Karibuni Liwale

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,573
44,803
Liwale ni wilaya inayokuwa kwa kasi sana kiuchumi na inajengeka mno tofauti na Ruangwa ambayo boss Majaliwa anaiforce iwe mji ila Karuangwa ni kadogo kama ngumi, kamji gani kama tarafa?

Liwale ina fursa sana ukianzia na ufuta, alizeti na korosho. Korosho ya Liwale ni bora ukilinganisha na ya pwani. Matajiri wengi wa Liwale hapo zamani walitajiriki kupitia ujangili wa meno ya tembo ila serikali Ilipokataza ujangili wakaamua kujiingiza katika kilimo.

Wageni wengi Wamakonde toka Newala wamekuja kufanya biashara hapa Liwale. Wasukuma pia wengi wanafuga mifugo yao kwa kuwa ardhi ipo ya kutosha Liwale, ni kubwa sana kuliko hata mkoa wa Kilimanjaro.

Uwepo wa Mbuga ya Selous upande wa Kaskazini Magharibi inayoambaa mpaka Tunduru na upande wa Mashariki kuna msitu mkubwa wa hifadhi kunaifanya Liwale iwe na hali ya hewa nzuri na mavuno ya uhakika.

Shida ya Liwale ni changamoto ya barabara, wilaya imetengwa sana kuikuta Kilwa Nagurunguruku km 203 na kupitia barabara ya Nachingwea km 160 na zote ni vumbi.

Mbali na utalii Liwale unaweza kuwekeza kwenye lodge, kwani wakati wa msimu wa korosho na ufuta huwa panajaa wageni sana.

Hapa halmashauri ya Liwale viwanja bei ni sawa na bure, na pako flat pia, water table iko juu uki drill mita 30-50 unapata Maji matamu hivyo kama una shamba utafanya yote mpaka ufugaji bila adha yoyote.

Liwale pia panasifika kwa uchawi wa ngende, kuna sehemu kuna bwawa hilo hapo kuna ushirikina wa kila aina, na sio matapeli, unapewa tiba unaambiwa ukifanikiwa ndio urudi kutoa asante. Ila ukiwa njiani baba usiongee na mtu yoyote mpaka ufike nyumbani.

karibuni Liwale, karibuni Lindi, karibuni Kusini.
 
Nilipapenda ukiwa na mifugo kwa kweli unafaidi mno na kilimo jamani. Yaani nikiishi huko ,ndugu akitoka Tarime kunitembelea inabidi atumie siku tatu ama nne kufika huko so itakuwa tizi mno.ila wakija kuweka lami huko patakuwa mwake mno

Liwale kuna pesa si ya kitoto. Ukitaka investment nenda Liwale. Wananchi sio wachoyo hata shamba unapewa bure ukalime kwa muda.
 
Liwale ni wilaya inayokuwa kwa kasi sana kiuchumi na inajengeka mno tofauti na Ruangwa ambayo boss Majaliwa anaiforce iwe mji ila Karuangwa ni kadogo kama ngumi, kamji gani kama tarafa?

Liwale ina fursa sana ukianzia na ufuta, alizeti na korosho. Korosho ya Liwale ni bora ukilinganisha na ya pwani. Matajiri wengi wa Liwale hapo zamani walitajiriki kupitia ujangili wa meno ya tembo ila serikali Ilipokataza ujangili wakaamua kujiingiza katika kilimo.

Wageni wengi Wamakonde toka Newala wamekuja kufanya biashara hapa Liwale. Wasukuma pia wengi wanafuga mifugo yao kwa kuwa ardhi ipo ya kutosha Liwale, ni kubwa sana kuliko hata mkoa wa Kilimanjaro.

Uwepo wa Mbuga ya Selous upande wa Kaskazini Magharibi inayoambaa mpaka Tunduru na upande wa Mashariki kuna msitu mkubwa wa hifadhi kunaifanya Liwale iwe na hali ya hewa nzuri na mavuno ya uhakika.

Shida ya Liwale ni changamoto ya barabara, wilaya imetengwa sana kuikuta Kilwa Nagurunguruku km 203 na kupitia barabara ya Nachingwea km 160 na zote ni vumbi.

Mbali na utalii Liwale unaweza kuwekeza kwenye lodge, kwani wakati wa msimu wa korosho na ufuta huwa panajaa wageni sana.

Hapa halmashauri ya Liwale viwanja bei ni sawa na bure, na pako flat pia, water table iko juu uki drill mita 30-50 unapata Maji matamu hivyo kama una shamba utafanya yote mpaka ufugaji bila adha yoyote.

Liwale pia panasifika kwa uchawi wa ngende, kuna sehemu kuna bwawa hilo hapo kuna ushirikina wa kila aina, na sio matapeli, unapewa tiba unaambiwa ukifanikiwa ndio urudi kutoa asante. Ila ukiwa njiani baba usiongee na mtu yoyote mpaka ufike nyumbani.

karibuni Liwale, karibuni Lindi, karibuni Kusini.
👀👀
 
Back
Top Bottom