Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,342
- 8,267
1. Tai huruka peke yao na kwenye anga la Juu - Hawaruki na shomoro, kunguru na ndege wengine wadogo.
MAANA - Kaa mbali na watu wenye mawazo finyu, wale wanaokuangusha. Tai huruka pamoja na Tai. Weka ushirika mzuri na Tai wenzako.
2. Tai wana maono sahihi - Wana uwezo wa kuzingatia kitu kilicho umbali wa kilomita 5. Haijalishi vizuizi, tai hatabadilisha uelekeo wake kutoka kwenye windo lake hadi atapolinyakua.
MAANA - Kuwa na maono na bakia kuwa makini bila kujali vikwazo na utafanikiwa.
3. Tai hawali vitu vilivyokufa - Wanakula tu mawindo mapya.
MAANA - Usitegemee mafanikio yako ya zamani, endelea kutafuta mipaka mipya ya kushinda. Acha zamani zako panapostahili, zamani.
4. Tai hupenda dhoruba - Mawingu yanapokusanyika, tai husisimka, tai hutumia upepo wa dhoruba kujiinua juu. Mara tu anapopata upepo wa dhoruba, tai hutumia dhoruba kali ili kujiinua juu ya mawingu. Hii inampa tai fursa ya kuteleza na kutuliza mbawa zake. Wakati huo huo, ndege wengine wote hujificha kwenye matawi na majani ya mti.
MAANA - Zikabili changamoto zako kwa kujua kuwa hizi zitakufanya uwe na nguvu na bora kuliko ulivyokuwa. Tunaweza kutumia dhoruba za maisha kupanda hadi juu zaidi. Waliofanikiwa hawaogopi kupanda katika kimo kirefu zaidi. Waliofanikiwa hawaogopi changamoto, badala yake wanazifurahia na kuzitumia kwa faida.
5. Tai hujitayarisha kwa mazoezi - Huondoa manyoya na nyasi laini kwenye kiota ili watoto wapate tabu katika maandalizi ya kuruka na hatimaye huruka wanaposhindwa kuvumilia kukaa kwenye kiota.
MAANA - Liache eneo lako la faraja, hapana ukuaji hapo.
6. Tai anapozeeka - Manyoya yake huwa dhaifu na hayawezi kumfikisha haraka juu kama inavyotakiwa. Hii humfanya kuwa dhaifu na inaweza kumfanya afe. Hivyo hupumzika mahali ambapo ni mbali katika milima. Akiwa huko, hung'oa manyoya dhaifu.