Karibu Tarime mama Kilango 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Karibu Tarime mama Kilango 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsayaMwita, Nov 26, 2009.

 1. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu wana Jf nachukua fursa kumkaribisha mama yetu hapa Tarime kwani nimeona anaweza kufanya kila kinachowezekana kulitwaa jimbo hili mikononi mwa CHADEMA.

  Nimeamua kulisema hili kwani kwa kile mama kilango alichokisema kuwa 2010 atakuwa pale Moshi sasa basi sijasikia mwanasiasa yoyote toka CCM akijiandaa kuja kulitetea jimbo letu la Tarime!

  Maswali tunayoweza kujiuliza hapa je wanaogopa tafrani huko Tarime?

  Wasiwasi wangu je hii demokrasia inayotumika ina mshiko?

  Angalizo mama Anna asisahau kuwa hawa wapinzani wana mchango mkubwa pale Bungeni?

  Mama anna asisahau kuwa hao anaotaka wasirudi kule bungeni ndiyo nguvu yake.
   
 2. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Huo ndio ukweli. Maana hata hayo anayoongelea bungeni na yakampandisha chati yameletwa humo na wabunge wa upinzani na wao "wapambanaji ndani ya CCM" wakadandia kwa kasi ya ajabu.
   
 3. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Chakaza,
  Ni kweli lakini kuna kila sababu kulijua hili je ni haki mama Ana ana mtizamo uliyo hai? ama ni mgema akisifiwa t............!!!!
   
 4. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Huyu mama anachofanya ni kupima kina cha maji. Amepima maji ya moshi akaona anauwezo wa kusema aliyo sema, japo naona hya maji yatamchukua kwani ailipima pembeni ni si kwenye kina kirufu, sasa amejitupa ndani ya maji, tusubiri matokeo.

  Kwa upande wa tarime, hasije kabisa akathubutu, atarudi same kwa miguu bila kandambili. Tarime si moshi ambako anauhusiano wa damu. kule ni mikuki,pinde manati atavstahimili?
   
 5. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama mama anaogopa mikuki, wasiwasi wangu ni kuwa mbona anataka kutokomeza demokrasi hii inayoanza kuchipuka hapa Tanzania?
   
 6. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  anatafuta nishani ya CCM
   
 7. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ulimbo

  Sidhani kama utakuwa sahihi ukisema hivyo, ila hoja ya msingi ya kutaka kuwang'oa wapinzani ina mshiko(maslahi) kwa watanzania?
   
 8. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ametonywa kuwa Slaa akiwa raisi atashghurikia mafisadi wote halafu mama Simba kamkumbusha kuwa na yeye ni fisadi. Alichokosea mama simba ni kuwa ametumegea kidogo tu kati ya yale wanayoyajua ya huyu mama.

  Mimi nakwambia huyu mama atatumika sana mwaka huu atakoma kuwanyoshea vidole wenzake kabla ya kutubu ya kwake
   
 9. O

  Orche Senior Member

  #9
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu mama anatafuta sifa tu. Hakuna kingine hakuna mabadiliko yoyote aliyoleta ndani ya CCM, wala kwa wapiga kura wake ila anataka Mrisho amwone mwakani ubunge wa kuteuliwa akishindwa. Kumbukeni ana kadi ya njano, anaogopa almashauri kuu kupitishwa kugombea kwa hiyo anajipendekeza kwa chama chake.
   
 10. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Shalom;

  Shalom;hapa hoja si kutumika , mimi wasiwasi wangu ni kuwa je huyu mama ameweza kutambua kuwa haya yote anayoyasema amepata nguvu toka kwa wapinzani?
   
 11. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Orche; Mimi ningetamani kama mama Anna angekuwa mzalendo na si kusukumwa na hisia zake, ajaribu kupima nyakati na si udhanifu, anapofikia maha;li akawa anatishia wabunge wapinzani kuwa atawapora ubunge naona si sahihi, mimi nadhani yeye ana jimbo lake, na CCM si yeye tu, la Hasha yawezekana kavaa kofia ya uenyekiti wa chama kwa sasa.
   
 12. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hiyo si kweli ila hoja hapa ni kwamba je yuko tayari kuitetea Demokrasia hii ya Tanzania au ilikuwa ni kelele ili kuendeleza udikteta wa ccm? Tazama kama angekuwa Mzalendo wa kweli nadhani angekuwa tayari kuona Upinzani ukikua ila yeye anachokifanya wenye akili tunajua.

  Nadhani kuna kila sababu Mama anna aje hapa Tarime, ajifunze kuwa sisi watanzania tunataka nini.
  Namkumbuka sana MTIKILA Nadhani tangu ametoka Tarime na siasa zake chafu zimekwisha

  Simuombei mabaya ila aje tu 2010 apate kujifunza kutoka kwetu.

  Mungu ibariki Tanzania,

  Mungu kinusuru kizazi kijacho na haya wasiokuwa wazalendo
   
 13. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi huko tarime hakuna wabunge? wa CCM?
   
 14. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sura-ya-Kwanza;
  Tarime kama jimbo kwa sasa hawapo, ila naamini ukija hapa wewe utakuwa mbunge wetu karibu ndugu.
   
 15. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sura-ya-Kwanza;
  Tarime kama jimbo kwa sasa hawapo, ila naamini ukija hapa wewe utakuwa mbunge wetu karibu ndugu.
   
 16. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  I.mwita,
  Hawapo CCM? Jimboni?
  nani wapo na wana ajenda gani?
  nipo kinondoni dar!
   
 17. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2009
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sura-ya-Kwanza
  Na ndiyo maana nimekuambia ukija hapa jimboni kwa kupitia tiketi ya ccm uatakuwa Mbunge wetu, karibu Sura-ya-Kwanza
   
 18. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  :D
  Sitaki tiketi!
  Nipeni kura-na siyo ya CCM!
  :D:D
  I am not a politician! Siasa, haswa siasa, siasa-siyo kigezo cha maendeleo Tarime!

  Nitaweza kuwasaidia watu hapa Tarime pale watu wa Tarime watakapo kubali kuwa uzalendo ni wa "Watanzania" na Ujamaa mamboleo upo! sina kanga, sina soda!

  naelewa uozo uliopo!
   
 19. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ninavyoona mimi Moshi katumwa na Mengi, Nani atamfadhili Tarime?
   
 20. W

  Wasegesege Senior Member

  #20
  Nov 28, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabla hamjamzungumzia Mama Anna wa Kilango wa Malecela tafuteni kwanza HISTORIA yake tangu alipokuwa Shule ya Sekondari ndipo mtamjua ni MSANII WA KIWANGO GANI? Huyu Mama hana lolote ni mbabaishaji wa hali ya juu.

  Halafu kuna Gezati moja la kila siku MWANANCHI lilinikasilisha sana. Wakati maafa yametokea kule Same, sasa badala ya kumuuliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Wilaya ya Same, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same ambao walikuwa kwenye tukio eti wanamuuliza Mana Kilango wa Malecela ambaye alikuwa Musoma ili aweze kuzungumzia hali ikoje kwenye tukio la watu kufunikwa na udongo. Huu ni ubabaishaji wa HALI YA JUU WA MAMA KILANGO WA kutumia magazeti ili aonekane kwamba anauchungu na wananchi.
   
Loading...