Kariakoo imehamia Stendi ya Magufuli, Mbezi Louis

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,123
7,709
Kwa mara ya kwanza leo hii nimefika stendi mpya ya Magufuli, hakika inastahili kubeba heshima ya Jemedari wetu Dr. JPM, nimeshuka tu nilidhani nimefika South Africa! ni nzuri sana na kubwa, ya kisasa!

Movements niliyoiona ni kama vile Kariakoo yote imehamia Mbezi!

Stendi hii imebadilisha kila kitu hapa, abiria ni wengi sana!

Hakika baada ya mwaka mmoja kutakuwa na uwekezaji mkubwa sana maeneo ya Mbezi na viunga vyake.

Nadhani ni muda kwa wafanyabiashara wenzangu kuwekeza ktk maeneo haya maaa a abiria wengi haswa wafanyabiashara wanatarajia kupata mahaitaji/bidhaa zote hapa hapa badala ya kwenda K/Koo.

"K/Koo imehamia Mbezi mwisho na viunga vyake".

Fursa ya kufanya biashara kwa sasa iko mbezi.

Tuwekeze Mbezi Mwisho.
 
Mapungufu au changamoto ndogondogo zilizopo ktk kituo hicho ambazo pia zinafanyiwa kazi haziondoi sifa kuwa kituo hicho ni cha kimataifa.

Hakuna ubishi kuwa K.koo inahamia Maeneo haya. wageni wnamiminika hapa usiku na mchana wengi wao ni wafanyabiashara.
tuchangamkie fursa ya uwekezaji. Muda ndio huu, ndio kwanzaa kituo kimeanza kazi.

Nilibahatika kuonana na wafanyabiashara kutoka;

Malawi, Zimbabwe, Zambia, Kenya, Uganda na Burundi wengi wanapongeza sana serikali ya Tanzania kwa ujenzi wa stendi hiyo mpya ya kisasa, wengi wao wanatamani kila kitu kipatikane hapahapa mbezi kuliko kwenda k.koo.

Jamani changamkieni fursa acheni kukaa na kulaumu tu mambo mengine yatajiseti tu yenyewe, jambo la msingi ni kutengeneza pesa, kwa sasa tuvumilie changamoto ndogondogo.
 
Back
Top Bottom