Kaoa Mwingine Baada Ya Kumpa Mimba

Kaoa Mwingine Baada Ya Kumpa Mimba

Illuminata Rodgers

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2015
Posts
2,845
Reaction score
2,030
Habari wana jf,mi nina shost yangu huyo shost alikua na jamaa yake ambaye wamedumu miaka 2 katika mahusiano yao jamaa alionesha kumpenda sana shost pia shost alimpenda sana jamaa na kila alichohitaji kwa jamaa jamaa alimpata,basi ikafikia kipind shost akawa anaenda kwa jamaa anakaa hata wiki then anageuza..kuna kipindi shost akashika mimba akampa taarifa jamaa jamaa alifurahi sana na kumjali kukaongezeka ila kwa bahati mbaya mimba haikufika hata miezi miwil ikaharibika akamwambia mpenz wake akampatia hela kwa jili ya kusafishia then mahusiano yakaendelea kama kawaida,baada ya mwez kupta shost akawa akimtumia jamaa sms hajibiw akipiga sim haipokelewi had siku alipojibiwa kwamba jamaa kaoa sababu kuna bint almpa mimba kwa hiyo ukawa msala ikabdi aoe..shost kachanganykiwa sabu aljiwekea asilimia mia moja kwamba jamaa ndo mumewe mtarajiwa,jamaa anadai bado anampenda shost pia shost anadai bado anampenda jamaa,kuna nguo aliziacha kwa jamaa jamaa anadai mkewe alivozkuta akazchoma moto..ushaur jaman afanye nn?
 
Mbona majanga matupu...kunani vijana.??
 
huyo shosti wako ndiye aliyekupa ruhusa ya kuja kumuanika hapa?

anyway,kama bado wanapendana hakuna tatizo,lakini ajiandae kuwa kimada tu maana hamna jinsi!
 
Tatizo lazma lilianzia kwenye hiyo "mimba"
Iliharibika au iliharibiwa??? Kuna ukweli umejificha hapo
 
kama anataka kuendelea kuwa kimada basi asimwache jamaa aendelee nae tu.
 
Kama imani inaruhusu aolewe mke wa pili. Kama imani inakataa basi amsahau huyo bwana
 
Ajitahidi kukubaliana na ukweli,na huyo bwana aachane nae maana kashakua mume wa mtu tayari...yeye aangalie yake wanaume wapo atapata mwingine kikubwa atulie asipaparike kuingia kwenye uhusiano mwingine kwa haraka,ila huyo bwana aachane nae kabisa hata mawasiliano nae akate.
 
Back
Top Bottom