(Kanusho) CHADEMA: Zitto ni adui yetu namba moja nchini Tanzania

Status
Not open for further replies.

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
CHADEMA wamevunja ukimya na kuweka bayana kwamba kwa sasa hapa Tanzania adui yao namba moja ni kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo, ndugu Zitto Zuberi Kabwe.

Hayo yamesemwa na Mnyika akiwa kwenye mikutano yake anayoendelea nayo kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Mnyika kaenda mbali zaidi na kusema kamwe hawezi kumkaribisha Zitto kwenye umoja wao unaotambulika kama UKAWA.

Wakati Mnyika akisema hawezi kumkaribisha Zitto UKAWA wenzake wa CUF wao wamesema wanamwita Zitto kujiunga nao kwenye harakati za ukombozi wa taifa hili.

Ngoma ndiyo kwanza inaanza kunoga yetu macho na masikio ngoja tuone nani mwanaume na nani ni mvulana kati ya Mnyika na Zitto.
=========================



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuwa adui yake namba moja ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and Transparance (ACT-wazalendo), Zitto Kabwe.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha Mwanza juzi, alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutokana na kile alichosema ‘ni adui kwao'.

"Mtume Muhamad (S.A.W) alikuwa anazungumzia unafiki ambao una sura mbili na sifa zake, leo (ACT) wanasema wapo upinzani, wanasema msiunge mkono Ukawa halafu mnawakaribisha?

"Nendeni kila mahali waambieni wananchi adui yetu mkuu ni Zitto. Sikilizeni niwaambie Taifa hili kama ni ufisadi tumeshazungumzia sana kuanzia EPA mpaka Richmond. Dk. Slaa (Willbrod) alipoingia bungeni aliyasema haya kwa sasa si mapya. Adui yetu ni Zitto na hatumtaki Ukawa," alisema Mnyika.

Alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo Ukawa kwa sababu adui kwao.

Zitto ajibu
Akihutubia mamia ya wananchi wa Mwanza jana, Zitto alisema kadri siku zinavyosonga wabaya wake wamekuwa wakijionyesha.
Zitto alisema pamoja na hali hiyo, ACT-Wazalendo haiko tayari kuzungumzia siasa za wakati uliopita kwa vile kufanya hivyo si afya njema kwa siasa za upinzani.

Alisema ni vema viongozi wa vyama vya upinzani waachane na ugomvi binafsi na watangulize masilahi ya taifa mbele.

"Mwanzo walipotufukuza walituambia tukatafute vyama vingine hilo likafanyika, tulipopata vyama vya kufanyia siasa wakasema vipo kwa ajili ya kugawa upinzani tukasema tupo tayari kuunganisha nguvu ya pamoja kwa ajili ya kuiondoa CCM…wenzetu pia hili hawalitaki sasa ni wajibu wenu kutambua watu gani hawataki kuiondoa CCM," alisema Zitto.

Alisema wao (ACT) wana nia ya dhati lakini wenzao wanaweka ugomvi binafsi mbele ya masilahi ya taifa.

"Sisi ACT Wazalendo bado tupo tayari kushirikiana kwa mujibu wa misingi. Shabaha yetu ni moja tu, kubomoa mfumo wa uchumi wa kinyonyaji na ufisadi ili kujenga uchumi shirikishi wa wananchi," alisema na kuongeza:

"Sikufundishwa kugombana na watu barabarani au kusema ovyo mitaani, kufanya hivi hakuna tofauti na kumsema mke au mume mlioachana…mmoja kwa kukosa busara na kwa kuwa aliachana na yule mke anaamua kwenda vijiweni na kutoa siri za mzazi mwenzie, hili kwetu hapana.

"Tunakuja na jahazi jipya ambalo ndugu zangu wa Mwanza nimekuja kuwakabidhi, kubwa tunataka kulirudisha taifa katika misingi yake ya ujamaa na kujitegemea, tunahitaji ujamaa wa demokrasia," alisema Zitto.

