Jackal
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 9,559
- 12,681
HONGERA TENA DK. MWELE MALECELA
Dk. Mwele Macelela ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika na kwa hiyo atakuwa mtu wa pili kimamlaka katika Makao Makuu ya Shirika hilo barani Afrika kwa ujumla. Hiyo ina maana kuwa nchi zote za Afrika zitamkimbilia ili kupata mabilioni ya fedha yanayotolewa na WHO kusaidia kuhuisha sekta ya afya.
Mwaka 2016 Uteuzi wa Dk. Mwele Malecela kama Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (National Institute for Medical Research - NIMR) ulitenguliwa na Rais John Magufuli, siku moja baada ya Dk. Mwele kusoma hadharani ripoti iliyoonesha kuwa kuna kina mama wamekutwa na dalili za virusi vya ZIKA nchini Tanzania.
Inadaiwa kuwa kabla hajafukuzwa kazi alikataa shinikizo la kukanusha matokeo ya ripoti kutoka kwa serikali na akaweka msimamo kuwa "masuala ya kitabibu huendeshwa na watalaamu kupitia tafiti na si wanasiasa na siasa."
Pamoja na yote hayo, Dk. Malecela anashikilia rekodi nyingi na kubwa sana. Kwa mfano, Dk. Mwele ndiye mwanamke wa kwanza duniani na mwafrika wa kwanza kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Afya Jamii (IANPHI) taasisi ambayo ni mwamvuli wa taasisi zote za kitaifa za afya kwenye mataifa yote duniani.
Dk. Malecela alijiunga NIMR mwaka 1987 baada ya kuhitimu shahada zake kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM), pia ana Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha London Uingereza mwaka 1995.
Sekta ya Afya nchini Tanzania haitamsahau kwa mchango wake mkubwa kwenye kujenga misingi ya tafiti za afya na hasa usimamizi wake kwenye Mchakato wa Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa vya Tafiti za Afya ambao ulianzishwa mwaka 1999 na baadaye kufanyiwa mapitio mwaka 2005.
J.Mtatiro
=======
UPDATES:
Taarifa za Dkt. Mwele Malecela kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, sio za kweli.
Habari zaidi, soma=>Dkt. Mwele Malecela aula Umoja wa Mataifa. Kuongoza vituo vya magonjwa Afrika
Rais atengua uteuzi wa Mkurugenzi NIMR Dr. Mwele Malecela
Dr. Mwelecele (aka Mwele) Malecela pamoja na Dr. Kigwangala wamechukua fomu ya kugombea Urais wa JMT
Dk. Mwele Malecela ateuliwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa NIMR