(Kanusho) CHADEMA: Zitto ni adui yetu namba moja nchini Tanzania

Status
Not open for further replies.
Kama alitaka kuiua Chadema wakamstukia na kumtema wewe unashauri wamuinguze UKAWA ili aendelee jutoa siri na mikakati ya UKAWA kuiondoa Ccm madarakani?? Kwanini asiendelee na ushirika wake na Ccm?? Kama hawatoshi wako kina TLO, UDP, DOVUTWA MZIRAY na vingine vingi mamluki. Zitto ni sawa na ukoma.
 
Kwani sifa za kuwa UKAWA ni zipi?
Na wanachama hawana haki ya kuhama chama na kujiunga na chama kingine ? Naliza tu!
 
DSC01553.jpg
 
Ukisoma kwa undani gazeti la Mtanzania na kuchambua kauli za Mnyika dhidi ya adui wa CHADEMA kwa sasa utagundua tu hata wao CHADEMA ni pandikizi wa CCM.

Chama makini chenye lengo la kushika dola hakiwezi kutangaza vita dhidi chama pinzani ili kuipa unafuu CCM.

Nionavo mimi adui wa upinzani ni CCM, sasa leo hii Mnyika anapotuambia kuwa adui number moja ni ZZK yaonesha kabisa kuwa upinzani bongo haupo serious.
 
Acha kumlisha mnyika maneno kinywani mwake we kijana
Uaduii wa zitto kwa ustawi wa demkorasia upo wazi na john alisema zitto ni adui wa demokrasia yetu na ni kweli
Sasa ghafla unataka kuigeza cdm kuwa act nenda kijiji kawadanganye
 
Mkuu soma gazeti la mtanzania mkuu ili povu likutoke vizuri.
 
[h=1]Topic: (Kanusho) CHADEMA: Zitto ni adui yetu namba moja nchini Tanzania[/h]
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuwa adui yake namba moja ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and Transparance (ACT-wazalendo), Zitto Kabwe.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha Mwanza juzi, alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutokana na kile alichosema ‘ni adui kwao’.

“Mtume Muhamad (S.A.W) alikuwa anazungumzia unafiki ambao una sura mbili na sifa zake, leo (ACT) wanasema wapo upinzani, wanasema msiunge mkono Ukawa halafu mnawakaribisha?

“Nendeni kila mahali waambieni wananchi adui yetu mkuu ni Zitto. Sikilizeni niwaambie Taifa hili kama ni ufisadi tumeshazungumzia sana kuanzia EPA mpaka Richmond. Dk. Slaa (Willbrod) alipoingia bungeni aliyasema haya kwa sasa si mapya. Adui yetu ni Zitto na hatumtaki Ukawa,” alisema Mnyika.

Alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo Ukawa kwa sababu adui kwao.

Zitto ajibu
Akihutubia mamia ya wananchi wa Mwanza jana, Zitto alisema kadri siku zinavyosonga wabaya wake wamekuwa wakijionyesha.
Zitto alisema pamoja na hali hiyo, ACT-Wazalendo haiko tayari kuzungumzia siasa za wakati uliopita kwa vile kufanya hivyo si afya njema kwa siasa za upinzani.

Alisema ni vema viongozi wa vyama vya upinzani waachane na ugomvi binafsi na watangulize masilahi ya taifa mbele.

“Mwanzo walipotufukuza walituambia tukatafute vyama vingine hilo likafanyika, tulipopata vyama vya kufanyia siasa wakasema vipo kwa ajili ya kugawa upinzani tukasema tupo tayari kuunganisha nguvu ya pamoja kwa ajili ya kuiondoa CCM…wenzetu pia hili hawalitaki sasa ni wajibu wenu kutambua watu gani hawataki kuiondoa CCM,” alisema Zitto.

Alisema wao (ACT) wana nia ya dhati lakini wenzao wanaweka ugomvi binafsi mbele ya masilahi ya taifa.

“Sisi ACT Wazalendo bado tupo tayari kushirikiana kwa mujibu wa misingi. Shabaha yetu ni moja tu, kubomoa mfumo wa uchumi wa kinyonyaji na ufisadi ili kujenga uchumi shirikishi wa wananchi,” alisema na kuongeza:

“Sikufundishwa kugombana na watu barabarani au kusema ovyo mitaani, kufanya hivi hakuna tofauti na kumsema mke au mume mlioachana…mmoja kwa kukosa busara na kwa kuwa aliachana na yule mke anaamua kwenda vijiweni na kutoa siri za mzazi mwenzie, hili kwetu hapana.

“Tunakuja na jahazi jipya ambalo ndugu zangu wa Mwanza nimekuja kuwakabidhi, kubwa tunataka kulirudisha taifa katika misingi yake ya ujamaa na kujitegemea, tunahitaji ujamaa wa demokrasia,” alisema Zitto.

