yote miwili, sijajua ni utamaduni wa pwani au labda huduma ya kuchimba gesi inapatikana. All in all karibuni Ikwiriri mle nyama za mbuzi kama zote. Weekend njema wakuu
Eagle bar yangu enzi hizo kabla sijahama.....wasukuma wakiingia hapo ni full shangwe yaani mtakunywa hata msiohusika ....napapenda sana ikwiriri
 
Eagle bar yangu enzi hizo kabla sijahama.....wasukuma wakiingia hapo ni full shangwe yaani mtakunywa hata msiohusika ....napapenda sana ikwiriri
Hahaha kweli mkuu, ulikua unapenda kukaa angle gani au pale ghorofani juu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom