Kariakoo bila ya visima vya maji sijui ingekuaje

O-man

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
323
65
Kwa wakazi wa Kariakoo adha ya maji kwa siku ya tano leo imekuwa kero isiyo mfano. Ingekuwa hakuna visima vya maji (vingi maji yake yana chumvi mno), kungezuka balaa. Magorofa yaliyobanana, wingi wa watu - nahisi hata soko la Kariakoo lingefungwa.
Hata maji yanapopatikana Kariakoo bado ni chafu. Vyoo vya Kizungu haviingiliki. Hivi mamlaka husika haina aina yoyote ya supply kwa dharura? Tunawashukuru wenye visima wachache ambao wanaruhusu watu kuchota maji bila malipo (kama umeme upo).
 
Hebu tujulishe , hivyo visima ni vile vifupi?( mita 6 au 7) au ni vile virefu( mita 40 na kwenda chini zaidi).
Kama ni vifupi basi tutegemee kipindu pindu katika mud a mfupi ujao katokana na ukweli kuwa vinachukua uchafu wa vinyesi katika vyoo vilivyo sehemu nyingi Kariakoo.
 
Back
Top Bottom