Karia ameihangaikia Simba tu kwa kipindi chake chote

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,339
2,000
Hatujui ni kwasababu gani Karia anajivunia mafanikio ya soka yaliyopatikana wakati wa kipindi cha cha miaka 4. Binafsi sioni mafanikio ya soka kwenye kipindi chake zaidi ya Karia kuhakikisha kuwa Simba inakuwa bingwa kwa kipindi chake chote na inafanya vizuri kwenye mashindano ya African Champions Cup. How?

Baada ya Karia kuingia madarakani TFF,

1. Simba ilirahisishiwa kuingia kwenye mfumo mpya wa uendeshaji wa club bila kufuata njia zote zinazotakiwa bila kupewa adhabu yoyote.

2. Baada ya Simba kuonekana kuwa ina pesa za kusajili kuliko vilabu vingingine kwenye ligi, Simba ilirahisishiwa kusajili wachezaji 10 wa kigeni.

3. Simba ilirahisishiwa kumpata mchezaji yeyote waliyemtaka akiwemo Morrison bila kufuata kanuni.

4. Simba ilipangiwa ratiba kwenye ligi ambayo ni rafiki sana, yaani iliruhusiwa kuwa na viporo hadi 9 kwenye ligi.

5. Simba haikuathiliwa na maamuzi ya waamuzi viwanjani.

6. Alihakikisha kuwa Simba haina malalamiko yoyote kwa TFF

Hali hii ilisababisha Simba iwe comfortable kwenye mashindano yote iliyoshiriki wakati wote wa Bw Karia. Simba ilikuwa comfortable hata pale muda wa mechi yake Na Yanga ulipobabadilishwa ghafla bila kutolewa sababu za maana.

Siwezi kusema wakati wa kipindi chake nchi ilipiga hatua kwenye mpira, lahasha, sema tu alipata bahati akakuta viongozi wengi wa serikali ni wanachama au shabiki wa Simba.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,295
2,000
Ni wakati sasa kwa vilabu vya michezo kutengeneza kanuni za kuviwezesha kuongozwa na wanamichezo wenyewe!

Badala ya wanasiasa, makada na mamluki, kwa mgongo wa elimu ya chuo kikuu.
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,339
2,000
Yanga imecheza mechi nne mfululizo ikiwa uwanja wa nyumbani,vipi hili tuiteje mkurungwa ?
Kumbuka Simba ilianza ligi Na timu laini makusudi iwe kama njia ya kuifanya simba iwe kwake kama pre season baada ya mapunziko ya corona
 

Kobello

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
7,596
2,000
Taifa Stars kushiriki AFCON baada ya miaka 30 kupita.
Nusu ya nchi zote za Africa zilishiriki. Na bado tumeshindwa baada ya hapo.
Kabla ya hapo Tanzania ilishiriki ikiwa ni miongoni mwa nchi nane tu zinazotakiwa kushiriki.
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,339
2,000
Kwa hili nadhani tuwashukuru Waganda...walitubeba kama Ndugu zao na majirani
Na ndio maana kule kwenye mashindano hatukufua dafu, kwani TFF iliongeza kitu gani kipya kwa taifa stars hadi ipate nafasi afcon?
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
15,033
2,000
1. Simba ilirahisishiwa kuingia kwenye mfumo mpya wa uendeshaji wa club bila kufuata njia zote zinazotakiwa bila kupewa adhabu yoyote.

2. Baada ya Simba kuonekana kuwa ina pesa za kusajili kuliko vilabu vingingine kwenye ligi, Simba ilirahisishiwa kusajili wachezaji 10 wa kigeni.
Hizi ni sifa nzuri maana ni za kutaka maendeleo, na hakuna klabu iliyozuiwa kufanya mabadiliko ya uendeshaji au kusajili wachezaji 10 wa kigeni. Kwa hiyo Karia anastahili pongezi, minne tena!
 

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
7,339
2,000
Hizi ni sifa nzuri maana ni za kutaka maendeleo, na hakuna klabu iliyozuiwa kufanya mabadiliko ya uendeshaji au kusajili wachezaji 10 wa kigeni. Kwa hiyo Karia anastahili pongezi, minne tena!
Wachezaji 10 wa kigeni Karia aliilenga Simba tu ambayo kwa wakati ule ndo iliyokuwa Na uwezo wa kifedha wa mo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom