GRAMAA
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 1,155
- 3,399
Juhudi bila ya kufuata sheria na kanuni za juhudi hizo ni kujitesa tu.
Vijana wengi wanapambana sana usiku na mchana kufanya Biashara mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi ila waliowengi wanatoka patupu. Zaidi wanaambulia madeni mazito sana na kufilisiwa.
Jamani ndugu zanguni jitahidini mtoke kwenye huo usingizi mzito mliolala wa kuamini utafanikiwa kibiashara kwa bahati na juhudi binafsi.
Jamani eee biashara ni zaidi ya mtaji ulionao,ubora wa bidhaa ulionao au eneo zuri ulilofungua biashara hiyo.
Biashara ni roho yenye uhai hivyo basi ili unfanikiwe inabidi ujue na uzingatie sheria na kanuni za roho hai ya biashara.
Kama unafanya Biashara bila ya kujua hili basi ndugu yangu hutoboi ng'oooooo hata ufanye nini. Yaani hata uwe na frem kariakoo bila ya kufuata sheria za roho hai ya biashara huchomoki dogo.
Aisee hivi unajua kama biashara nayo inapenda,inachukia,inafurahi,inaumwa,inaiba,inalala,inapumzika,inatamaa,inamawazo n.k. Yaani naomba nieleweke sizungumzii mfanyabiashara ninazungumzia Biashara yenyewe.
Sasa ngoja nikusanue kidogo ili akili ikukae sawa. Wengi mmefungua biashara zenye roho zifuatazo ndio maana hamtoboi
i/ Biashara yenye roho ya chuki. Sifa ya biashara hii inakuwa inakuchukua sana wewe uliyeifungua. Kila ukipambana kuiweka sawa inagoma. Biashara haikupendi inakuchukia kinoma ila wewe unakaza tu bila kujielewa. Sanuka dogo unapoteza muda bure.
ii/ Biashara yenye roho ya wizi. Watu wengi sana humu mmefungua biashara zenye roho ya wizi ndiyo maana mnaibiwa sana mitaji yenu na biashara hizi. Kila ukiwekeza mtaji wako kwenye biashara, biashara inakuibia mtaji wote. Kazi yako inakuwa kila mara ni kuongeza mtaji kila siku. Daaah huruma sana.
iii/ Biashara yenye roho ya utasa. Biashara ina miaka kibao haizai. Wengi mnabiashara zenye roho ya utasa. Yaani kila ukipambana biashara haizai kabisa. Unashindwa kuelewa kuwa biashara yako ni tasa unaendelea kukomaa kizembe tu. Duuuuuh poleni sana.
.
iv/ Biashara yenye roho ya tamaa. Kijana kama Biashara yako inaroho ya tamaa huchomoki mzee. Biashara zenye roho ya tamaa ni mbaya sana na zinawafirisi wengi sana hapa duniani. Ukiona biashara inakumalizia hela na sio kukuingizia hela hiyo biashara inatamaa achana nayo haraka sana
v/ biashara yenye roho ya ukorofi na utovu wa nidhamu. Ukifungua biashara hii kila siku utakuwa unashinda kwa mwenyekiti wa mtaa au polisi kutatua kesi zinazosababishwa na biashara yako uliyoifungua. Mara gari yako ya biashara imegonga mtu,Mara ukuta wa mgahawa wako umedondokea wateja na mengine mengi. Hahahahaa balaa sana
vi/ Na mengine mengi
Sasa kutatua yote haya ni kazima urudi kwenye sheria za roho hai za biashara ambazo kwa bahati mbaya wanazifahamu watu wachache sana na zinabaki kuwa siri kwa watu wachache sana.
Sanuka wewe ili utoboe acha ujuaji.