CARDLESS
JF-Expert Member
- Apr 2, 2017
- 7,786
- 15,732
Wanabodi habari za siku
Nimekaa nikaangalia namna nchi yetu tunavyoendesha Chaguzi zetu hasa huu Uchaguzi mkuu, na zaidi hapo kwenye Urais.
Urais ni level kubwa sana ya Kiutawala na Uongozi nchi hii na karibu nchi zote Duniani. Rais hatakiwi kupatikana kirahisi rahisi tu.
Mchakato wa kumpata Rais lazima uwe mchakato mgumu wenye lengo la kumpata Rais halisi na anayekubalika na Wananchi wake.
Nchi yetu hii, ina taratibu moja mbovu sana kwenye kumpata Rais.
Sheria yetu ya uchaguzi inatamka kuwa MSHINDI WA KITI CHA URAIS NI YULE ALIYEPATA KURA NYINGI KATIKA UCHAGUZI MKUU.
Sheria hii ni mbovu na imepitwa na wakati. Kwenye nchi yenye Mikoa 31 na Makabila 120+ Rais apatikane kwa wingi wa kura tu?
Ikitokea mimi nimegombea Urais na nikaamua sasa nipige kampeni mikoa 10 tu yenye wapiga kura wengi, na nikapata kura za kuwazidi wengine itakuwa haki? Yaani Rais awe amepata kura kutoka zone fulani tu na bado awe Rais wa Tanzania nzima kisa amepata kura nyingi?
Kwa Dunia ya leo, nashauri Sheria hii ifutwe na uwekwe utaratibu mpya sasa, utaratibu huu uwe kama ifuatavyo.
1. RAIS ANATAKIWA KUPATA 50%+ 1 YA KURA HALALI ZOTE.
2. RAIS ANATAKIWA KUPATA ANGALAU 40% YA KURA KATIKA KILA MKOA KWA MIKOA 20 KATI YA 26 YA TANZANIA BARA + 25% YA KURA ZOTE ZA ZANZIBAR.
IKITOKEA HAKUNA MGOMBEA ALIYEFIKISHA VIGEZO HIVYO, UCHAGUZI URUDIWE KWA DURU YA PILI KWA WALE WAWILI WA JUU.
Utaratibu huu utatupatia Rais anayekubalika katika Eneo kubwa la nchi yetu. Hivyo kuondoa uwezekano wowote wa kupata Urais Kupitia, Ukanda, Ukabila, Dini au hata Matumizi makubwa ya Fedha.
Urais uwe mgumu mtu kupata, ili kuleta ufanisi, kwa sasa ni rahisi mjinga mmoja kushinda uchaguzi kwa kutumia Ukanda au Dini.
Nawasilisha wadau.
Pascal Mayalla
Mohamed Said