Kapteni Tesha na vita ya Majimaji

Kapteni Tesha na vita ya Majimaji

Kwa nini watoto wauliwe kipumbavu? Kwa nini muwauwe? Anayeua kwa nini awaue? Wewe ni mjinga kupindukia.
Mkuu wala usihangaike naye, Karma ipo, hizi kejeli za jamaa ni kama za kina Jenista enzi wakiwa bungeni, anawalaumu waliouwawa badala ya aliyewaua.

Juzi niliona watoto wa Jenista wakijiliza na kugalala na kulalamika, nikajisemea Vuneni matunda ya Mama yenu, mlidhani uchungu wa kufiwa ni kwa wengine tu
 
Kapteni Tesha ni sauti ya waliowengi Jeshini, hapo kinachosubiriwa ni nafasi (opportunity), kikitokea tu kikundi kma cha M23, utaona wimbi la uasi litakavyo tokea na kuungana na hilo kundi, hapo bado wananchi hasa waliopoteza ndugu zao…
Hilo kundi la M23 lilikuwepo kule Kibiti mbona Kapteni Tesha hakuungana nao? wanaJeshi wa JWTZ hawakuchaguliwa kujiunga na jeshi kiboyaboya kama unavyodhani. Usidhani wanajeshi wa JWTZ hawajui dunia inakwendaje.

Shida yetu pekee tuliyonayo sisi ni viongozi wezi kuachwa bila kupewa adhabu wanayostahili, wamejiwekea kinga, baaasi!!! Mengine haya ni kwaajili ya usalama na ustawi wa taifa.

Vyama vya upinzani Afrika havijafikia levels za kuongoza mataifa yao kwasababu zifuatazo:
1. Havina sera mbadala na vyama tawala
2. Vingi vinategemea nchi za Magharibi (waloni wetu) kuviingiza madarakani.
3. Wanatumia uongo na shida zilizopo Afrika kuwashawishi vijana wawaunge mkono.
4. Asilimia 80 ya shida za mataifa ya Afrika zimetokana na mfumo wa dunia unaotawaliwa na wazungu kama vile World Bank, IMF, Shirika la biashara la dunia (WTO), kura ya VETO.
5. Havina pia technolojia ya kuvuma rasilimali zetu wala masoko huru ya kuuza rasilimali zetu.

Ndiyo maana Afrika ni ileile hata kwa zile nchi ambazo vyama vya upinzani vimeshinda uchaguzi. Hata kule Libya, Iraq, DRC, Sudan, na Somalia wanachi wao sasa hivi wanazikumbuka serikali zao zilizoangushwa. Wanaona ni heri ya vile kuliko hivi, heri ya yule kuliko huyu.

Majeshi yetu yameshiriki peace keeping nyingi ndani na nje ya Afrika wanafahamu namna vyama vya upinzani vya kweli kwa taifa na vya uongo kwa taifa.
 
congratulation stupido! Guess what! You've been added on my ignored list!! So long sucker!
Ila watu wenye homa ya akili mnachekesha sana!! Sasa wewe kidampa tena anonymous unamtishia mtu kumuweka kwa ignore list? Halafu aathirike na nini? 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ukweli ni kwamba Tz haifanani na Congo, Sudani, Somalia, Ethiopia, Kenya, Burundi kwa utulivu kwasabu ya kazi ya majeshi yetu. Kazi ya kulinda nchi, watu na mali zao inaweza kuhusisha kung'oa magugu na visiki kwa kadiri watakavyoona inafaa. Hakuna taifa hata moja ambalo halina vibaraka, watu walionunuliwa. Ndiyo maana ya ule msemo wa mjenga nchi ni mwananchi na mvunja nchi ni mwananchi. Miongozi mwetu wako watu ambao kwa maslahi ya wengi lazima wao wakae pembeni kwa gharama yoyote ile.

Mfano, wale "waandamaji" kama wasingesimamishwa kwa njia ile wangeenda kuharibu wapi na wapi mpaka wapi? Je, unadhani kuwa wasingefika hadi kwenye kambi za majeshi? wasingefika kwa mkuu wa majeshi? wasingefika Ikulu? na huko kote wangefanya nini kama wangefika?. Vitu walivyoharibu hazikuwa kodi zetu sisi wote? Je, Samia anatumia usafiri wa SGR au mwendokasi? Je, kama vituo vyoote vya polisi vimeungua usalama wetu dhidi ya majambazi na wezi huko mitaani ungekuwaje? Je, Lake group hawalipi kodi TRA? watanzania wangapi wamepata ajira Lake group?

Ukweli nguvu iliyotumika ilikuwa sahihi kabisa.
Povu la nini?Mimi nimeandika yanayoungwa mkono na jeshi kabla ya MO29......
Hata wakati wa kuwatoa wakoloni watu walikufa.....
Huwezi kuwa na akili ya kawaida kukubali upuuzi unaoitwa uchaguzi, utekaji na mauaji...
Kwani hao waliotekwa na kuuwa hawakuwa wanalipa Kodi?
Majambazi yanayoiba rasilmali za nchi CCM inawaficha kwa mikataba mibovu....
 
Nilikuwepo na nilishuhudia polisi wakilenga waandamananji na kile kikundi kisichokuwa na sare sijaona mwanajeshi akimpiga silaha mwananchi na tumepiga nao stori usiku wa tar 1
Kama ulikuwepo na ulishuhudia Polisi na kile kikundi kikilenga na kuua waandamanaji, mbona wewe hujauawa? Wala hujajeruhiwa?
 
Wananchi walihamasishwa kipumbavu na wapumbavu kwa kumchonga mpumbavu waliyemwita Kapteni Tesha.

Kapteni Tesha na wenzake walijenga picha kuwa jeshi la JWTZ liko nyuma ya maandamano/mapinduzi ya Oktoba 29 hivyo kuwataka wajitokeze kwa wingi kwenye mapinduzi yale.

Hii haina tofauti na Kinjekitile Ngwale alipowahamasisha askari wake na wananchi kuwa wajitokeze kwa wingi kwenda kupigana na wajerumani kwakuwa risasi za adui zitageuka maji kabla hazijatua kwenye miili yao.

Ukweli ni kwamba risasi za wajerumani hazikugeuka maji hata kidogo.

Ukweli ni kwamba jeshi la JWTZ halikuwa nyuma ya wajinga wale na waandamaji wengi walikiona.


View: https://youtube.com/shorts/SOC50V3Ar1Q?si=Bo1TmY9Jh_XGX-uZ

Inasikitisha sana kwakweli,wametumia uongo mkubwa sana kuwajaza vijana hamasa na kuingia road

Matokeo yake tumepoteza wa watanzania wenzetu
 
Back
Top Bottom