Tunatafuta wanachama wa kukidhamini chama tunachotaka kukisajili hivi karibuni jina la chama (tunapendekeza kiitwe - Arusha Declaration Alliance kinachofuata misingi ya Azimio la Arusha. Tafadhali tukutane;
MUDA: 26 Novemba, 2016, Jumamosi, kuanzia saa 8 mchana.
UKUMBI: RAMADA ENCORE HOTEL, City Centre, Opposite Exim Tower (Posta Mpya) - Dar es Salaam.
MGENI WA HESHIMA: JULIUS MALEMA (MB) kutoka Afrika ya Kusini
MAWASILIANO: +255 654 828025 (Ms. Warda - Kaimu Katibu Mwenezi & Mr. Frank - 0715734747 Kaimu Mweka Hazina)
NB: T-shirt, Kofia, Khanga, Chakula, Vinywaji na Nauli (Tshs. 380,000/=) vitatolewa kwa watakaohudhuria tu.
LIDUMU AZIMIO LA ARUSHA
Huu ni uharibifu wa kisiasa ambao hauna tija kwa maendeleo ya Watanzania hata chembe. Huwezi kuanzisha chama kwa dhana ya Azimio la Arusha ambalo hata hivyo linahitaji marekebisho mengi ili kuendana na hali halisi ya uchumi wa dunia na mahusiano ya kimataifa kwa sasa.
Sioni jema lolote lenye uhalisia sahihi litapatiana kwa kukopi na kubandika Azimio la Arusha kama lilivyoandikwa 1967 chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na mtangamano dhaifu wa muingiliano wa kimataifa. Ama ni vigumu kwa yeyote kusema ananguvu za kupingana na mabadiliko ya dunia yanayotokea kwa kasi katika nyanja zote.
Wachambuzi wa siasa wataniunga mkono kwamba Azimio la Arusha kama lilivyo haliwezi kuhimili mazingira yalipo sasa duniani. Linahitaji maboresho. Na kama litaboreshwa, siyo azimio la Arusha tena. Kitakuwa kitu kingine.
Pili mambo mengi yaliyomo katika Azimio la Arusha ni mazuri tu na yanafaa lakini hayawezi kujitosheleza. Hivyo ni mchakato mkubwa sana unahitajika kubumba kitu kinachoweza kuleta tija katika misingi ya Azimio la Arusha.
Hata hivyo, kama ndivyo, kuna vyama vingi vya siasa Tanzania ambavyo vinaonyesha mwanga wa kusimamia maslahi ya taifa ingawa vinahujumiwa. Kwa maana ya kwamba, maono yao yanatumiwa kuwahadaa Wtanzania kisha yanachakachuliwa na hatimaye kutekelezwa kwa namna isiyo sahihi na hivyo kupoteza mwelekeo na maana nzima ya dhana hizo.
Kama kweli kila Warda, Frank na wenzako mnalengo jema, jiungeni na vyama vya siasa kimojawapo kilichopo chenye nia ya dhati, kisha mkae mboreshe kwa ku incorporate agenda zilizomo katik aAzimio la Arusha ili kuimarisha nguvu ya upinzani ingawa Tanzanaiupinzani una nguvu kuliko chama wengine.
Hiyo itaonyehsa uzalendo na uwezo wa kushirikiana na watu wengine katika kusimamia na kulinda maslahi ya Watanzania. Kuanzisha chama kipya ni ishara ya ubinafsi na udhaifu mkubwa wa ki uongozi lakini ipia wenye lengo la kuimarisha migawanyiko katika kura na inaweza kutafisiriwa kama uwakala wa hujuma kwa upinzani.
Vyama vilivyopo vinatosha, ila kama kuna wazo jipya itafutwe namna ya kuviboresha badala ya kila mwenye wazo anaanzisha chama. Viongozi wa vyama vya upinzania, fungueni milango ya kupokea maoni mapya ya kuboresha vyama venu kila inapobidi kama inaonekana ni sahihi.