Karibu Tujadili Kuhusu Upendo

Karibu Tujadili Kuhusu Upendo

Asante sana mtoa mada mungu akubariki....!!!!
Amri kuu ni upendo......
Upendo ni kila kitu....
Hata ustawi wa dunia unategemea upendo...
.........akamuuliza tena mara ya tatu je simion petro unanipenda unanipenda kuliko hawa....? Wewe bwana wajua.....
Upendo ni kila kitu
ameen
 
Kile Upendo Unachofanya (1 Kor. 13:4-8)
"Upendo huvumilia, hufadhili, … haufurahii udhalimu, … bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neon wakati wo wote" (1 Kor. 13:4-8).
Kuufasili upendo ni hatua ya kwanza; hatua inayofuata ni kuuweka upendo katika vitendo. Ni lazima tuwe na hadhari ya kuwa wepesi kusema tunapenda; badala yake tunahitajika kuchunguza kwa makini namna tunavyoishi na ni kwa uzuri kiasi gani tunatekeleza kanuni za upendo kama zinavyoelekezwa katika Biblia.
Soma 1 Wakorintho 13:4-8. Angalia kila Nyanja ya maana ya upendo, na kasha jihoji, Ni kwa jinsi gani naweza kutekeleza kanuni hizi nyumbani mwangu?
Tafakari kwa muda kazi zetu zingalikuwaje iwapo kwa neema ya Mungu tungalidumisha sifa za upendo wa kweli. Fikiria mibaraka ya kuishi katika mazingira ambapo wana – familia wanapendana na kutiana moyo. Pengine huwezi kuwafanya wengine wakutendee hivyo, lakini kama utatekeleza kanuni hizi, utaweza kuona jinsi zilivyo na mguso wa nguvu kwa wengine. Huwezi kubisha dhidi ya upendo; ni nguvu kuu kuliko zote katika uumbaji wote. Watu waweza kubisha juu ya teolojia yako, mtindo wako wa maisha, itikadi zako, Imani yako-naam, kila kitu. Lakini ni hoja gani waweza kutumiadhidi ya upendo usio na masharti, aina ya upendo uliofunuliwa kwa ulimwengu kupitia kwa Yesu kristo, aina ya upendo ambao sisi, kwa neema yake, tunaweza kuudhihirisha kwa wengine?
Ni sifa zipi za upendo wa kibiblia unazoona vigumu kuzitekeleza maishani mwako? Ni kwa vipi kwa neema ya Mungu waweza kuweka bidii katika kukuza kipengele hiki cha upendo? Kwa nini ni mhimu kwamba ufanye hivyo?
 
Kipimo Cha Upendo (Mat 5:43-48)
Soma Mathayo 5:43-48. Ni hoja gani muhimu Yesu anayotwambia kuhusu upendo?
Kama tunapaswa kuwapenda adui zetu, ni vyema kutambua ni nani hasa walio maadui zetu? Iwapo adui ni yule tu anayetishia uhai wako, waweza kudhani aya hii haikuhusu, kwa kuwa huenda hujatishiwa maisha yako hivi karibuni.
Lakini kwa tafsiri, adui ni mpinzani, mshindani, mtoa changamoto, mgombea. Adui ni yule anayekuchukia, au anyekutendea vibaya. Anaweza awe hata ni mwenzi wako, au mwanafamilia mwingine. Zinaweza kuwapo nyakati ambapo mwana-familia haonyeshi sana upendo. Hata anaweza kutafuta njia za kukusumbua au kukufanyia vibaya Zaidi. Hilo linapotokea, inakuwa rahisi kuingia kwenye mtego wa kulipiza kisasi na chuki ndogondogo.
Wakati mwingine waweza kupata mgogoro kazini, na wale ambao umekuwa ukifanya nao kazi bega kwa bega kwa miaka mingi wakaanza kukuhisi kama mpinzani. Adui aweza kuwa mtu ambaye umemjali sana maishani au anaweza kuwa mtu Fulani kanisani kwako.
Tunapaswa kutambua kuwa adui ambaye Yesu anamwelezea hapa sio tu yule anayetishia maisha yetu bali ni mtu yeyote anayetusababishia fadhaa au hofu kuu kiasi cha kututia majaribuni kutaka kulipiza kisasi.
Kuwapenda adui zetu? Watu kwa jumla wanapata wakati mgumu kuonyesha upendo kwa marafiki zao, sembuse maadui zao. Tunawezaje kujifunza kufuata kielelezo cha Yesu hapa? Ni kwa vipi mioyo yetu inaweza kubadilishwa ili tupate kuwapenda adui zetu? Ni kwa vipi kuwaombea adui zetu huchangia katika kufikia lengo lililo bora la maadili ya Kikristo?
 
