Karibia mtaa mzima Sinza A tumeibiwa

Karibia mtaa mzima Sinza A tumeibiwa

Chikwangara

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
685
Reaction score
940
Leo imekuwa ni vilio na hamaki kwa raia wa hapa Sinza A, baada ya kuamka asubuhi na kukuta madirisha yao yametobolewa na kukatwa kwa nyavu.

Inasemekana, walipuliza dawa ya usingizi ndipo wakafanya unyama huo. Watu wameibiwa pesa, laptops, simu, vitu vya ndani kibao.

Hapo unapoishi, kuna wizi wowote umefanyika?

Anayejua jinsi ya kujikinga na hiyo sawa, atupe elimu hapa.

Poleni wahanga wote wa wizi huo.

Nawasilisha!
 
Unajua bana kuna sehemu hapa dar inabidi ukiishi ukubali consequences.
Kwa mfano sinza au kino,ukiishi make sure una security sio unategemea miujiza kila siku uamke asubuh upate vitu vyako viko salama, Kwanza hamna doria yyte usiku,hamna cctv na nyumba zingine hazina fence/ electric fence, madirisha yanayoweza kutoboleka nayo ni hatari, hakuna hata mbwa kutokana na kuwa nyumba ni za kupanga. Sasa hapo its obvious kuwa wezi wakija lazima wawalize tena wanakuja wanne,wawili wanashirikiana kuiba wawili wanakaa mwanzo na mwisho wa hyo barabara.
Nanyie inabd mtumie mbinu ya ziada muanze kuwakamata.
 
Wanapokuja wezi kuwapulizia dawa ya usingizi kusudi mlale fofo na wizi ufanyike, fanyeni hivi kabla hamjalala!
Tia maji kwenye beseni lililo wazi kisha liweke chumbani kwako sehemu ya wazi, endapo wakija wakipulizia dawa tu, Yale maji yaliyopo kwenye ilo beseni basi litanyonya sumu yote iliyopulizwa humo ndani na kukuacha salama.
Na kwa njia iyo utaweza stuka mapema.
 
JF kuna waliokosa busara wengi kweli, mada serious watu wanachangia ujinga hadi kero. Dawa ya kudhibiti wezi kama hao ni kuweka zile chuma za dirishani zikiwa zimebanana tu ili asiweze kupitisha simu.

Madirisha mengi yana magrill yenye nafasi kubwa sana na mengine hayana kabisa. Inabidi kubadili staili ya ujengaji wa nyumba kukabiliana na hatari hii,
 
Bunju nako noma sana.. wanaingia ndani na kupora kila kitu
 
Leo imekuwa ni vilio na hamaki kwa raia wa hapa Sinza A, baada ya kuamka asubuhi na kukuta madirisha yao yametobolewa na kukatwa kwa nyavu.

Inasemekana, walipuliza dawa ya usingizi ndipo wakafanya unyama huo. Watu wameibiwa pesa, laptops, simu, vitu vya ndani kibao.

Hapo unapoishi, kuna wizi wowote umefanyika?

Anayejua jinsi ya kujikinga na hiyo sawa, atupe elimu hapa.

Poleni wahanga wote wa wizi huo.

Nawasilisha!
Wajanja mnaibiwaje kijinga hivyo? Sinza kw wajanja eeh.
Poleni.
Huku kwetu tukimjua mwizi, tunamkaushia mpaka weekend siku tunajua kila mtu yuko nyumbani. Tunaenda kamata chukua mpaka kwenye open space kisha tairi linamuhusu. Kila mtu aone.
Tun zero tolerance.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom