Waziri Mwandosya ambaye hotuba yake ilikuwa ikikatizwa kwa makofi ya wabunge, aliongeza kuwa moja na la msingi ambalo amejifunza ni kwamba sasa amejua kwamba Wizara ya Afya ni mhimu sana.
Afya ni mhimu sana, hasa baada ya kuugua
sijui kilimo ndiyo namba moja au elimu, lakini ukiugua kilimo wala elimu huwezi, hata hapa bungeni huwezi kuomba mwongozo wa Spika, kwa hiyo afya kwanza, alisema.
Aliwashauri wabunge kuendelea kupima afya zao, akisema kuwa kwa miaka 45 alikuwa hajawahi kulazwa hospitalini, lakini amekiona kitanda huko Hadrabad nchini India alipokwenda kutibiwa, maana awali alijiona ni mtu mwenye afya na mazoezi sana.
Sasa naomba pia tuangalie afya zetu hata baada ya kustaafu, maana tunajisikia tuko wazima tunapozungumza sana, lakini baada ya kumaliza je, tumeingia mkondo gani wa afya? Katika taratibu za afya nchini ni jambo la muhimu, alihitimisha Waziri Mwandosya.
Baada ya kuhitimisha,