Kapteni Tesha na vita ya Majimaji

Kapteni Tesha na vita ya Majimaji

Mimi nilikuwa DSM na usiku wa tareh 30 nilipokea simu kuwa mwisho kutembea Saatano Asubuhi na ndo niliamini hii ilikuwa zaidi ya majimaji war

Vijana wa Tanzania bado wajinga kiukweli

Tesha aliletwa kimkakati na wajanja ili kutengeneza imani ya Maji maji war.
Sasa hivi wanalaumiana wenyewe kwa wenyewe kwanini mikoa mingine hawakujitokeza kwenye vurugu zile. Wanadhani ndiyo maana mpango ulizimwa kirahisi kabisa. Maandamano yanayofanikisha mambo ni yale yanayohusisha umati/halaiki ya watu nchi nzima. Haya yalifeli kwakuwa watanzania sio wapumbavu kama wakenya, walijitokeza watu wachache sana kiasi kwamba huwezi kuwaita nguvu ya umma.

Tatizo moja chadema wanadhani kuwa wanao umati wa watu ambao uko tayari kufanya lolote kama wakiambiwa kufanya chochote. Chadema ya Lissu ina underestimate nguvu ya Mbowe ndani ya chama.

Mimi sijui na sina data, lakini nadhani walioandamana wengi ni wafuasi wa Gwajiboy, watu wa kabila lilee, waliohamasishwa na watru wa kabila lilee na mercenaries kutoka nchi jirani kwa malipo. Tuisubiri tume.
 
Ukweli ni kwamba jeshi la Tanzania lipo nyuma ya utekaji,mauaji, uchaguzi feki,ukosefu wa maji Dar es Salaam ,darasa moja kuwa na wanafunzi 100+,umeme wa kusuasua,ufisadi na kumpiga Tundu Lissu risasi!
kama ni hivyo basi Afrika yote ndio iko hivyo. Hizo shida zipo nchi zote barani Afrika, kwanini unaona Tanzania haipaswi kuwa na shida kama hizo?. Ni nchi gani Afrika imesambaza umeme kwenye vijiji vyoooote, ina reli ya umeme, inatumia mabasi ya kwendo wa haraka, ina mtandao mkubwa wa barabara za lami, shule na zahanati?

Ukweli mnawapotosha vijana. Tatizo la Afrika ni ukosefu wa uwezo wa kuzivuna rasilimali zetu bila kuwahusisha wageni, ukosefu wa uwezo wa kuziongezea thamani rasilimali zetu na ukosefu wa masoko huru na haki ya kuuza rasilimali zetu, kaka tunapunjwa na mabeberu kwakuwa wao ndio wanaotupangia bei ya kuuza na kununua.
 
Ukweli ni kwamba jeshi la Tanzania lipo nyuma ya utekaji,mauaji, uchaguzi feki,ukosefu wa maji Dar es Salaam ,darasa moja kuwa na wanafunzi 100+,umeme wa kusuasua,ufisadi na kumpiga Tundu Lissu risasi!
Ukweli ni kwamba Tz haifanani na Congo, Sudani, Somalia, Ethiopia, Kenya, Burundi kwa utulivu kwasabu ya kazi ya majeshi yetu. Kazi ya kulinda nchi, watu na mali zao inaweza kuhusisha kung'oa magugu na visiki kwa kadiri watakavyoona inafaa. Hakuna taifa hata moja ambalo halina vibaraka, watu walionunuliwa. Ndiyo maana ya ule msemo wa mjenga nchi ni mwananchi na mvunja nchi ni mwananchi. Miongozi mwetu wako watu ambao kwa maslahi ya wengi lazima wao wakae pembeni kwa gharama yoyote ile.

Mfano, wale "waandamaji" kama wasingesimamishwa kwa njia ile wangeenda kuharibu wapi na wapi mpaka wapi? Je, unadhani kuwa wasingefika hadi kwenye kambi za majeshi? wasingefika kwa mkuu wa majeshi? wasingefika Ikulu? na huko kote wangefanya nini kama wangefika?. Vitu walivyoharibu hazikuwa kodi zetu sisi wote? Je, Samia anatumia usafiri wa SGR au mwendokasi? Je, kama vituo vyoote vya polisi vimeungua usalama wetu dhidi ya majambazi na wezi huko mitaani ungekuwaje? Je, Lake group hawalipi kodi TRA? watanzania wangapi wamepata ajira Lake group?

Ukweli nguvu iliyotumika ilikuwa sahihi kabisa.
 
Kufeli kwa mbinu moja ya vita haimanishi ilikuwa haramu
 
We unajua ni nani aliwakula vichwa waandamaji?
Nilikuwepo na nilishuhudia polisi wakilenga waandamananji na kile kikundi kisichokuwa na sare sijaona mwanajeshi akimpiga silaha mwananchi na tumepiga nao stori usiku wa tar 1
 
Wananchi walihamasishwa kipumbavu na wapumbavu kwa kumchonga mpumbavu waliyemwita Kapteni Tesha.

