Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo(1 Kor. 13:13).
Siyo ajali kuwa orodha ya Paulo inayoeleza sifa za kitabia zinazotambulisha tunda la Roho huanza na upendo. Upendo ni sifa kuu kwa Mkiristo kwa vile ni sifa inayoelezea sifa ya tabia ya Mungu. Ni upendo uliomsukuma Mungu kutuumba, kututunza, na kujifunua mwenyewe kwetu, na kutupatia mwanawe ili aje kutukomboa.
Yohana huelezea kinaganaga na kwa maneno rahisi kuwa--"Mungu ni upendo" (1 Yohana 4:16). Kwa sababu upendo ni kiini cha tabia yake, upendo wapaswa kuwa kiini cha tabia yetu pia. Naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake (1 Yohana 4:16).
Kwa masikitiko, neno upendo hutumiwa visivyo siku hizi. Mara nyingi tunasema tunapenda hali ya hewa, tunapendelea chakula fulani tunachokipenda, tunampenda mbwa wetu. Lakini aina hizi za upendo hazikidhi kipimo cha upendo wa kweli wa Mungu(soma 1 Wakorintho 13). Upendo ni kitu tofauti kabisa, kitu fulani kinachoathiri maisha yetu kwa ujumla, mwenendo wetu, na namna tunavyohusiana na wengine. Viambato vya upendo ni kifurushi kimoja, na siyo orodha ya vitu ambavyo tunachagua vile vinavyotuvutia na kupuuza vingine.
Karibuni wanajamvi wote, tujadiri katika UPENDO.
Nakala kwa: Ntuzu Nkwesa Makambo Eiyer tedo juve2012 Blueband Ls man charminglady na wengine wote.

Last edited by a moderator: