Kapata Chuo Dodoma Asome Accounts Akiwa Amesoma PCB –Ushauri

Kapata Chuo Dodoma Asome Accounts Akiwa Amesoma PCB –Ushauri

Nijifunze nini sasa kuwa wazi! Unaandika kejeli tu sijaona ushauri wowte mpaka muda huu..
Comment ya kwanza niliongea yote, na zilizofata hivohvo labda kama unataka ukweli katika njia ya kubembelezwa lkn niliyosema ndo hayo hakuna utaloweza badilisha kuhusu mdog wako na ya kwako mwenyw kama utayachukua saw kama utak endelea kuuza mboga
 
Comment ya kwanza niliongea yote, na zilizofata hivohvo labda kama unataka ukweli katika njia ya kubembelezwa lkn niliyosema ndo hayo hakuna utaloweza badilisha kuhusu mdog wako na ya kwako mwenyw kama utayachukua saw kama utak endelea kuuza mboga
Hahaha unatumia hisia sana kijana! Unaongea kama umevurugika kidogo, kwahiyo wewe huwezi kumpa mtu ushauri kuhusu masomo akikuomba ushauri unamuacha atajijua mwenyewe! Haya acha nikauze mboga mieee😂
 
Habari wakuu,

Naomba kupata mawazo yenu kuhusu hili. Mdogo wangu amefaulu vizuri kidato cha sita akiwa na combination ya PCB, lakini amepangiwa kusoma chuo kimoja huko Dodoma Bachelor of Commerce in Accountancy katika. Hii kozi hakuichagua kabisa.

Jana kapokea majibu ya mkopo kutoka HESLB na amepewa kiasi cha ada 750,000, ambacho ni sawa na asilimia 97% ya ada kamili.

Nimemshauri kwamba akifika chuoni ajaribu kubadili kozi ili asome nursing badala ya accounts, maana kwa kweli kozi ya accounts haendani kabisa na PCB yake. Yeye anasema afadhali kapata chuo, wengine hawakupata kabisa hadi mwakani hii inaonyesha kwamba wanafunzi ni wengi sana na nafasi chache.

Anadai kuwa ada ya kozi ya nursing ni kama milioni 4.6 sasa swali langu ni:
Kama akibadili kozi kwenda nursing, je ataendelea kuchangiwa kiasi kilekile cha ada (750,000) au inaweza kuongezeka kulingana na kozi mpya?

Zamani waliosoma PCB wakapata daraja la kwanza walikuwa wanaenda moja kwa moja Muhimbili au Bugando, lakini sasa hali imebadilika sana. Hata waliofaulu vizuri wanakosa kozi walizochagua.

Nimewaza nikaishia hapa msaada tafadhali..
MKUU,HUO NI UPUMBAVU MKUBWA KUWAHI KUTOKEA MAISHANI MWAKE.
 
KUBADILI KOZI HAIWEZEKANI,ATAZUNGUSHWA TU,UDOM KUNA UJINGA MWINGI.

PIA,HIYO KOZI KUSOMA ATAJUTIA,HUWEZI KUSOMA PCB UKAENDA UHASIBU.

ATAJUTIA.
Ni st John, hiyo course wala chuo hajaapply huwezi amini.. sijui sikuhizi utaratibu ukoje!
 
Mkuu kwanza kabla hujaanza kuyachokonoa hayo mambo hakikisha uwe na jeuri ya pesa yaani namaanisha endapo atakosa huo mkopo wa kulipia ada ya nursing uwe na uwezo wa kumlipia kwa private,kama hauna huo uwezo muache aendelee kusoma hiyo hiyo kozi aliyochaguliwa vinginevyo utampotezea muda tu atasota nyumbani mwaka mmoja au miwili.
Maisha ya sasa yamebadilika anaweza akasoma hizo kozi za afya na bado asipate ajira.
Muache asome kozi hiyo hiyo atajiongeza mwenyewe mbele ya safari.
 
Vyitu vingine huwa anapanga Mungu, lazima ujiulize mtu kasoma pcb wapi na wapi na account?? Ila Mungu yeye anayeona mbele analo kusudi juu yake! Hoja kwamba kazi zake hamna ni uongo na ni kutengenezeana uoga! Nafasi za kazi zinatangazwa kila siku ni bahati ya mtu tu! Kuna watu wamesomea account na wameajiriwa mishahara yao ni minono sana!

Wakati mimi napply kozi ya kosomea chuo kikuu! Niliapply civil Engineering lakini nilichaguliwa kozi ya mechanical ambayo sikuipenda kabisa, nilienda kusoma basi tu baada ya kushauriwa na watu mbalimbali kuwa yamkini ni Mungu, kweli nilipomaliza tu sijawahi kukaa nyumbani nimefanya kazi taasisi tofouti na kampuni tofauti na kila taasisi na kampuni nilikuwa naajiriwa bila usaili hata kama wametangaza usaili nikituma tu maombi wananipigia simu kwenda kuanza kazi! Sasa hivi nimeajiriwa serikalini moja ya taasisi inayolipa vizuri Tanzania! Na kwenye usaili alihitajika mmoja pamoja na kuwa na wingi wa waomba kazi! Interview kuanzia writen, practical na oral ilikuwa ngumu lakini Mungu alinisaidia nikapata hiyo kazi! Kwa hiyo ndugu wakati mwingine ni mipango ya Mungu.
☕️☕️☕️🍵
 
Yeye alitegemea masomo ya afya lakini ile kuona wengine wamekosa chuo mpaka mwakani akahofia na kuona ata hii alichaguliwa bora japo sio chaguo lake!
Kama ana ufaulu sawa na wengine waliochaguliwa kozi za afya anaweza akafanikiwa lakini inategemea na nafasi.
 
Back
Top Bottom