Seran
JF-Expert Member
- Feb 7, 2025
- 10,540
- 31,598
Habari wakuu,
Naomba kupata mawazo yenu kuhusu hili. Mdogo wangu amefaulu vizuri kidato cha sita akiwa na combination ya PCB, lakini amepangiwa kusoma chuo kimoja huko Dodoma Bachelor of Commerce in Accountancy katika. Hii kozi hakuichagua kabisa.
Jana kapokea majibu ya mkopo kutoka HESLB na amepewa kiasi cha ada 750,000, ambacho ni sawa na asilimia 97% ya ada kamili.
Nimemshauri kwamba akifika chuoni ajaribu kubadili kozi ili asome nursing badala ya accounts, maana kwa kweli kozi ya accounts haendani kabisa na PCB yake. Yeye anasema afadhali kapata chuo, wengine hawakupata kabisa hadi mwakani hii inaonyesha kwamba wanafunzi ni wengi sana na nafasi chache.
Anadai kuwa ada ya kozi ya nursing ni kama milioni 4.6 sasa swali langu ni:
Kama akibadili kozi kwenda nursing, je ataendelea kuchangiwa kiasi kilekile cha ada (750,000) au inaweza kuongezeka kulingana na kozi mpya?
Zamani waliosoma PCB wakapata daraja la kwanza walikuwa wanaenda moja kwa moja Muhimbili au Bugando, lakini sasa hali imebadilika sana. Hata waliofaulu vizuri wanakosa kozi walizochagua.
Nimewaza nikaishia hapa msaada tafadhali..