Upendo Katika Vitendo (Lk 10:25-37)
Profesa wa seminari alilipanga darasa lake la mahubiri katika namna isiyo ya kawaida. Alimpanga kila mwanafunzi wake kuandaa hotuba kuhusu msamaria mwema. Mmoja baada ya mwingine walitakiwa kwenda darasa moja hadi jingine wakihubiri upendo na huruma kwa wengine. Kulikuwa na pumziko fupi tu kati ya kipindi kimoja na kingine, jambo lililowafanya wahubiri hawa watarajiwa wawe katika hali ya kuharakisha ili kutimiza ratiba yao. Kila mwanafunzi mhubiri alilazimika kupitia katika ukumbi na kumpita omba-omba Fulani ambaye kwa makusudi alikuwa amewekwa pale na yule profesa.
Kilichotokea ni fundisho lenye nguvu sana. Idadi ya wahubiri watarajiwa waliosimama na kutoa msaada kwa mhitaji huyu walikuwa wachache ajabu, hasa wale waliokuwa chini ya shinikizo la muda. Wakiharakisha ili kutoa hotuba juu ya Msamaria mwema, karibia wote walimpita tu yule omba-omba ambaye ndiye alikuwa kiini cha mfano huo!
Swali la kujiuliza ni, jirani yang uni nani? Ni kwa jinsi gani Yesu, katika Luka 10:25-37, hujibu swali hilo kwa ajili yetu? Ni kwa vipi mfano huu unahusiana na kile ulicho upendo wa kweli? Pia, kadiri unavyosoma mfano huo, kwa nini Yesu kwa namna ya pekee alitumia watu wa kidini, na hata viongozi wa kidini, na hata viongozi wa kidini kuwakilisha "watu wasiofaa"? Ni somo gani linapatikana hapa kwa ajili yetu pia?
Tafakari maneno haya: "Nilikuwa na njaa, ninyi mkaunda tume ya utu ili kujadili jambo hilo. Nilikuwa gerezani, ninyi mkawa mnalalamikia kuongezeka kwa uhalifu. Nalikuwa uchi, nanyi mkawa mnajadili uadilifu wa mwonekano wangu. Nilikuwa mgonjwa, ninyi mkawa mnashukuru Mungu kwa ajili ya afya zenu. Sikuwa na makazi, nanyi mkanihubiri kuhusu ulinzi wa upendo wa Mungu. Mnaonekana kuwa watakatifu mno na kuwa karibu Zaidi na Mungu; lakini mimi bado ni mwenye njaa, mpweke, mwenye kupigwa na baridi, na mwenye maumivu. Je, mnajali?"
Uwe mkweli. Ni aina gani ya mabadiliko ya mtindo wa maisha wapaswa kufanya ili uwe Msamaria mwema kwa wengine? Ni nani unayemfahamu hivi sasa ambaye kwa wakati huu yuko upande wa pili wa barabara katika ulimwengu wa maumivu? Je, itakugharimu kufia nafsi kiasi gani ili kumtendea mtu huyu kama "jirani yako"?
 
Mkuu tujiandae kujibu swali hili ambalo wengi walio neutral na mambo ya dini huuliza,kama Mungu ni upendo,kwa nini ameruhusu dhambi na mateso kuwepo?this is the most challenging question ambalo ni lazima ukutane nalo ukiwaambia watu wa leo waliojeruhiwa na maisha kwamba Mungu anawapenda sana.tujibu hili swali tukiendelea na mnakasha huu.
free will ya mwanadamu ndio iliyoamua dhambi na mateso
 
Back
Top Bottom