Kapteni Tesha na wenzake walijenga picha kuwa jeshi la JWTZ liko nyuma ya maandamano/mapinduzi ya Oktoba 29 hivyo kuwataka wajitokeze kwa wingi kwenye mapinduzi yale.

Hii haina tofauti na Kinjekitile Ngwale alipowahamasisha askari wake na wananchi kuwa wajitokeze kwa wingi kwenda kupigana na wajerumani kwakuwa risasi za adui zitageuka maji kabla hazijatua kwenye miili yao.

Ukweli ni kwamba risasi za wajerumani hazikugeuka maji hata kidogo.

Ukweli ni kwamba jeshi la JWTZ halikuwa nyuma ya wajinga wale na waandamaji wengi walikiona.

View: https://youtube.com/shorts/SOC50V3Ar1Q?si=Bo1TmY9Jh_XGX-uZ

Jambo ambalo naamini (binafsi) lipo na halisemwi ni hili. Vita ya majimaji sio kwamba mjerumani hakupata upinzani kutoka kwa wenyeji. Hata kama Kinjekitile alishindwa nahisi wajerumani walitumia plan B kumshinda. Hili laweza kuonekana kituko lakini tukumbuke historia yetu imeandikwa na watawala wetu (wazungu) na sijaona sehemu ambayo watanganyika walipewa ushindi isipokuwa sehemu zote wanaonekana kuwa mbuzi wa kafara na kondoo wa kuchinjwa. Yani kila vita walishindwa. Sikatai kwamba walishindwa na ndio maana tulitawaliwa, lakini sio kila sehemu wakoloni waliingia kirahisi.

Kama mbinu ya kinje ingekuwa ya hovyo, amini nawaambia ile vita ingepiganwa kwa masaa machache sana yasiyozidi mawili kwasababu vitani huwa kuna kitu kinaitwa morali. Endapo mambo yatakuwa kinyume na mipango yenu kivita na mkaelemewa mapema huwa ile hamu ya kuendelea kupigana inafifia na kuwafanya aidha mjisalimishe au mkimbie vita. Ukiangalia mwanzo hadi mwisho wa vita ni almost miaka miwili ambapo kuna mwaka mmoja katikati ulianza na kuisha wakati vita ikipiganwa (1906) siku zake zote 365 kulikuwa na vita.

Swali: ngome ya Kinjekitile ilikuwa na watu bilioni ngapi walioenda vitani hadi kufanya vita idumu kwa miaka miwili? Tukumbuke kwamba waandishi wa historia wanamuandika Kinje kama kiongozi asiye na uelewa juu ya masuala ya vita na sialaha za wajerumani. Hii ni kumaanisha kwamba kila siku vita ilipopiganwa, kulikuwa na vijana wasiojua nguvu ya risasi walikuwa wanaenda na morali ya kupigana na matokeo yake wanauawa kwa risasi ambazo hazikugeuka maji (kwa mujibu wa historia) kwasababu ni dhahiri huwezi kujificha kwenye uwanja wa vita kukwepa risasi ikiwa hauyajui madhara yake. Na hapandipo najiuliza wingi wa vijana walioshiriki ile vita hata kufanya vita ichukue muda mrefu namna hii.

Hoja yangu, huenda kweli ilifika wakati nguvu asilia ya zindiko la Kinjekitile kupungua ama kuisha kabisa lakini naamini haikuwa rahisi ama haikuwa hivihivi tu, kuna namna mjerumani alitafuta namna ya kumdhoofisha kwa kuwa ni dhahiri shayiri mapambano yalikuwa makali na ndio maana vita ilidumu kwa muda mrefu vile.

Jiulize zile hekaheka za october hazikuchukua hata wiki moja (october 29 hadi november 2) lakini cha moto tulikiona, mambo yangeendelea kwa mwezi mzima mfululizo ingekuwaje? Kwa kuzingatia mfano tajwa kwenye aya hii, jiulize swali hili kwamba: kama vijana wa kinje walitumia mikuki na mishale pekee huku mjerumani akiwa na risasi (bila nguvu ya yale maji) waliwezaje ku survive mikiki na hekaheka huku wakiendelea kushuhudia/kuletewa taarifa za mauaji ya askari wenzao waliokuwa wakienda vitani bila kujisalimisha?

Mimi naamini kama Kinjekitile asingekuwa na akili, vita ingedumu labda mwezi mmoja (siku 7 za kupigwa, na zingine za kutoroka uwanja wa vita) na baada ya hapo himaya yote ingejisalimisha na hata wanajeshi wa Kinjekitile wangemuasi kwa kuwa wanakufa hovyo.

Naomba kuwasilisha.
 
Sahihi - Ila siumsikia GEN Z wanataka kurudi tena !
 
Kapteni Tesha ni sauti ya waliowengi Jeshini, hapo kinachosubiriwa ni nafasi (opportunity), kikitokea tu kikundi kma cha M23, utaona wimbi la uasi litakavyo tokea na kuungana na hilo kundi, hapo bado wananchi hasa waliopoteza ndugu zao…
 
Nyie ndo maana mkaitwa Nyumbu uwezo mdogo wa kuelewa mambo
 
Back
Top Bottom