Kanuni ya Kubadili Fikra: Kanuni ya 8 ya Akili na Ulimwengu

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,221
Kanuni ya Ubadilishaji (Substitution)

Ubadilishaji wa fikra.



Hii ni kinuni mojawapo ya saikolojia inayohusu sana kubadili fikra, mazoea, hisia na mawazo. Kanuni inasema kuwa vyote hivyo havibadilishwi kwa kulazimisha kuvitoa au kwa kulazimisha kuvikubali bali unaweza kubadilisha mtazamo wako kwa kuweka ufahamu wako na umakini wako katika aina nyingine ya mawazo, uelewa n.k unaotaka kuelewa na kubadilisha uhalisia wa zamani.

Huwezi kubadili tatizo kwa ufahamu ule ule ulioutumia kutengenezea tatizo hilo.
Watu wengi wamekuwa hawafahamu jinsi ya kupambana na mazoea na hali tulizojizoesha. Ni vigumu sana mtu kupambana na udhaifu wake hasa aliouendekeza mwenyewe. Lakini kanuni hii ni simple kabisa kwani inatufungua kuwa hatuwezi kubadili tatizo kwa ufahamu tulioutumia kutengenezea tatizo hilo. Ndio maana kukiwa na tatizo tunaamua kutafuta chanzo chake, tunapotafuta chanzo cha tatizo ni sawa na kubadili ufahamu wetu kuwa bora zaidi ya ufahamu ule uliotengeneza tatizo hilo bila kufahamu matokeo yatakuwaje.

Hivyo vilevile kwenye kutoa aina ya mawazo na kuweka aina nyingine ni kitendo cha kubadilisha mtazamo wetu na msisitizo wetu kwenye aina nyingine ya ufahamu na wazo kisha lile wazo la zamani linatoka lenyewe bila kipingamizi.



Kama umesoma sheria zilizopita najua utakuwa umeshaelewa ni kwanini ni muhimu mtu kuwa makini na mawazo na fikra yake. Kuna sheria moja ilikuwa inasema kuwa chochote unachokipa umakini wako au concentration kinakua katika uhalisia wako. Hivyo ukiwa unajaribu kupambana na fikra fulani uliyojizoesha au mazoea au aina fulani ya uelewa sio kupambana nayo kwa kuiwaza sana na kuiruhusu uendelee kuumbika akilini bali ni kwa kuweka concentration katika hali nyingine,, nayo taaratibu itakua na ile fikra, mazoea au tabia ya zamani yenyewe itaondoka. Ni kama maajabu lakini hii ni kanuni ya muhimu sana.

Unaweza ukawa umeshafunguka kufahamu ni kwanini ni muhimu watu wanashauriwa kuwaza mawazo chanya na sio hasi. Lengo ni kwasababu wengi wana tabia ya kuyapa nafasi mawazo hasi zaidi ya chanya.

FANYA MAJARIBIO.
Jaribu kujitazama kwa undani zaidi (kutafakari), je kuna aina gani ya mawazo ambayo sio mazuri yanayokutawala akilini bila wewe kuyapenda? Labda ni kutokana na kujizoesha, kutojua kuwa unajizoesha au kwa kurudia rudia mazoea hayo sana na sasa imekuwa ngumu ku control. Ukichunguza jizoeshe kujitazama kama unaweza kuyaondoa. Utagundua ukiyafikiria zaidi nayo yanakua. Ukitaka kuondoa mawazo hayo usiweke concentration au umakini kwenye kuondoa bali weka umakini kwenye kuzoesha aina nyingine ya fikra na ufahamu na izoeshe kama ulivyozoesha hali usiyoipenda. Taaratibu utaona ile hali mpya inaanza kuchukua sura nyingine katika ulimwengu wako zaidi ya ile uliyopunguza kuipa nafasi.

Sheria hii kikawaida ni sawa na mtu kupenda kitu fulani au hali fulani na baada ya muda akijizoesha kupenda hali nyingine au kitu kingine utaona anakipa kipaumbele zaidi ya zamani. Unaweza ukawa hata ujajijua lakini ukijichunguza utajijua kuwa upo hivyo ..

Kufahamu hilo ni vyema sana kwani inatupa nafasi kuwa makini na uelewa wetu, mawazo yetu, na fikra yetu kwani kwa kubadilisha hivyo tunabadilisha na maisha yetu.



Pia utagundua kuwa meditation/taamuli ni njia nzuri sana katika kujizoesha kuongoza ufahamu wako na mawazo yako pale unapotaka wewe. Meditation inafundisha mtu kutazama kinachoendelea ndani yake, ndani ya ufahamu wake. Na pale akili inapotulia na kujifunza kuiweka katika sehemu moja inakuzoesha kuiongoza akili yako hasa pale inapotawaliwa na aina mbalimbali za mawazo na hisia. Unakuwa kama farasi pori mwenye nguvu na uhuru wa kwenda popote.

 
Etcetera

Nashukuru sana Etcetera. Karibu sana na tuzidi kufahamu zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Akili n Shamba kubwa sana. Ndan ya shamba hilo tunaweza kupanda chochote na tukakitunza na kikakuwa na kuleta matokeo tuyatakayo.
Lakin pia katika shamba hilo tunaweza tukachimba na kuibuka na dhahabu pamoja na vitu vingine vya thamani.

Shamba Lenye Rutuba(Akili) na linalopata maji kwa wakati tunaita shamba hai, ikiwa na maana haliwezi kuacha kuotesha mmea, ikiwa mkulima(mimi na wewe)Hatutaotesha kile tutakacho basi yataota magugu na majani kwenye shamba(akili).

Akili haiwezi kukaa Idle ukikosa cha kuwaza itawaza itakacho chochote pasi kupingwa na wewe au mimi.
Apollo
 
Apollo nikurudishie nini bwana ama nikupe Linda? Sio kwa kuniingia huku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom