Kapotelea wapi Daz Baba Wa Daz Nundaz?

mmash

JF-Expert Member
Nov 30, 2013
832
1,237
Kuna kipindi nilisikia sikia kuwa jamaa amezama kwenye madawa ya kulevya huko Moro hadi hajielewi lakini yeye mwenyewe alikuja kuhojiwa na Millard Ayo akakana kuwa hatumii kabisa madawa,....lakini ukimuangalia tu jinsi alivyo wala huwezi kubisha kuwa jamaa ni Mteja,...

Ombi langu Kwa watanzania hasa wale wenye mauwezo yao,....Kwa nini wasijitokeze kumsaidi Daz Baba Kwa kumpeleka sober house akapate Tina sahihi ya dawa za kulevya?

Pengine anaweza akarudi kwenye game na akawa msanii bora kama zamani,wapo baadhi ya watu na taasisi zilizowahi kuwasaidia baadhi ya wasanii kupata tiba ya dawa za kulevya lakini baadhi ya wasanii wamerudia tena dawa hizo hali inayofanya watu wakate tamaa ya kumsaidia msanii mwingine tena,lakini ombi langu wana JF,msaidieni huyu jamaa maana Kwa muda aloteseka akipona anaweza asirudie tena uteja.
 
Huyu jamaa alitokea kuwa msanii mzuri sana hasa kutokana na sauti yake nzuri.

Kwani yeye ni nani alimtuma kula ngada mkuu mpaka asaidiwe?kupanga ni kuamua hivyo aendelee zake tu kubembea tu kwa raha zake wala usimrushie stimu zake broo
 
Attachments

  • tapatalk_1483906572536.jpeg
    tapatalk_1483906572536.jpeg
    33.5 KB · Views: 151
Huwezi kumpeleka mtu rehab kwa kumlazimisha.

Akitaka msaada atasema au atajipeleka mwenyewe sober house sio kwa kumlazimishwa.
 
Kwani yeye ni nani alimtuma kula ngada mkuu mpaka asaidiwe?kupanga ni kuamua hivyo aendelee zake tu kubembea tu kwa raha zake wala usimrushie stimu zake broo
Daaah aisee hiv huyu ndo yule wa "wife" "nipe tano"??? "Daz baba nishakuwa mtu mzima mi nahitaji mrembo wa kuishi nami, kuzaa na kulea watoto nami, kwenye shida na raha avumilie namii." Hii ngoma yake cjawai ichoka .Mungu amsaidie
 
jamaa hali ngada sema ganja,pombe kali, imani kali za kirasta, matunzo zero na usela mwingi zinamfanya aonekane kama dishi limeyumba ila ni mtu wa kusafiri sana.. Nimekaa nae sana maskan na hata jana tulikua nae
acha kupotosha jukwaa JONASON .. Daz baba anatumia unga toka kitambo.. mwaka 2010 nlisoma advance na binamu yake, kuna likizo nli hang out nao sana tu.. kiufupi ilikua kama ukoo wao mzima wanatumia hii makitu, kuna kipindi kaka yake huyu mshkaji wangu alitoka UK na demu wake mzungu sijui ndo alileta 'mzigo wa mbele' maana daz alikua akiusifu sana akawa analalamika bongo wanauziwa vumbi..

kama ni mshkaji wako na unasema hatumii madawa then unatuongopea hapa jukwaani, i have seen him and his crew doing drugs na si mara moja mkuu.. labda useme ameacha which i'll highly doubt.
 
Nakumbuka jamaa kipindi kile yupo advanced level pale Makongo. Miaka ya 2003. Jamaa alikuwa na masela kibao sana. Alikuwa akifika mwenge wanakuja marafiki zake kibao, alikuwa na masela wengi sana ambao ni watukutu sana. Jamaa ata pale Makongo alikuwa kapinda, alikuwa anakula bangi sana
 
Hiyo picha ya mwisho balaa,the lost talent...so sad...nasikia Feruz naye kijugu?,amekuwa nyoka anabwia bwimbwi?
 
Yeye mwenyewe hajaamua kuacha apelekwe soba so ndio yale yale ya chidi na ray c
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom