Nimependa sana style hii ya uandishi
Aisee jamaa kaishuka nondo vizuri sana.
Watu wanalalamikia CCM miaka 50 waulize USA ni miaka mingapi wapo huru .Na ukienda kule hali ngum watu wanavyolia.
South Africa ndio mkuu kwa Africa leo hii hali kule ipoje,watu taabani,na wenye fursa ndio hao walioenda kuitumia kisha watu wanastuka kumekucha.Ndio hapa.Tusubiri umoja wa Africa Mashariki ukae sawa waje Wakenya na Waganda hapa wachukue kazi sie kulalamika tu.
Maisha ni jinsi unavyojituma mwenyewe.Kwa wale mlioenda ZAIRE(DRC),kule vyuo vikuu kibaoooo,kila mtaa kuna Gradutes zaidi ya mia.Sasa we unategemea nini.Wale wajanja wenye kujitambua wanajipanga na kisha wanatoka.
We unataka ajira na wale waliozaliwa kabla yako wasemeje.
Kwa wale mliofuatilia kipindi cha Uswazi jana,kuna jamaa walikuwa wamejiajiri wenyewe,walipoulizwa je mtu akikuajiri utakubali,jamaa wakasema sitaki kuajiriwa.
Mleta post hapo juu hajakosea hata moja,huo ndio mfumo tunaoendanao na kutaka maisha kuwa rahisi namna hiyo na nidham ya pesa kuwa mbovu kupita kiasi.Leo hii muuza Karanga mtaani ana niadham ya pesa kuliko Muajiriwa.
Fuatilieni Kipindi cha
Mboni Show Marejeao,kuna yule Dogo
DICK SOUND.
Ukisomea Historia yake unaweza kusema kama maisha ya kuigiza,tena yeye ni STD 7,ambao watu mnawadharau ni alilelewa na Single parent.lakini amefanya makubwa kwa kuwa alijitambua.
Leo kwa juhudi zake na kwa fursa serikali ilizomuwekea wazi.Leo hii ana miliki mijengo ya maana na Prado moja kali sana inakaribia 40m na nyingine ndogo almost usafiri wake tu si chini ya 70m kwa ujumla.Na Branches kadhaa za kazi zake na Pia anaeda China kuchukua bidhaa mwenyewe na Sasa hivi ameajiria watu tena wengi wamemzidi Elim.
Sasa yeye ni STD 7,aliejitambua,nyie wengine mnavamiwa vyuoni kwa kuwa wanaona wengie mliopo huko baadhi yenu mmeishajikatia tamaa wenyewe na ni rahisi kuwashawishi.
Maisha magum waliishi Mitume wetu tu,sie wengine ni kujipanga tu na dhambi zetu ndio zinatuhukumu.
Wewe kama unajiona maskini na maisha magum kwanza jitathmini wewe kama wewe mbele ya mungu wako.
Kisha jitambue,jitume na umuamini basi maisha yatakuwa ya kawaida sana.
Lakini ukasubiria nchi ya Asali na maziwa hapo ni ndoto na uzee huoooooooo.