Alisema tafsiri ya ujamaa haina maana kuwa chama hicho kitataifisha mali za watu, bali kitarekebisha makosa ya ubinafsishaji kwa kurejesha mali zote za taifa zilizouzwa na wanunuzi hawajatekeleza mikataba yao.
Mapokezi

Zitto ambaye amefuatana na Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira, waliwasili Mwanza saa 8.00 mchana na kupata mapokezi makubwa yaliyoanzia wilayani Misungwi.

Mapokezi hayo yaliongozwa na vijana waendesha pikipiki (bodaboda) na kikundi cha wanawake ambao muda wote walikuwa katika shamrashara hadi alipoingia kwenye uwanja wa Furahisha.
 
Topic: (Kanusho) CHADEMA: Zitto ni adui yetu namba moja nchini Tanzania

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuwa adui yake namba moja ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and Transparance (ACT-wazalendo), Zitto Kabwe.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha Mwanza juzi, alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutokana na kile alichosema ‘ni adui kwao'.

"Mtume Muhamad (S.A.W) alikuwa anazungumzia unafiki ambao una sura mbili na sifa zake, leo (ACT) wanasema wapo upinzani, wanasema msiunge mkono Ukawa halafu mnawakaribisha?

"Nendeni kila mahali waambieni wananchi adui yetu mkuu ni Zitto. Sikilizeni niwaambie Taifa hili kama ni ufisadi tumeshazungumzia sana kuanzia EPA mpaka Richmond. Dk. Slaa (Willbrod) alipoingia bungeni aliyasema haya kwa sasa si mapya. Adui yetu ni Zitto na hatumtaki Ukawa," alisema Mnyika.

Alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo Ukawa kwa sababu adui kwao.

Zitto ajibu
Akihutubia mamia ya wananchi wa Mwanza jana, Zitto alisema kadri siku zinavyosonga wabaya wake wamekuwa wakijionyesha.
Zitto alisema pamoja na hali hiyo, ACT-Wazalendo haiko tayari kuzungumzia siasa za wakati uliopita kwa vile kufanya hivyo si afya njema kwa siasa za upinzani.

Alisema ni vema viongozi wa vyama vya upinzani waachane na ugomvi binafsi na watangulize masilahi ya taifa mbele.

"Mwanzo walipotufukuza walituambia tukatafute vyama vingine hilo likafanyika, tulipopata vyama vya kufanyia siasa wakasema vipo kwa ajili ya kugawa upinzani tukasema tupo tayari kuunganisha nguvu ya pamoja kwa ajili ya kuiondoa CCM…wenzetu pia hili hawalitaki sasa ni wajibu wenu kutambua watu gani hawataki kuiondoa CCM," alisema Zitto.

Alisema wao (ACT) wana nia ya dhati lakini wenzao wanaweka ugomvi binafsi mbele ya masilahi ya taifa.

"Sisi ACT Wazalendo bado tupo tayari kushirikiana kwa mujibu wa misingi. Shabaha yetu ni moja tu, kubomoa mfumo wa uchumi wa kinyonyaji na ufisadi ili kujenga uchumi shirikishi wa wananchi," alisema na kuongeza:

"Sikufundishwa kugombana na watu barabarani au kusema ovyo mitaani, kufanya hivi hakuna tofauti na kumsema mke au mume mlioachana…mmoja kwa kukosa busara na kwa kuwa aliachana na yule mke anaamua kwenda vijiweni na kutoa siri za mzazi mwenzie, hili kwetu hapana.

"Tunakuja na jahazi jipya ambalo ndugu zangu wa Mwanza nimekuja kuwakabidhi, kubwa tunataka kulirudisha taifa katika misingi yake ya ujamaa na kujitegemea, tunahitaji ujamaa wa demokrasia," alisema Zitto.

Alisema tafsiri ya ujamaa haina maana kuwa chama hicho kitataifisha mali za watu, bali kitarekebisha makosa ya ubinafsishaji kwa kurejesha mali zote za taifa zilizouzwa na wanunuzi hawajatekeleza mikataba yao.
Mapokezi

Zitto ambaye amefuatana na Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira, waliwasili Mwanza saa 8.00 mchana na kupata mapokezi makubwa yaliyoanzia wilayani Misungwi.

Mapokezi hayo yaliongozwa na vijana waendesha pikipiki (bodaboda) na kikundi cha wanawake ambao muda wote walikuwa katika shamrashara hadi alipoingia kwenye uwanja wa Furahisha.

CHADEMA mmefilisika kisera sasa mmegeukia siasa za maji taka na kujadili watu badala ya hoja! Kuna mtu aliwahi kusema katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa anavizia matukio ndio anaibuka, baada ya zoezi la kura ya maoni kusitishwa kwa sasa CHADEMA wamekosa cha kuongelea imebaki Zitto.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom