Ngoja nikupe true stori moja ambayo mimi nimeishuhudia labda italeta mwanga sina uhakika kama ina uhusiano na Mada ya Kanye, kuna siku nilikwenda Bagamoyo sasa yule jamaa aliyekuwa anatumbeza kwenye mambo ya kale na kutuelezea mambo ya Kihistoria alikuwa Mzee mmoja wa makamu na dogo mmo hivi kwenye miaka kama 25 hivi, yule dogo mwishoni akasema yafuatayao, ,, aisee bro mimi sielewi ni kwa nini Shuleni tunafundishwa kwamba Utumwa na biashara ya utumwa ilikuwa mbaya hivi hawa akina Michael Jordan, Tupac si ndo watumwa wenyewe hawa,? akaendelea nakwambia bro leo hii ikija Meli ya Kizungu ikatia Nanga hapa na kusema anayetaka kwenda USA na Ulaya kuwa Mtumwa apande nakuhakikishia Meli itajaa", dogo alinifanya nitafakari sana sasa sijui kama ina uhusiano na Kanye, who knows?