Alisema tafsiri ya ujamaa haina maana kuwa chama hicho kitataifisha mali za watu, bali kitarekebisha makosa ya ubinafsishaji kwa kurejesha mali zote za taifa zilizouzwa na wanunuzi hawajatekeleza mikataba yao.
Mapokezi

Zitto ambaye amefuatana na Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira, waliwasili Mwanza saa 8.00 mchana na kupata mapokezi makubwa yaliyoanzia wilayani Misungwi.

Mapokezi hayo yaliongozwa na vijana waendesha pikipiki (bodaboda) na kikundi cha wanawake ambao muda wote walikuwa katika shamrashara hadi alipoingia kwenye uwanja wa Furahisha.

Chanzo: Mtanzania

Kanusho la Mnyika
attachment.php
 
Si rahisi kula pamoja na YUDA na ukabaki salama maana dhambi hiyo haimtoli mtu mpaka afe.
 
Chadema wamevunja ukimwa na kuweka bayana kwamba kwa sasa hapa tanzania adui yao namba moja ni kiongozi mkuu wa ACT ndugu zitto zuberi kabwe,

Hayo yamesemwa na mnyika akiwa kwenye mikutano yake anayoendelea nayo kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini,

Mnyika kaenda mbali zaidi na kusema kamwe hawezi kumkaribisha zitto kwenye umoja wao unaotambulika kama ukawa,

wakati mnyika akisema hawezi kumkaribisha zitto ukawa wenzake wa cuf wao wamesema wanamwita zitto kujiunga nao kwenye harakati za ukombozi wa taifa hili,

Ngoma ndiyo kwanza inaanza kunoga yetu macho na masikio ngoja tuone nani mwanaume na nani ni mvulana kati ya mnyika na zitto.

Chanzo; gazeti la mtanzania la leo tarehe 20/4/2015.

Post za kijinga za MACCM ZINAVUMILIWA. MSEME ZITTO UONE ZITACHOMOLEWA HARAKA.
 
Niliwaambia..kwenye msingi wa CHADEMA, Zito alikuwa ni jiwe kuu la pembeni (Cornerstone)!

chadema wameshikwa pabaya sana na zitto mwaka huu watapata shida sana zitto anawajua pamoja na mapungufu yao yote.

AKILI YAKO IKIKUAMINISHA YA KWAMBA HUWEZI SONGA MBELE BILA YA ZITTO HAKIKA fahamu unatatizo KUBWA KUPINDUKIAPL

mnyika nadhani hamjui zitto ntacheka sana mwaka huu mnyika atakula mweleka wa ajabu sana.

Chama cha wasaliti kinatetewa na wafuasi wa CCM MITANDAONI.
 
......wakati mnyika akisema hawezi kumkaribisha zitto ukawa wenzake wa cuf wao wamesema wanamwita zitto kujiunga nao kwenye harakati za ukombozi wa taifa hili,.....
Chanzo; gazeti la mtanzania la leo tarehe 20/4/2015.
CUF ni Chama kilichopitia misukosuko mingi kuliko vyama vingine vyote vya upinzani.

Mwacheni Zitto ale pesa za wanyonge, lakini CUF na Ukawa hatakaa atie mguu.
 
Unapopachika maneno ya uwongo kwenye story yako jaribu kupachika maneno yanayofanana na ukweli hata kidogo, CUF wamemkaribisha Zitto lini mtu ambaye chama chake kimeweka bayana kuwa kitaisambaratisha CUF katika ukanda wote wa pwani, kwa hiyo CUF wamemkaribisha Zitto ili akawasambaratishe vizuri?.
 
Unapopachika maneno ya uwongo kwenye story yako jaribu kupachika maneno yanayofanana na ukweli hata kidogo,CUF wamemkaribisha Zitto lini mtu ambaye chama chake kimeweka bayana kuwa kitaisambaratisha CUF katika ukanda wote wa pwani,kwa hiyo CUF wamemkaribisha Zitto ili akawasambaratishe vizuri?.
mkuu umelipata gazeti la leo la mtanzania lakini watu wabishi hata kama hajui anachokibishania soma mtania mkuu usiropoke tu unatia aibu mtu mzima.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom