Kaomba ufafanuzi juu ya hili.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaomba ufafanuzi juu ya hili..

Discussion in 'Jamii Photos' started by TANMO, May 21, 2011.

 1. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Waungwana kutokana na ujio wa hii Teknolojia ya picha nadhani kuna baadhi ya mambo ambayo hayakustahili kuonekana na jamii flani lakini inatokea yanawekwa wazi baada ya picha kupigwa kwenye tukio husika..

  Kwa mfano, kwa mujibu wa utamaduni wa dini ya Kiislamu ni kuwa wanawake hawaruhusiwi kushiriki maziko makaburini. Nilivyoziona hizi picha ndiyo nikapata swali kuwa haiwezekani ikawa tunavunja miiko ya dini kwa kuchukua picha za tukio ambalo kuna watu hawakutakiwa kufahamu jinsi jambo linavyofanyika? (Naomba kueleweshwa juu ya hili)

  Nyingine ni kitendo cha picha za maiti kwenye jeneza zikitundikwa kwenye Blogs, hivi ni sawa kweli au niko nyuma kimaendeleo?

  Rejea hizi picha:
  003.JPG
  001.JPG
  006.JPG
   
 2. blackdog

  blackdog Member

  #2
  May 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  mimi nafikiri upo sawa,kwani chimbuko la dini hiyo (nchi za kiarabu awaonyeshagi picha za makaburini wakati wa tukio la mwisho),
  kwa mawazo yangu elimu ya DINI bado ndogo kwa watu.inatakiwa juhudi ziongeze kuelimisha.
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo mkuu labda tunatumia vibaya Teknolojia kwa kuonesha visivyopaswa kuoneshwa?
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kwani kwenye picha hizi kuna wanawake wanaonekana kwenda huko makaburini? Mimi siwaoni unless wamejibaraguza waonekane kama wanaume!!
   
 5. P

  Percival JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,566
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Hi ni kweli kuchukua picha ya maiti au maziko haina maana ni kuongeza huzuni tu kwa watu.
   
 6. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Chamahani mimi chichemi kitu.
   
 7. L

  Leornado JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Uko sawa kabisa mkuu, sisi jamii ya waafrica hatuna heshima kabisa na miili ya wenzetu waliotangulia mbele ya haki. Sio vizuri kucukua picha za marehemu na kuzisambaza kwenye mablogu, hasa kwa dini ya wenzetu waislamu. Hebu cheki sasa mambo yote hadharani haa watoto wadogo wanajua ni nini kinafanyika. Tuangalia tusijekuwa watumwa wa tekonolojia.

  Mimi huwa najiuliza, how comes mtu unachukua mkanda wa video kwenye mazishi, kuanzia marehemu akiwa kwenye jokofu, anavyosafishwa, valishwa na kisha akiwa kwenye jeneza. What for? hivi mtu ukiangalia mkanda kama huu si ndio kujiongezea machungu?

  Africa tujirekebishe kwenye hili na kupunguza mbwe mbwe misibani.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,280
  Likes Received: 19,432
  Trophy Points: 280
  tunapenda kudandia sana vitu(dini na technology) au tunapenda kumeza tu kila kitu tunacholetewa
   
 9. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama ujui mambo ya dini kaa kimya usitumie akili yako, wewe umeshiona wapalestina wanavyozika???
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa waislam kuzika wazi ndio mafundisho yana sema hivyo... sijui kwa dini zingine
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Mkuu Chatu Dume hoja yetu hapa siyo utaratibu wanaotumia Waislamu kwenye kuzika, bali kitendo cha kupiga picha shughuli ya maziko (ambayo kwa mujibu wa Uislamu, kuna watu ambao hawaruhusiwi kushiriki.. na kama hawaruhusiwi kushiriki, sidhani kama wanapaswa kujua shughuli inavyofanyika)... Kingine ni tabia ya picha za maiti kuwekwa kwenye blog mbali mbali.. Pia kuna mchangiaji amezungumzia kitendo cha kurekodi video mwili wa marehemu na shughuli za mazishi....

  Mapendo.
   
 12. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,785
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  wewe ni muislamu? Pili pili usioila inakuwashia nini? Wenyewe wanaona utaratibu unawafaa, wataubadilishha wakiuona kero? Kwa nini uhoji mambo ya dini za wenzako!
   
 13. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Mkuu umenikusudia mimi?
  Kama jibu ni ndiyo, basi jaribu kunielewa kabla hujaamua kukasirika,,,
  Ninachomaanisha siyo utaratibu wa Waislamu kwenye maziko bali kitendo cha kuchukua picha kaburini..
  And, yes! Mimi ni Muislamu...
   
 14. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mmmh mimi niko nyuma kweli. Nilifikiri umuhimu wa picha ni kutunza kumbukumbu!! Babu na bibi yangu walikufa na kuzikwa kukiwa hakuna tekelinalokujia ya kamera. Hivyo sikuwa na bahati ya kutambua hata walivyokuwa wanafanana. Wakati mwingine hizi picha zinakufanya kuwa karibu na marehemu kwa hisia. Kama marehemu alikuwa na impact kubwa katika maisha yako, naamini hizo picha zinaweza kuongeza chachu katika maendeleo yako.
  Ni maoni yangu tu.
   
 15. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo ndiyo madhara ya maendeleo ya sayansi na teknolojia, hamna jinsi
   
Loading...