Karibu hakika jonathan bookshop

Karibu hakika jonathan bookshop

Mwalimu Truth

Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
57
Reaction score
79
KITABU CHA "DAMU NA MACHOZI"
:
:BEI SH 10000
:
"Mshindi wa tatu ni Patreporo Clekozik kutoka Slovenia, mshindi wa pili ni Linda Windsay kutoka Marekani na mshindi wa kwanza niiiiiiiiii! "Alipofika hapo mcBing alivuta kidogo na watu roho zao zikabaki juujuu, kwasababu nyuma ya pazia walikuwa wamebaki wasichana watatu.

"MISS TANZANIAAAAA! "Alisema mcBing na ukumbi wote ukapiga kelele kushangilia kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo, mrembo kutoka Afrika alikuwa amelivaa taji la mrembo wa Dunia!

Kila mtu alionekana kuyategemea matokeo hayo, Isabella aliangua kilio cha furaha. Alipita jukwaani akienda nje huku akilia na kusema maneno "Thank you Wilbert, thank you Wilbert "watu wote hawakuelewa ni kwanini alisema maneno hayo.

Wlibert alikuwa mbele ya jukwaa akirukaruka kwa furaha, hata yeye machozi yalimtoka! Alijiskia yu kama Sheikh Yahaya kwa kutabiri kitu na kikatokea. Hakuamini kama tayari alikuwa mume wa Miss World!

"The respect of this crown, goes to my parents back home in Tanzania, who are watching me right now on television and my husband to be Wilbert, who is here with me. I love you Wilbert! (Heshima ya taji hili inakwenda kwa wazazi wangu nyumbani Tanzania, ambao wananiangalia kwenye runinga hivi sasa pamoja na mume wangu mtarajiwa, Wilbert, ambaye yuko pamoja nami hapa, nakupenda Wilbert!) Isabella aliongea kwa kiingereza kitu kilichowashangaza watu wengi ukumbini na kuwafanya washindwe kuelewa ni kwanini alihitaji mkalimani.

Baada ya onesho hilo waliingia katika magari tayali kurudi kwenye hoteli walizofikia. Isabella alipanda gari moja na Miss Slovenia na Wilbert alipanda gari jingine na kuanza kulifuatilia gari lao kwa nyuma ,hakuruhusiwa kupanda katika gari la Miss Word pamoja na kuwa alikuwa ni mchumba wake.

"Fuatilia hilo gari upesi ".Dereva alimwambia dereva wa teksi aliyopanda kwa lugha ya kiingereza.

"Lipi? "
"Lile benzi jeusi ".
"Sawa bosi ".

Walikuwa wamekwenda kama kilometa moja hivi kutoka ukumbini, Wilbert alipolishuhudia gari kubwa aina ya Ford likitokea ubavuni mwa gari la akina Isabella na kuwagonga vibaya! Wilbert alishika kichwa chake na kupiga kelele, kabla hajafanya kitu chochote alimshuhudia Isabella akirushwa kupitia kioo cha mbele cha gari hilo na kuanguka pembeni kama hatua kumi hivi kutoka kwenye gari hilo alilokuwemo. Damu nyingi zilimtoka puani na mdomoni.

Kama vile chui Wilbert aliruka kupitia dirishani na kukimbia moja kwa moja hadi mahali alipoangukia Isabella, taji la mrembo wa dunia likiwa pembeni mwake. Neno pekee alilosema kabla ya kunyamanza ni "I love you Wilbert, be faithful to me forever! "(Nakupenda Wilbert uwe mwaminifu kwangu milele) Wilbert alilia machozi akiomba tukio hilo liwe ndoto, lakini lilikuwa kweli.

"Isabella! Isabella! Isabella! please don't die! Remember the promice you gave me! you promised me to be married with you, please don't die i love u so much Isabella! "(Isabella! Isabella! Isabella! tafadhali usife! Kumbuka ahadi uliyonipa, uliniahidi nitakuoa! Tafadhali usife! nakupenda mno Isabella!) Alisema Wilbert huku akilia.
:
JIPATIE KITABU HIKI KISICHO CHOSHA KUSOMA "DAMU NA MACHOZI " KWA SH 10000.KAMA UKO MOROGORO MJINI, HAKIKA JONATHAN BOOKSHOP TUNAKULETA MPAKA MLANGONI, MIKOANI TUNAKUTUMIA. KARIBU SANA HAKIKA JONATHAN BOOKSHOP!
IMG_20190609_154948_205.jpeg
 
Skuiz ni mwendo wa soft copy janjarooo, hardcopy ishapitwa na wkt so shusha mzigo wa soft copy
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom