Sitasahau siku tulipo ibiwa nyumbani nikiwa na babu yangu chumbani mimi nikiwa kadogo nazani ni mwaka 1993.Hii ya madawa kupuliziwa ilikuwa haijawa insu sana kwa miaka ile ila ndo ilitutokea.
Kutokana na mazingira ya kijijini, mzee wetu alikuwa ana nyumba zaidi ya moja hapo nyumbani na sisi kama wajukuu tulikuwa tukilala na babu mimi pamoja na kaka yangu.Asubui baada ya kuamka ndo tukagundua kuwa tumeibiwa. Babu alikuwa na bunduki moja ambayo alikuwa ameiegemeshea ukutani karibu na kitanda,magunia kama manne ya mpungu na mahindi,wakachukua na vitu vingine vidogo dogo, tuliamka saa mbili asubui tena kwa kuamshwa maana haikuwa kawaida ya mzee kulala usingizi wa namna hiyo, kawaida yake yeye alikuwa mtu wa kukaa macho sana wakati wa usiku kutokana na hali ya kuwa na mifugo hapo nyumbani.
Babu alishangaa, alisema mara moja tu alipo amka" tumeibiwa" kuangaria bunduki haipo kutoka nje mlango umevunjwa sijui na mashine gani hiyo. Polisi wakaja wakamchukua babu hadi kituoni baada ya kuangalia mazingira ya huo uporaji.Walienda kumuweka hapo kituoni lakini mkuu wa kituo sijui na nani wakasema haiwezekani mzee kufunguriwa mashitaka kwa kosa la upotezefu wa siraha, mana wengine walijaji ya kwamba huenda ameamua kuiuza kwa majambazi kwa kuwa amezeeka,ila huyo jamaa alikataa akasema huyu mzee kamiliki silaha tangu serikali ya mkoloni na ameshirikiana na sisi aiku nyingi kwa mambo ya kiusalama haiwezekani kumhisia vibaya katika tukio hilo, ikabidi wamuachie, wakamrudisha home mida ya saa nne usiku. Hiyo bunduki ilikuja kukamatwa na polisi katika tukio moja la kijambazi ikiwa imekatwa ule mtutu na kuwa fupi, yani ikipigwa risasi mita mia tatu utazani imepigiwa mgongoni mwako.
Sifa ya mzee ilikuwa ni shabaya, alikuwa mlengaji, sniper, hakuna wa kuweza kumfuata kwa uwezo wake na hivyo alikuwa akitumika a serikali kwa mambo ya kupiga wanyama waliotoka hifadhini na kuanza kuleta madhara kwa raia, mana mnyama mkari ilitakiwa umpige kichwa na ukikosea ukapiga hewa hapo kitimu timu lazima kiwepo mana na yeye anaanza kujihami, walio kaa kalibu na mapori wanajua, utasikia anasema nina hasira kama nyati aliyekoswa na risasi. Sasa huyo mzee alikuwa nauwezo wa kupiga kichwa cha mnyama hata kama anakimbia.
Mara ya mwisho alimpiga mwewe aliyekuwa anachukua vifaranga vya kuku alikuwa ametuakwenye mti pembeni na nyumbani,alipigwa kichwa kikasambaa kwa risasi, yani ilibaki shingo tu kichwa hakipo,wakamchokonoa kwa selele yale ma miti malefu yanayoota katikati ya katani ndo akaanguka mana alikuwa amenasa miguu yake ivo ivo kama alivyokuwa hai kule mtini. R.i.p babu yetu.