Nimepakumbuka sana Bunda. Nilikuwapo huko mwaka 2005, kipindi cha uchaguzi. Nakumbuka Bunda ni kama njia panda. Barabara ya Mwz-musoma, kwenda Mwibara na pia Nyamuswa. Nilikuwa nalala guest inaitwa White house unapoanza tu barabara ya kwenda Nyamuswa. Ilikuwa kipindi cha uchaguzi. Watu wa Tarime walikuwa wanakimbilia Bunda maana hali haikuwa shwari huko! Ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona ugali wa ulezi.
Umenikumbusha mbali sana Mkuu! Asante sana. Huo utakuwa ugali wa Muhogo!