Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Sasa umma wa Tanzania unafahamu kuwa watajwa hapo juu ambao walitia nia kugombea Ubunge kwenye majimbo mbalimbali hapa nchini. Katika kura za maoni zilizoendeshwa hapo jana ndani ya CCM, wote hao wamezidiwa kwenye kura za maoni kwenye Majimbo yao: wengine wameachwa mbali sana na wengine wamepitwa kiasi kidogo.
Kwa mujibu wa Kanuni 'mpya' za kiuchaguzi ndani ya CCM kadiri ninavyozifahamu, makabrasha ya waliopigiwa kura za maoni yatawasilishwa Kamati Kuu kwa ajili ya uamuzi kufanyika. Kamati Kuu ndiyo itakayoamua juu ya mgombea halisi wa Jimbo lolote la kiuchaguzi kwa tiketi ya CCM.
Naamini, bado akina Dr. Mwakyembe wana imani ya kuwa wagombea. Wana imani ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM itakayoketi kuamua chini ya Rais Magufuli. Kama ilivyowahi kushuhudiwa huko nyuma (kama ilivyotokea kwenye lililokuwa jimbo la NZEGA mwaka 2010 ambapo mshindi wa tatu Dr. Kingwangala ndiye aliyeteuliwa akiachwa Bashe na Selelii).
Kura za Maoni za jana na leo zinatoa tu sura na dalili za ushindi kwa wanaoongoza Majimboni. Si kura za kuhitimisha. Kamati Kuu bado yaweza kuteua kinyume na matarajio ya wengi. Kamati Kuu, hakika, inabaki kuwa tumaini pekee la washindwa wa jana na leo.